728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, June 19, 2011

  kundi la Underzone ndio kinara wa Serengeti dansi la fiesta 2011 usiku huu.

   Hili ndilo kundi liloshinda fainali za msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti 2011.liitwalo UnderZone kutoka jijini Dar,katika fainali hizo ambazo zilijumuisha makundi mengine kutoka mikoa kadhaa ikiwemo Mwanza,Zanzibar,Tanga,Arusha,Morogoro pamoja na Tanga na kilele ya fainali hizo zilikuwa usiku huu ndani ya ukumbi wa New Maisha Club,jijini Dar.
  Pichani ni Kundi la Underzone kutoka jijini Dar es Salaam likishangweka vilivyo usiku wa leo mara baada ya kufanikiwa kunyakuwa ushindi murua kabisa wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2011, lililofanyia Maisha Club jijini Dar es Salaam,kundi hilo limeyabwaga mengine kadhaa machachari likiwemo kundi la Kontejazz kutoka jiji Arusha pamoja na MYUT kutoka mjini Morogoro.Kufuatia ushindi huo kundi hilo la Underzone limejinyakulia kitita cha shilingi milioni moja,ikiwemo na pia kuonyesha umahiri wao kucheza kwenye jukwaa la kilele cha msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti 2011,litakalofanyika baadaye hapa jijini Dar.Pichani kundi la Underzone likiwa limekabdhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja.
  Haikuaminika wala kufahamika kirahisi kwanini jaji huyu alikuwa akilia mara baada ya fainali kuisha,Ooh baadae ikabainika kuwa alikuwa akitoa machozi ya uchungu kabla ya kutangazwa kwa mshindi ambaye tayari walikwisha mbaini kwamba ni kundi fulani,Pichani Majaji wa shindano hilo la kulia ni Hamis mandi a.k.a B Dozen kutoka Clouds Fm 88.4 pamoja na jaji mwingine ambaye ni muandaaji wa kipindi cha ‘Step Up Player’ Isakwisa Thomson wakijaribu kumpigisha kimya jaji mwenzao kutoka T.H.T aitwaye Msami.
  Mmoja wa Watangazaji mahiri wa redio ya Clouds FM 88.4 Adamu Mchomvu ambaye pia ni mkali wa kufloo kwa namna yake kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya,akiwasha moto ndani ya Maisha Club ikiwa ni sehemu ya burudani katika mchakato mzima wa kuisindikiza fainali ya kulisaka kundi bora la mismu wa dhahabu unaoendelea wa Serengeti dansi la Fiesta 2011. 

  Kundi la Face 2 Face likiwa jukwaani likonesha umahiri wake wa kutaka kuibuka mshindi kwenye shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea wa serengeti dansi la fiesta 2011,linalofanyika katika ukumbi wa New Maisha Club jijini dar,ambapo watu kibao walijitokeza kulishuhutia shindano hilo ambalo lilikuwa limejawa na msisimko mkubwa.
   Mashabiki wakiendelea kufuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea jioni ya leo wakati wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea wa serengeti  2011.


  Kundi la Under Zone wakionyesha umahiri wao wa kucheza mbele ya mashabiki wakati wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea wa Serengeti 2011 jioni ya leo kwenye ukumbi wa New Maisha Club,jijini Dar.
  Majaji wa Serengeti Dance la Fiesta kutoka kulia ni  mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar es Salaam Hamis Mandi a.k.a B Dozen,Msami kutoka Tanzania House of Talent pamoja wa muandaaji wa kipindi cha ‘Step Up Player’ cha Clouds Tv, Isakwisha Thomson wakiwa ndani ya Maisha Club jijini Dar es Salaam.
  Kundi la Ice Cream kutoka jijini Tanga likisubiri majibu mara baada ya kuonyesha umahiri wao wa kucheza,jioni ya leo kwenye ukumbi wa New Maisha Club,jijini Dar wakati wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti 2011.
   Baadhi mashabiki wakijadiliana jambo huku wengine wakifuatilia kwa makini mchakato wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea wa Serengeti dansi la Fiesta 2011,linalofanyika ndani ya ukumbi wa New Maisha Club,jijini Dar.
  Palikuwa hapatoshi leo ndani ya ukumbi wa New Maisha Club,wakati wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti dansi la fiesta 2011.Pichani ni kundi la MYUT kutoka Morogoro.
   Mashabiki wakifutilia kwa makini mchakato wa kulisaka kundi bora la msimu wa dahahbu unaoendelea wa Serengeti dansi la Fiesta 2011 ndani ukumbi wa New Maisha Club,jijini Dar.
   Vijana kutoka jijini Dar,kundi la Still Unity wakionyesha manjonjo yao mbele ya mashabiki kibao waliojitikeza leo jioni kwenye shindano ya kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea wa Serengeti 2011,linalofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa New Maisha club.
   Kundi la Bsix kutoka Zanzibar wakionyesha umahiri wao wa kucheza kwa namna ya kipekee kuhakikisha karata yao ya ushiriki ndani ya shindano la dansi la fiesta haipotei bure.
   Mashabiki waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo katika kushuhudia shindano la washiriki wa shindano la msimu wa dhahabu unaoendelea wa Serengeti dansi la Fiesta 2011,kwenye ukumbi wa New Maisha Club,jijini Dar.
   Kundi la MHT kutoka jijini Mwanza likiwa ndani ya ukumbi wa New Maisha Club katika mchakato mzima wa kushiriki shidano la kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti dansi la fiesta 2011.
  Mmoja wa majaji kutoka Clouds FM 88.4 Hamis Mandi a.k.a B Dozen akifuatilia kwa makini mpambano wa washiriki wa dansi la Fiesta 2011 unaofanyika ndani ya ukumbi wa New maisha club,jijini Dar.

  Mmoja wa majaji kutoka Clouds TV,Kwisa Thomson akifafanua Mmoja wa majaji kutoka Clouds TV,Kwisa Thomson akifafanua jambo wakati wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta 2011 ndani ya ukumbi wa Maisha Club,jijini Darjambo wakati wa kulisaka kundi bora la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta 2011 ndani ya ukumbi wa Maisha Club,jijini Dar.
  Leo ndio ilikuwa fainali ya kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta 2011,baada ya makundi yaliyofanikiwa kuibuka washindi katika Mikoa yao,ikiwemo Dar,Tanga,Zanzibar,Morogoro,Arusha pamoja na Mwanza,Makundi hayo yamepambana leo katika ukumbi wa maraha New Maisha Club,jijini Dar.Pichani ni kundi la UB40 likionesha umahiri wake wa kucheza mbele ya mashabiki kibao waliofika kushuhudia shindano hilo lililokuwa na msisimko mkubwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: kundi la Underzone ndio kinara wa Serengeti dansi la fiesta 2011 usiku huu. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top