Monday, June 25, 2012

mwanafunzi wa saut jijini mwanza ajishindia bajaj promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo

Mariam Karumba (mwenye blauzi ya bluu) ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Jijini  Mwanza akiwa na wanafunzi wenzake wakifurahia muda mfupi baada ya kukabidhiwa pikipiki aina ya bajaji aliyoshinda kupitia promosheni ya "vumbua hazina chini ya kizibo" inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Kanda ya Ziwa, Patrick Kisaka (kushoto) akikabhi funguo za bajaj kwa Mariamu Karumba,mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT)  ambaye ni mshindi wa pikipiki aina ya bajaj ambayo ameshinda kupitia promosheni ya "vumbua  hazina chini ya kizibo"inayoendeshwa na kampuni hiyo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Kanda ya Ziwa, Patrick Kisaka (kulia) akitoa maelezo mafupi muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki aina ya bajaj kwa Mariam Karumba,mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT)  ambaye ni mshindi wa promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo inayoendeshwa na kampuni hiyo.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.