Monday, January 30, 2012

TAARIFA YA MSIBA WA SAID TAMIMU ALLY


Ndugu zangu
TAARIFA YA MSIBA WA SAID TAMIMU ALLY 
Ningependa kuwajulisha kuwa  Tamimu amefariki dunia Usiku wa kuamkia Jumapili  na mazishi yalifanyika jana saa kumi jioni makaburi ya Tabata Segerea. 

Natoa shukrani zangu za dhati na kwa niaba ya familia ya ndugu Said Tamimu Ally. 
Nashukuru sana kwa wote waliotoa michango yao ya mali na hali kwa ajili  ya kuokoa maisha ya  ndugu yetu Tamimu.Shukrani pekee ziwaendee ndugu walioko UK, USA Norway, Canada Muscat, Dar es salaam,Tabora, Arusha na sehemu nyinge nyingi  kwa msaada wao wa hali na mali ikiwemo ushauri na kutoa pole.


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

kwa ndugu, jamaa marafiki na woote walioguswa na msiba huu, nawapa POLE, kwa wakati huu mgumu ambao ndugu yetu kisharudi kwa mola wake sina la kusema zaidi ya kusema INNA LLILLAH wa INNA ILLAH RAJEOUN, BAKI ALLAH, POLENI SANA.

sisi sote ni wa Mungu na marejeo yetu ni kwake mungu amrehemu ndugu Said

Hakika huu nim mtihani;Mwenyezi Mungu ni mkubwa,'hakika sisi ni milki ya Allah na hapana shaka kwake tutarejea'