Saturday, May 5, 2012

Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais wafanya usafi mji wa forodhani leo

 Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo wameshiriki katika kazi za usafishaji  wa mji katika eneo la Forodhani Mjini Zanzibar.

Utaratibu huo ni uzinduzi wa kazi za Usafi unaoongozwa na Baraza la Manispaa hapa  Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mikakati yake yakushajiisha Wananchi juu ya Usafi katika sehemu za Mjini na Nyenginezo.

Akielezea juu ya uzinduzi wa Usafi huo, Mkurugenzi wa Baraza la
Manispaa Zanzibar Rashid Ali  amesema kuwa Kazi hiyo ya usafi kwa sehemu za Mjini na nyengineze itakuwa ikifanyika kila mwanzoni mwa mwezi kwa siku  ya Jumaamosi.

Amesema kuwa kazi hiyo itakuwa endelevu na sio ya zima moto na
Jumaamosi ijayo itakuwa  kwa kila Nyumba ,Wadi na Shehia kufanya usafi na wao  watakuwa na Wajibu wakukusanya Taka hizo  ili wazipeleke kunakohusika kwa kuzitupa.

Aliendelea kusema kuwa Jumaamosi nyengine kazi hiyo itaendelea tena hiyo  ambapo watalazimika kufunga baadhi ya  Nija kuanzia saa12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Nae Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwinyiussi Abdulla kwa niaba ya Waziri Dkt Mwinyihaji Makame amesema kuwa Madhumunui ya Ofisi hiyo kuanzisha utaratibu huo wakufanya usafi kila siku ya Jumaamosi ya wanzoni mwa mwezi ni kuwashajiisha Wananchi kuona kuwa kazi hiyo si ya Baraza la Manispaa tu bali ni ya kila mtu.

Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu   pale alipo kuungana na Serikali katika kazi hiyo ya kufanya usafi kwani ni kwa faida ya mtu mwenyewe na Taifa kwa ujumla,

Katika uzinduzi huo Maofisa mbali mabli katika ofisi hiyo walishiriki
katika kazi za usafi wakiwamo Manaibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Masheha pamoja na Wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali ziliomo katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

IMETOLEWA NA IDARA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
5/5/2011

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.