Thursday, June 30, 2011

HOTUBA YA Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora. 2011/2012

 NA NAFISA MADAI
KUTOKA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kupandisha kima cha chini
cha mishara kwa asilimia 25. Aidha  kwa upande wa wale wafanyakazi  wa kima ambacho wanaendelea na utumishi wao pamoja na wale wa ngazi nyengine, mbali na kurekebisha
mishahara yao kwa mujibu wa ngazi zao zqa mishahara yao itakuwa na
ziada itakayozingatia elimu na muda wa utumishi wao kazini.

Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya rais, utumishi wa umma na
utawala bor Mhe Haji Omar Kheri wakati alipokua akiwasilisha Hakadirio
ya mapato na matumizi ya  ofisis yake katika kiako cha baraza la
wawakilishi  mbweni nje kidogo wa mji wa zanzibar.

amesema kuwa upandishaji huo wa  mishahara umezingatia pia nyongeza
walizozikosa wafanya kazi tokea mwaka 2007,ingawa hakutokuwa na
malimbukizo  yaani AREA

Mh kheiramesema  kwa kuzingatia ufinyu wa bajeti utekelezaji wa
mabadiliko hayo ya mishahara mipya bil ya malimbkizo utafanywa kuanzia
mwezi wa octoba 2011. Aliendelea kwa kusema upandishaji jhuo wa mishahara umekwenda sambamba na Ahadi za Rais wa Awamu ya saba Dk Ali Mohd Shein  katika kampeni za
kuomba ridhaa ya kuongoza nhini aliahidi kupitia ilani ya uchaguixi ya
CCM kuimarisha mazingirz bora ya kazi na maslahi ya watumishi wa umma
serikalini.

Aidha alisema rasilimali watu ni nyezo muhimu katika kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa sera na mipango mabalimbali ya kitaifa inapiga hatua. 
Hata hivyo  waziri huyo ailsema katika kuzingatia hilo Serikali imekua
ikichukua hatua  mbalimbali za kuwaendeleza kielimu na maslahi kwa
wafanya kazi wake.

Akizungumzia Utalawa Bora Mhe Kheri amesema ilani ua uchaguzi
inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja
wa Kitaifa ibara ya 186 imeweka msisitizo wa kusimamia utawala bora
nchini kwa kuimarisha demokrasia  pamoja na kulinda hai za binadamu.

Wizara  ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeomba
idhinishiwe jumla ya shiling bilion 4,855,246,000=/ kwa mwaka wa fedha
2011/2012 kwa ajili ya matumizi ya ofisi hiyo.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

 
Nafasi Ya Matangazo