728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, February 21, 2011

  majina ya wanaowania tunzo za Kilimajaro Tanzania Music Awards 2011 watangazwa leo.

  Mratibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2011,kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Angelo Luhalla,akitaka kuyafungua majina ya wasanii waliochaguliwa kushiriki/kuwania tuzo hizo kwa mwaka 2011 mbele ya Waandishi wa Habari,leo jijini Dar.

  Mratibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2011,kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Angeloh Luhallah akikabidhiwa bahasha ya majina ya wasanii wa muziki walioingia kwenye mchakato wa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya mahesabu ya Innovex Auditions,Lloyd Zhungu.
  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ndiyo wadhamini,George Kavishe akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar,kuhusiana na mchakato mzima wa kuyataja majina ya wanamuziki bora watakaochaguliwa kuwania tunzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards,kwa mwaka 2011,kulia ni Mratibu wa tunzo hizo kutoka BASATA,Bwa. Agello Luhalla.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  2 comments:

  1. Mzee Luhala na timu yako. Nawapongeza sana kwa uteuzi mzuri. Ninasema mzuri na siyo mzuri sana. Uteuzi huu umeacha sehemu nyingine mfano hakuna majina ya wapigaji bora wa vyombo, pia hakuna uteuzi wa muziki wa asili "ngoma" uliofanyika, kwaya ziko wapi?.

   Kwa uelewa wangu (yawezekana nimepitwa na wakati)Sidhani kana akina Mpoto wanafanya muziki wa asili ya kitanzania. Akina mpoto wanafanya contemporary music of Tanzania, kama ilivyo kwa akina twanga, na bongo flava pia. Ninasema contemporary kwa sababu wanachanganya uzungu na utanzania, iwe midundo, lunga, vyombo n.k. Hivyo basi tunaposema asili ya Mtanzania inabidi tuwe makini kidogo. Tunawapeleka wapi wanamuzi ambao wanafanya style za akina Marehemu Dr. Hukwe Zawose na akina Nyunyusa?

   Uteuzi huu unanisikitisha kuwa unaendelea kutambua zaidi muziki genres za nje ukiacha za nyumbani. Au kwa sababu hawa wa vijijini hawawezi kurecord na kuingia kwenye soko la biashara? Jamani biashara itatufikisha mahali pabaya kama mataifa mengine ambayo yamepoteza asili zao na wanatafuta kuzirudisha hawawezi.

   Asanteni sana,

   Kedmon Mapana

   ReplyDelete
  2. Ninapopitia tena uteuzi huu, ninapatashida sana ninaposoma kuwa kuna tuzo ya "wimbo bora wa Kiswahili (Bendi)". Sasa hapa kuna maswali yanasumbua akili yangu: Neno bendi limewekewa mabano ili kutoa ufafanuzi wa neno Kiswahili? Je kuna wimbo bora wa Kiswahili? kiswahili hapa kimetumika kama lugha au aina ya muziki? Je hizo nyimbo zingine zinatumia lugha gani? Kwa nini wasingesema wimbo bora wa bendi?

   Ikumbukwe kuwa muziki wa bendi ni muziki mkongwe nchini, hapo zamani wengine waliita muziki wa dansi, jazz band, au orchestra band. Lakini uteuzi huu wa kili awards unatoa nafasi finyu sana ya muziki huu. Unatokea pale tu panaponipa utata wa jina "wimbo bora wa Kiswahili (bendi)". Kwa nini aina moja ya muziki bongo flava na R&B zitawale?

   Hitimisho langu ni kwamba: 1)Uchambuzi wa majiana na aina za muziki uwe wa makini kidogo na unaoshirikisha wadau mbali mbali wa muziki ili kupunguza changamoto zinazoweza kutokea. Hii itasaidia hata wale watakaopata zawadi hii wakaweza kuelezea mahali popote wakaeleweka. Sidhani kama mtu akiuliza eti umepata tuzo gani? Nawe ukakurupuka 'wimbo bora wa Kiswahili'. Hapa dhana inayokwenda moja kwa moja kichwani ni lugha ya kiswahili si aina ya muziki wa dansi au bendi.2) Awards za Kili zipo kibiashara zaidi na si kuboresha muziki wa Tanzania, tusipokuwa makini muziki wetu utadumazwa badala ya kukuzwa

   ReplyDelete

  Item Reviewed: majina ya wanaowania tunzo za Kilimajaro Tanzania Music Awards 2011 watangazwa leo. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top