NAFASI ZA KAZI
Mambo PUBLISHERS ni wachapishaji na wauzaji wa vitabu mbalimbali vya ziada na kiada.
Tunatangaza nafasi za kazi ya uwakala wa usambazaji vitabu vyetu kwa wateja wetu waliopo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI.
1. Umri miaka 18 hadi 45. 2. Elimu kidato cha nne , cha sita na kuendelea.2. Awe smart ( maridadi ) na anayejituma kazini.
3. Awe tayari kufanya kazi katika kituo chochote cha kazi atakacho pangiwa kilichopo ndani ya wilaya anayo ishi.
4. Awe na uwezo wa kununua kwa bei ya jumla kuanzia vitabu kumi na kuendelea kwa ajili ya kuvisambaza kwa wateja wetu mbalimbali waliopo katika eneo ama kituo atakacho pangiwa.
5. Awe na uwezo wa kuandika na kuongea kwa ufasaha lugha za Kiswahili na kiingereza.
6. Akiwa na uzoefu wa kazi ya usambazaji vitabu, magazeti, majarida au bidhaa yoyote ile, itakuwa ni sifa ya ziada itakayo muongezea nafasi ya kupata kazi hii.
MAJUKUMU YA KAZI
Kwa mwombaji atakaye pata nafasi hii ya kazi atakuwa na majukumu yafuatayo :
Kununua vitabu kutoka ofisini kwetu, kiwandani au kwa wakala wetu kwa bei ya jumla na kuvisambaza kwa wateja wetu waliopo katika maeneo yaliyo karibu na kituo chake cha kazi.
Tuma barua yako ya maombi ya ukiambatanisha na C.V yako kwenda kwa :
Managing Director ,
Mambo PUBLISHERS
S.L.P 35967
Dar es salaam
TUNAPOKEA MAOMBI KUTOKA KWA WAOMBAJI KUTOKA KATIKA WILAYA ZOTE ZA TANZANIA BARA NA VISIWANI.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05 FEBRUARI 2012 , kazi kuanza tarehe 13 FEBRUARI 2012. Watakao timiza vigezo vya maombi ndio watakao itwa ofisini kwa ajili ya usaili.








Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment