Friday, June 29, 2012

MABONDIA WAAHIDIWA BAISKELI

Mabondia wa klabu ya mazoezi ya bigright ya mwananyamala  wameahidiwa
baiskel na katibu kata wa vijana wa CCM kinondoni REHEMA MBEGU ili ziwasaidie kwenda mashuleni mwao na mazoezini,Rehema mbegu mara nyingi
huwa yupo karibu sana na vijana hao katika ushauri na kuwasaidia
chakula na vinywaji wakati wakijiandaa na mashindano mbalimbali ,safari hii ameamua kutoa baiskeli ili  kuhamasisha ushindani zaidi na
kuwapa moyo vijana kupenda zaidi michezo kuliko vijiwe.

Baada ya kuhakikishiwa kuwa kila bondia atakae shinda toka klabu ya
ngumi ya bigright atazawadiwa baskeli,wameahidi kukatika mikono
ulingoni yaani ni lazima washinde na wamebadilisha mfumo mzima wa
mazoezi,kwa sasa wapo pamoja,kikambi zaidi nyumbani kwa kocha wao
Ibrahim bigright na kuongeza muda zaidi wa mazoezi kwa sasa wanafanya
mara tatu hadi nne kwa siku.

Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo
ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele toka
kambi ya matumla katika uzani wa fly,Mwaite juma toka bigright boxing
atapigana na mkongwe Anthony Mathias katika uzani wa bantam.

Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa kati ya JUMA
FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo toka kambi ya mzazi

mapambano hayo yameandaliwa na kaike siraju na kusimamiwa na TPBO

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.