kwaheri 2010 na karibu 2011.

Friday, December 31, 2010
Wadau wa JIACHIE BLOG popote pale mlipo inawatakia kila la kheri katika kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011.

Ni vema tukayukumbuka mazuri yote yaliyofanyika mwaka ACHWA na kuyaacha mabaya yake yakibaki kama kumbukumbu.

Basi na tuukaribishe mwaka mpya KARIBISHWA kwa amani,utulivu na upendo popote pale tutakapokuwa.

Wadau wa JIACHIE BLOG ninaamini kwa namna moja ama nyingine kama mwendeshaji wa blog hii,niliwakosea ama kuwakwanza kwa vyovyote vile,basi nayakubali mapungufu hayo kama binadamu mwingine yeyote ambaye si Malaika,tusameheane na na kuyafuta kabisa, tuanze mapya ya kutujenga sisi wanajamii na nchi yetu kwa ujumla.

JIACHIE BLOG pia inatoa shukurani maalumu kwa wadhamini wake wakubwa ambao kwa hakika wamewezesha mengi kufanyika na kuhakikisha blog hii haishii njiani wala kuyumba yumba kama baadhi ya blog nyingine ambazo kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo hasa katika uendeshaji wake,zimeishia njiani kama si kufa kabisa.

Wadhamini hao ni Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) pamoja na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel. Ama kwa hakika nawashukuru sana sana,lakini pia bado msaada wenu wa hali na mali unahitajika zaidi katika kuhakikisha JIACHIE BLOG inasimama imara bila kuyumba kwa aina yoyote ile,ili izidi kuihabarisha jamii katika mambo mbalimbali.Sukurani pia za kipekee na maalumu zimuendee mtaalamu wangu Christopher Makwaia wa MK GROUP.

Mbali ya wadhamini hao wakubwa,pia nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru wadhamini wangu wengine wadogo wadogo kama vile Mini Argos,MagariBeipoa.com,Flora Promotions pamojana Zizzou Stores.

Nawatakia heri na fanaka ya Mwaka Mpya.
Ahmad Issa Michuzi (michuzi Jr).
Mwendeshaji wa JIACHIE BLOG
.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

kumbe arusha nako mtungo kama kawaa..!

Mie nilijua Mtungo ni kwa Dar tu ,kumbe hata huku Arusha kitu mtungo ni kama kawa,tena unaambiwa hii mbona ndogo,kwa sababu watu wengu wamerudi makwao na wengine wako likizo,shughuli ngoja wenye mji warudi, na wafanyakazi wamalize likizo,Arusha panakuwa hapatoshi kabisa kwa mtungo.Picha hii nimeinasama mapema leo mchana (jina la barabara hii limenitoka kidogo,wakazi wa Arusha sio mbaya mkinipa taafu),nikiwa kwenye matembezi yangu ya hapa na pale ndani ya jiji la Arusha.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Salamu kutoka kwa Mdau wa JIACHIE BLOG.

KHERI YA MWAKA MPYA WADAU WOTE WA JIACHIE BLOGSPOT NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA


New is the year, new are the hopes and the aspirations,

new is the resolution, new are the spirits and forever my warm wishes are for u.

Have a promising and fulfilling new year.


KHERI YA MWAKA MPYA WADAU WOTE

WA JIACHIE BLOGSPOT NA WATANZANIA

WOTE KWA UJUMLA

CEO - Tutoke Media & Advertising
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

RAIS, DK SHEIN atoa salamu za mwaka mpya kwa wananchi wa zanzibar leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitoa salamu za mwaka mpya wa 2011 kwa wananchi wa Zanzibar,kwa kuwatakia kheri ya mwaka mpya, kuwa na Amani na Utulivu,bila ya kuwa na migogoro ya aina yoyote,aliyasema hayo leo Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

jenga afya yako kwa msimu wa matunda mkoani tanga

Ni msimu wa Matunda Mkoani Tanga.Pichani ni baadhi ya matunda ya aina mbalimbali yakiuzwa mapema leo maeneo ya Korogwe-Mkoani Tanga.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

kizazaa cha wafanyabiasha wa mboga mboga mjini arusha leo

Wafanyabiashara wa mboga mboga na matunda wakitimka mara baada ya kuvamiwa ghafla na askari wa jiji leo asubuhi kwenye soko kuu la Kilombelo jijini Arusha.Wafanyabiashara hao wamekuwa wakitimuliwa sehemu ya eneo hilo kwa madai kuwa wanafanya biashara sehemu isiyoruhusiwa. Kwa mtazamo wangu wafanyabiashara hawa ambao wanaonekana ni wengi sana wanapaswa kutafutiwa eneo maalum la kufanyia shughuli zao ili kuepukana na adha ya kusumbuliwa kila siku na askari wa jiji.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 1

nani mkombozi wa kilio cha samaki..!

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 2

tuwalinde watoto wetu dhidi unyanyasaji wa aina yoyote ile.

Picha hii niliinasa nikiwa katika matembezi yangu ya hapa na pale mjini Tunduma,nikiwa mjini humo nilishuhudia watoto wengi chini ya umri wa miaka 18 wakifanyishwa/tumikishwa kazi nzito ikiwemo na kubebeshwa mizigo mikubwa na mizito,jambo ambalo ni ukatili na unyanyasaji kwa watoto wetu kuwafanyia vitendo kama hivyo,kama uonavyo pichani ni mtoto akiwa amebebeshwa mabox yenye bidhaa ndani akizipeleka anakokujua yeye.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mpakani mwa tanzania na zambia.



Bango hili liko mpakani mwa Tanzania (Tunduma-Mbeya) na Zambia (Nakonde) kama lionekanavyo pichani .
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 3

boniface wambura aangwa na jambo leo

Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Boniface Wambura (wa pili kushoto),ambaye ameteuliwa kuwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), akikabidhiwa zawadi ya kompyuta ndogo iliyotolewa na uongozi wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), wakati wa hafla ya kumuaga Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa JCTL, Juma Pinto, Meneja Mkuu, Ramadhani Kibanike, Mkurugenzi, Benny Kisaka na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Perfect Solutions, Evance Aveva ambaye ni Mshauri wa JCTL.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

EVANGELIST EMANUEL MAYUNGA


DEAR FRIENDS AND ALL PEOPLE OF GOD.THIS IS A GOOD NEWS FOR YOU AND IT IS A BAD NEWS FOR SATAN.

I HAVE OFFICIALLY STARTED THE WORK OF EVANGELISM BY THE GRACE AND THE CALL FROM GOD AFTER YEARS OF TRAINING.

I'M PRIVILEDGE TO ANNOUNCE TO YOU THE NEWLY ESTABLISHED MINISTRY CALLED UPENDO WA YESU OUTREACH BASED IN NORFOLK V.A USA.I'M THE FOUNDER AND THE GENERAL OVERSEER.YOU CAN KNOW MORE ABOUT ME AND THE MINISTRY BY VISITING MY BLOG.
http://upendowa-yesu.blogspot.com, YOU CAN ALSO EMAIL ME AT EMAPATRICK10@HOTMAIL.COM

THERE WILL BE A GOSPEL CONFERENCE IN WASHINGTON DC ON SATURDAY 22JAN2011.THE VENUE AND TIME WILL BE ANNOUNCED LATER.I INCOURAGE YOU TO COME TO MEET THE LORD AT THE POINT OF YOUR NEEDS BECAUSE YOU WILL NEVER REMAIN THE SAME.

THE YEAR 2011 SHALL BE THE YEAR OF YOUR GREATER GLORY IN JESUS CHRIST NAME. MAY GOD BLESS YOU AND HAPPY NEW YEAR TOYOU ALL.

FOR WITH GOD,NOTHING IS IMPOSIBLE(LUKE 1:37)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, December 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Bobby farrell wa Boney M afariki dunia.!

Thursday, December 30, 2010
Bobby Farrell wa Boney M wakati wa uhai wake

Bobby Farrell wa Boney M afariki dunia mjini St.Petersburg ,Urusi


Bobby Farrell (61) alikuwa mwanamziki mashuhuri katika miaka ya 1970s kutoka kundi maarufu enzi hizo Boney M,Mr.Bobby Farrell amekutwa amefariki dunia katika chumba cha hotel aliyofikia mjini St.Petersburg,nchini Urusi.

Mwanamziki huyo alikuwa katika ziara ya kimziki nchini urusi,maiti yake iligunduliwa katika chumba cha hotel aliyofikia baada ya kumaliza show zake.idara ya usalama ya mji wa St.Petersburg umeunda kamati maalumu kuchunguza chanzo
cha kifo cha Bobby farrell.

Marehem Bobby Farrell (61) alikuwa mwanamziki anayeongoza safu ya mbele ya iliyokuwa bendi maarufu duniani Boney M,ambapo alifanyakazi na wanamziki Maisie Williams,Liz Mitchel na Marcia Barret.

Kundi la Boney M lilijizolea umaarufu kila kona duniani kutokana na umahili wa nyimbo zake kutingisha katika madisco na redio za kimataifa,Kundi hilo lilikuwa na maskani yake nchini Ujerumani na kuweza kupiga tour katika kila kona duniani.

Baada ya kundi la Boney M kusambaratika marehem Bobby Farrell alihamishia makazi mjini Amsterdam,nchini uholanzi.

Bobby Farrell mwanamziki mtanashati aliyetamba na kundi la Boney M hatunae tena!!!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

RAIS, DK ALI MOHAMED SHEIN AKUTANA NA BALOzI WA uturuki

Rais wa Zanzibar wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania,Dr.Sander Gurbuz,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania,Dr.Sander Gurbuz,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo.Picha kwa hisani ya Ramadhani Othman,Ikulu Zanzibar.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mwanamuziki nguli nchini,lady jay dee azindua mradi wake wa maji na mgahawa jijini dar


Lady Jay Dee akionesha maji ya kunywa ambayo yana jina lake yanayotolewa na Mohamed Enterprises Limited, akiwa ni msanii wa kwanza kupata endorsement ya aina hiyo nchini. Hafla hii imefanyika leo katika hoteli ya Paradise City jijini Dar. Akiongea na waandishi katika hafla hiyo Jay Dee pia aliweka wazi mipango yake kwa mwaka 2011 ikiwa ni pamoja na kufungua mgahawa uitwao 'Nyumbani Lounge' karibu na Best Bite Restaurant maeneo ya Ada Estate pamoja na kutoa albamu yake ya tano.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 30, 2010 | | Permalink | Maoni 1

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

EXCLUSIVE INTERVIEW WITH SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. ANNE SEMBAMBA MAKINDA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Sembamba Makinda akishuka kwenye gari lake kuelekea ofisi za Bunge mjini Dodoma.


SPIKA mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Semamba Makinda, (61) ambaye alichaguliwa hivi karibuni amefanikiwa kufanya mahojiano maalum na mtandao wa MO BLOG ya Jijini Dar es Salaam, na katika mahoajiano hayo aligusia vipengele vifuatavyo:

-Asema hataki kuondoka kwa shangwe za aibu

-Asisitiza muda wa miaka 40 Bungeni inatosha

-Aahidi kuhimili mikikimikiki ya wabunge vijana

Kupata mahojiano haya kwa kina bonyeza hapa:

http://www.mohammeddewji.com/blog/?cat=5
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Tangazo la Ibada ya Kiswahili itakayofanyika J'2 hii ya Jan 2nd 2011

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, December 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Wednesday, December 29, 2010
JESHI LA POLISI LAWATUNUKU ASKARI WAKE VYETI VYA KUTUKUKA LEO JIJINI DAR.

Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema pichani kulia akimpongeza meneja mauzo wa hsc Fatma Washoto (kushoto) jijini Dar leo,pichani kati akishuhudia ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Shamsi Vuai Nahodha.

====== ======= ======== ======== ========


Benjamin Sawe na Mwanakombo Jumaa

Maelezo

Dar es Salaam


Jeshi la Polisi limewatunuku askari wake vyeti vya kutukuka na zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu kwa utendaji uliotukuka na raia walioshiriki kufanikisha utendaji wa kazi za polisi.

Akikabidhi zawadi hizo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha amesema katika utekelezaji wa program ya maboresho, jeshi la polisi limebuni utaratibu wa kuwatunuku maafisa na askari waliotekeleza majukumu kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.

Waziri Nahodha alisema utaratibu huo unaongeza motisha,ari na moyo wa kujituma kwa wale wanaotunukiwa na kupewa zawadi. “Nitawaunga mkono katika kutekeleza mambo yote yenye lengo la kuimarisha utendaji wa kazi zenu”Alisema Waziri Vuai.

Askari tisa na raia mmoja walikabidhiwa zawadi hati ya cheti cha ubunifu pamoja na pesa taslimu shilingi laki tano kila mmjoa kuhusu utendaji kazi wa kipolisi.Wengine waliokabidhiwa hati ya utendaji wenye uadilifu na uminifu ni askari nane na raia wawili ambapo askari hao walikataa rushwa ya shilingi milioni 17.

Kundi la tatu lililotunukiwa vyeti na pesa taslimu shilingi laki tano ni la maofisa wa polisi kumi ambao walifanikisha kutoa elimu ya polisi bara na visiwani. Wengine waliotunukiwa hati ya chetii ni askari elfu thelathini na nne waliokuwa katika madawati ya uchaguzi mkuu uliopita kumalizika kwa amani na utulivu.

Aidha askari 118 wa kanda maalumu ya Ilala walikabidhiwa vyeti vya sifa ambapo kikosi hicho kimekuwa kikipambana na majambazi na kati yao saba walitunukiwa vyeti vya sifa na zawadi. Wakati huohuo Waziri Vuai alizindua doria ya Jeshi la Polisi kwa kutumia baiskeli 30 ambao watakuwa wakizunguka katika kata mbalimbali ili kuimarisha usalama.

Akitoa maelezo kuhusu kikosi hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Said Mwema alisema lengo la kuanzisha kikosi hicho ambacho kitashirikiana na raia ni kuongeza nguvu ya ulinzi kwa raia ambapo hatua hiyo ni moja kati ya maboresho ambayo yamefanywa na jeshi la polisi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

HON.MOHAMMED DEWJI DOCUMENTARY TEASER...!!!

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

joseph mbilinyi awashukuru wakazi wa mbeya.

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (MR II) akiwahutubia wananchi waliofika kwa wingi katika mkutano wake wa kuwashukuru jioni hii katika viwanja vya SIDO jijini Mbeya.Picha kwa hisani ya Rashid Mkwinda.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

ni nani huyu?!

Amekuwa gumzo kwa namna moja ama nyingine hapa jijini na hata kwenye baadhi ya vyombo vya habari,hasa magazeti.Unaweza kumbaini ni nani huyu?!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 16


Sammy Cool awakumbuka madansa.

*aja na
Black Moses Dancing Competition*!

NA MWANDISHI WETU

DANSA wa zamani Sammy Cool, ameanzisha mashindano ya kucheza muziki yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao, jijini Dar es Salaam. Akizungumza jijini Dar leo, Sammy Cool amesema kuwa mashindano hayo anatarajia kuyapa jina la Black Moses Dancing Competition, lakini baada ya kupata ridhaa ya ndugu za marehemu wa mcheza dansi huyo wa zamani. Sammy Cool alisema kuwa lengo la mashindano hayo, mbali na kuendeleza vipaji vya madansa, pia ni kumuenzi Black Moses aliyekuwa dansa maarufu nchini kutokana na umahiri wake katika fani yake hiyo.

Alisema kuwa anatarajia kuwashirikisha wadau mbalimbali katika mpango huo, lengo likiwa ni kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa ufanisi zaidi kama alivyokusudia. “Kwa sasa kuna vipaji vingi vya madansa hapa nchini, lakini hakuna mpango wowote wa kuwasaidia…hivyo nimeona ni vyema nikaanzisha mashindano haya ili kila mwenye kipaji cha kucheza muziki,” alisema.

Alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa yakifanyika zaidi ya mara moja kwa mwaka katika maeneo tofauti nchini, japo yataanzia jijini Dar es Salaam na baadaye kuhamia mikoani. Aliwataka madansa wote wenye vipaji, zaidi wakiwa ni chipukizi kukaa mkao wa kula kwani shindano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake na lenye mvuto wa kipekee. Sammy Cool ni miongoni mwa madansa waliotamba nchini kutokana na uhodari wake wa kucheza muziki, akiwa ametwaa tuzo kadhaa nchini.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 3

CHINA YAAHIDI KUSAIDIA SEKTA YA SANAA NCHINI.

Na Mwandishi Wetu.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeingia kweye makubaliano na ubalozi wa China nchini ya kubadilishana kazi za sanaa na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha mashirikiano ya kiutamaduni na kukuza sekta hiyo nchini.

Akiwa katika ziara yake BASATA ambayo aliambatana na maofisa wawili wa ubalozi wake Huang Wei na Wang Hong,Balozi muambata wa utamaduni kutoka China,Liu Dong amesema kwamba nchi yake imejipanga kusaidia sekta ya utamaduni nchini kwa kuwashirikisha watanzania kwenye matamasha mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya sekta hiyo.

Bw.Liu alikubaliana kimsingi na BASATA katika kuimarisha mahusiano ya kiutamaduni ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuwezesha ubadilishanaji wa kazi za sanaa na wasanii ili wapate fursa za kuuza kazi zao, kujitangaza na kushiriki katika matamasha mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

“China kwa sasa inaweka nguvu kwenye suala la kubadilishana utamaduni baina ya mataifa haya mawili.Tunategemea kuwashirikisha wasanii wa Tanzania katika matamasha mbalimbali tutakayoyaandaa pamoja na kuwapeleka nchini China kwa ajili ya kuongeza na kubadilishana ujuzi” alisisitiza Liu huku akitaja sanaa za uchongaji, filamu, uchoraji, ngoma za asili, sarakasi na nyinginezo kuwa watazipa msisitizo.

Kwa kuanzia Balozi huyo wa China alisema kwamba,wasanii wa Tanzania watapata nafasi ya kushiriki matamasha na maonesho ya kuazimisha mwaka wa China ambayo yanatazamiwa kuanza mwishoni mwa Februari mwaka 2011 ambapo pamoja na wasanii kutoka Tanzania watakuwepo pia magwiji wa tasnia hiyo kutoka China pamoja na waandishi wa habari maarufu.

Kwa upande wake,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, ziara hiyo ya maofisa wa ubalozi wa China ambayo imekuja baada ya ile ya awali ya maofisa wa Baraza ubalozini kwao ni yenye manufaa makubwa na italeta tija kubwa katika tasnia ya sanaa na utamaduni kwa ujumla hasa ukizingatia wasanii wamekuwa na uhitaji mkubwa wa maonyesho na masoko ya kazi zao.

Alingeza kwamba,BASATA iko tayari kusaidiana na China katika masuala mbalimbali ya ukuzaji wa sekta ya sanaa huku akiweka wazi kwamba,uhusiano wa China na Tanzania ni wa muda mrefu sana hivyo kuna kila sababu ya kuuendeleza na kuuimarisha zaidi.

“Kama kuna suala lolote mtakalohitaji tuwasaidie katika kukuza ushirikiano wa kiutamaduni sisi tuko tayari na milango iko wazi.Bila shaka eneo hili la mashirikiano ya kiutamaduni ni nyeti sana na hatuna budi kulipa msukumo wa kipekee” alisisitiza Materego.

Picha/Habari na Alistide Kwizela,BASATA

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

andrew chenge ahukumiwa miaka 3 au kulipa faini ya sh.700,000/=

Mbunge wa Bariadi na aliyewahi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali Mh Andrew Chenge leo amehukumiwa kifungo cha miaka 3 au kulipa faini ya shilingi 700,000/= na mahakama ya Wilaya ya Kinondoni baada ya kukutwa na hatia ya kusababisha vifo kwa ajali. Hata hivyo Mh Andrew Chenge amelipa faini hiyo ya shilingi laki 700,000/= na kuachiwa huru. Hukumu hiyo imetolewa na hakimu wa mahakama hiyo Bw.Lusema na Mh. Andrew Chenge alikuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Simon Mponda.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 9

Msimu wa raha kamili na serengeti kuitikisa Dar na arusha mwaka mpya.!

Lile tamasha la Msimu wa Raha kamili na Serengeti 2010 baada ya kufanyika katika mikoa kadhaa ikiwemo Iringa,Mbeya,Tunduma,safari hii linatinga ndani ya jiji la Dar katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni,wakati huo huo mjini Arusha katika viwanja vya Matongee nako kutakuwa na msimu wa raha kamili.Kwa habari zaidi endelea kuperuzi hapa hapa jamvini.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 1

Taarabu jijini New-york - 'Chozi lanitoka' (Remix)



Wimbo wa 'Chozi Lanitoka' ulioimbwa na Alsarah dada toka Sudan aishiye Brooklyn jijini New - York Marekani. Alsarah alihamia Marekani akiwa na umri wa miaka 12 toka kwao Sudan na ni mpenzi mkubwa wa miondoko ya Taarabu, pia ni mpenzi mkubwa wa lugha ya Kiswahili.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, December 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mh nyarandu alivyopokelewa kwenye jimbo lake leo

Tuesday, December 28, 2010
Na wapiga kura walimshukuru kwa kumpatia zawadi kemkem.
Akivishwa joho na viatu vya kimira baada ya kupokea silaha za jadi kwa ajili ya mapambano.
Akisalimiana na wapiga kura wake.
Akicheza ngoma za kinyaturu za kikwao.

Baada ya kutembelea miradi ya umeme wa upepo Mh Nyalandu alikwenda katika jimbo lake kuwashukuru wapiga kura wake na kupongezwa kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri. Mengi yalifanyika.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 2

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

STANDARD CHARTERED NA BOT TUNAOMBA

MTUFAFANULIE HILI.!


Dear Bloggers,

Mimi ni Mtanzania ninaishi hapa mjini Dar es Salam. Wiki iliyopita Jumatano niliamua kwenda kununua Inverter lakunistiri ili nipungukiwe na adha ya Tanesco. Nilimpigia simu rafiki yangu Mmoja kwa jina la Mercellina nikamwuliza amenunua wapi Inverter akanielekeza TROPICAL POWER ambayo ipo mtaa wa Narug’ombe. Akanishauri nisiende na gari langu mwenyewe ila nitumie usafiri wa Teksi kwa sababu parking ni za shida hapo mahala. Nilitumia ushauri wake nikapaki gari langu mjini na kuchukua teksi hadi mtaa wa Narung’ombe nikakuta hiyo Tropical Power ipo Jengo Moja na Benki ya Stanbic mkabala na Benki ya Standard Chartered.

Niliamua kufanya shughuli zangu za Kibenki hapo nikiwa kama mteja wa benki zote mbili na haswa mteja wa branch ya Kariakoo ya Standard Chartered. Nilipoingia ndani nilimsimulia dada mmoja kuwa nimekuja kuomba kadi ya Visa ambayo nitaweza kutumia nikiwa nje ya nchi kwa maana nasafiri sana na kila nikisafiri nakuwa siwezi kutumia hela zangu kwenye hiyo account labda nikiwahi ndio nizihamishie kwenye account yangu ya Stanbic. Akaniuliza una account ya dola na sisi? Nikamweleza kuwa sina Account ya dola hapo Stanchart ila ninayo benki ya Stanbic. Akaniambia ni mpaka niwe na account ya Dola ndio nitaweza kutumia kadi ya Visa nikiwa nje.

Nikamwelezea kuwa ni Ghali kumudu account mbili za dola na pia nikampa mfano kuwa je mtanzania wa kawaida akipata bahati akapewa safari ya kwenda nje atafanyaje? Mnatulazimisha tufungue account za dola mbona nchi za wenzetu kufungua account za hela za kigeni ni shida? Nikamweleza kuwa mimi pia nina account ya Shilingi na Benki ya CRDB na Stanbic ila sijawahi kupata tatizo nazo nikisafiri sasa kama mtanzania ni Kosa kuwa na account ya Shilingi hapo STANCHART? Huyu dada akanishauri niende kuonana na Branch Manager na mimi nakakubali.

Nilivyofika kwa Branch Manager nilimkuta yupo na Dada Mwingine nadhani anafanya kazi hapo hapo Benki, nikamsimulia shida yangu huyo Dada akaniambia zamani walikuwa wanatoa TEMPORARY VISA CARD kwa ajili ya wateja wenye account za Shilingi wakiwa wanasafiri yenye limit ya Dola Elfu Kumi kwa siku Thelathini ila sasa hivi hawazitoi tena na ikitaka Visa inayoweza kufanya kazi nje ya Nchi lazima nifungue account ya fedha za kigeni. Nikawaeleza mbona Benki Nyingine kadi zao zinafanya kazi na hizo hizo za Shilingi? Kwa nini mimi leo Mtanzania nalazimishwa kuwa na account ya Dola ilikuweza kutumia account yangu nikiwa nje?

Mbona mtu kutoka South Africa, Marekani au Uingereza hawaambiwi wafungue account za Shilingi huko nchini kwao? Nilitoa sababu zote za Kimsingi ila meneja na Mwenzie walishindwa kunisaidia wakaniambia hilo swali haliwezekani aliniomba account Yangu nikampa kadi akatazama kwenye mtandao wao na kuona mimi ni mteja mdogo sana ndio hata nguvu ya kunisaidia niliona imeshuka wakasema hawawezi kabisa kunisaidia kwa Kuwa ni Policy kutoka BANK OF TANZANIA wao wanafuata. Nikawaeleza hiyo policy ni ya kuwaumiza watanzania wa chini kwa kuwa Madirectors wote wa BOT na Maofisa wakubwa wa kubwa huko au la wafanyakazi wote wanamiliki account za fedha za kigeni na pia wanamaacount ya Shilingi yenye Visa cards kwenye mabenki Mengine.

My dear Bloggers, to cut this story short, what I am trying to raise here is that One day you here this bank saying one story and another bank saying another story. Whenever you try to reason with them they say it is a directive from BOT. If I can remember when the new Governor started in one of his conversations or press releases he said they will do their best to make sure we use more Shillings than dollarizing the economy. They went on to say people should stop quoting rents and all in foreign currency and trade in Shillings. How can we trade in shillings when we cannot access our Shillings account because of their directives?

My humble request is for the directorate of Banking Supervision at the BANK OF TANZANIA to clearly help clarify this with the banks. A few months ago I visited an EXIM BANK BRANCH at Namanga and they refused to accept USD $ Dollar bills that were printed before 2003 and the reason they gave is that they had received a circular from their top Management and also a directive from BANK OF TANZANIA. Can you please help us with clarifications in regards to handling of foreign currency.

STANDARD CHARTERED naomba mliangalie hili swala kwa mtazamo mpya mkishirikiana na BOT kama kweli mna nia ya kumsadia Mtanzania unless mtu asiyeweza kumudu account ya Dollar kwenye benki yenu sio TARGET CLIENT WENU. Au kosa kuwa mtanzania na kumiliki account ya Shilingi?

Asanteni
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 6

Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) laingia ubia na kampuni ya Power Pool East Africa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Power Pool East Africa, Machwa Kagoswe akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu juu ya eneo la kuzalishia umeme wa upepo mkoani Singida . Serikali imeingia Ubia kupitia Shiriaka la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni binafsi ya Power Pool East Aftrica ili kuzalisha umeme huo kuanzia mwakani.

======= ====== ======= ====== ====== ======

Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) limeingia ubia na kampuni ya Power Pool East Africa wa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida utakaogharimu takribani ya Sh Bilioni 180.

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu alisema tayari makubaliano yamesainiwa na serikali NDC kwa niaba ya serikali itakuwa ikimiliki asilimia 51 za hisa na nyingine zitakuwa za mwekezaji binafsi.

Nyalandu alisema kwa mradi huo ambao utakuwa wa gharama nafuu katika uzalishaji utaingizwa katika gridi ya taifa na kwa kuanzia zitazalishwa megawati 50 na baadae zitaongezwa kulingana na uwezo wa wabia hao.

“Tokea kuanza kufungwa kwa mitambo itachukua takribani miezi 15 ili umeme uingie katika gridi na hii itakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme kwa sasa” alisema Nyalandu.

Mkurugenzi wa Viwanda vikubwa wa NDC Alley Mwakibolwa alieleza kuwa kwa ujenzi wa mitambo hiyo ya kutumia upepo kutasaidia kuzalisha umeme ampema kwani mitambo ya aina hiyo huchukua muda mfupi kuwekwa ikilinganishwa na ya maji ama ya gesi.

Tutajitahidi mradi huu uende kwa kasi kubwa kwani kwa kuanzia tutazalisha megawati 50 na baadae tutaongeza 50 ili kuoingia katika gridi ya taifa" alisema.

Aidha katikaeneo hilo ambalo liko ukingoni kwa bonde la ufa, upepo ni mkakli kiasi cha kufanya miti karibu yote kulalia upande mmoja na upeo huende kwa kasi ya hadi mita 21 kwa sekunde

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 1


JUKWAA LA SANAA BASATA LAJA NA SURA MPYA 2011

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Ghonche Materego amesema kwamba, kuanzia mapema Januari mwaka 2011 Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu Basata litakuwa na muonekano mpya huku likitoa fursa kwa wasanii kulitumia kama Jukwaa la kutangaza na kuonesha kazi zao.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa la kufunga mwaka wa 2010 Jumatatu hii,Materego alisema kwamba,kwa sasa Jukwaa pamoja na kubeba mada na mafunzo mbalimbali kama ilivyokuwa awali litakuwa wazi kwa wasanii wote wanaotaka kuzindua kazi zao, kuzionyesha kwa wadau, kuziwasilisha (listening event) kabla ya kuzipeleka sokoni na vilevile kuzitambulisha kwa wadau wapana.

“Leo Jukwaa letu la Sanaa linamaliza mwaka,2011 tunadhamiria kuhakikisha sanaa inaweza kuongeza pato binafsi la msanii, kuongeza ajira na kupunguza umaskini wa kipato miongoni mwa wasanii na taifa kwa ujumla.Kwa kuanzia lazima tuanze kwa kuwapa nafasi wasanii kuonesha kazi zao na baadaye kupata mrejesho kutoka kwa wadau” alisema Materego.

Alizidi kufafanua kwamba,wasanii wamekuwa wakipeleka kazi zao sokoni bila kupata wasanii wa kuzijaribu na kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali hali ambayo imekuwa kwa kiwango kikubwa ikisababishwa kazi zao zishindwe kufanya vizuri sokoni kutokana na kutoshirikisha wadau mbalimbali.

“Ili kupata nafasi ya kuboresha kazi za wasanii na wao kupata maoni mbalimbali kutoka kwa wadau, Jukwaa la Sanaa litatoa fursa kwa wasanii kufanya maonyesho katika vipindi mbalimbali na baadaye kuulizwa mawasili, kupokea maoni na michango mbalimbali” alisisitiza Materego.

Akizungumzia mafanikio ya Jukwaa la Sanaa katika kipindi cha mwaka unaomalizika,Materego alisema kwamba, jumla ya mada mbalimbali 43 zimewasilishwa na wawasilishaji 47 ambapo wadau wa tasnia ya sanaa zaidi ya 2,600 wameelimishwa juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto mbalimbali zilizoibuliwa kutatuliwa na mamlaka mbalimbali za serikali.Idadi hiyo ya wadau 2,600 iliyohudhuria katika kipindi cha mwaka huu ni zaidi ya malengo kwani lengo lilikuwa ni wadau 1,000.

Alizitaja baadhi ya changamoto ambazo ziliibuka kwenye Jukwaa la Sanaa na kutatuliwa na mamlaka husika kuwa ni pamoja na maadili mabovu ya wasanii katika vipindi vinvyorushwa kwenye runinga,elimu ya sanaa kufundihswa toka ngazi za shule za awali, uboreshaji wa matamasha ya sanaa,uboreshaji wa masoko ya ndani na ya nje kwa kazi za wasanii, urasimishaji wa sekta ya sanaa, matumizi ya lugha miongoni mwa wasanii na kufuatilia pia kudhibiti uvaaji usiofaa wa wasanii hasa wanenguaji kwenye majukwaa.

“Masuala kama elimu ya sanaa kutolewa kuanzia ngazi ya shule za awali,uboreshaji wa sanaa zetu, usimamizi thabiti wa matamasha ya sanaa, uboreshaji wa masoko ya ndani na ya nje yako kwenye mpango mkakati wa BASATA wa mwaka 2011-2014.Pia ninaamini sheria ya hakimiliki na hakishiriki iliyo chini ya Cosota katika bunge hili itajadiliwa na kupitishwa rasmi” alimalizia Materego huku akitoa pongezi kwa wadau wa sanaa wote waliohudhuria katika kipindi cha mwaka unaomalizika.

Awali kabla ya Materego kuongea,Mwalimu Komba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Idara ya Sanaa alitoa elimu juu ya Matumizi ya ala katika sanaa ya muziki ambapo alitoa wito kwa wasanii kuingia darasani na kujifunza matumizi ya ala za muziki hasa zile za asili badala ya wao kuwa waimbaji pasi na kutumia ala.

Jukwaa la Sanaa litaendelea tena wiki ijayo (Jumatatu ya Januari 3, 2011) ambapo Mratibu wa onyesho maarufu la kila mwaka la Sauti za Busara,Kwame Mchauru atawasilisha mada itakayohusu ‘Mchango wa Matamasha ya Sanaa Katika Kuongeza Ajira na Pato nchini Tanzania’.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

TANGA BEACH RESORT ndio mahala pekee pa kujiachia kwa raha zako


"TANGA BEACH RESORT"
Kijiwe safi kwa wasafiri kati ya Dar es salaam na Arusha/Mombasa.
Mahali pa kupumzika na pia tuna vyumba vya kulala vya kifahari na kumbi za mikutano za kisasa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 1

warembo sita kutoka arusha na karatu wafuzu mchujo wa kumsaka kisura wa tanzania.


NA MWANDISHI WETU

WAREMBO sita wa Mkao wa Arusha na mmoja kutoka Karatu, wamefanikiwa kufuzu katika mchujo wa kumsaka Kisura wa Tanzania 2010/11 uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii, ikiwa ni awamu ya pili ya mchakato huo ambao fainali zake zinatarajia kufanyika Machi mwakani.

Mwenyekiti na Mwazilishi wa Kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), waandaaji wa shindano hilo, Juliana Urio, aliwataja wasichana hao kutoka Arusha kuwa ni Dotinata Soro, Glory Ephrahim, Naomi Meckon, Neema Kirango, Neema Selle na Susan Manoko. Na kutoka Karatu ni Kipoyane Laiboni.

Alisema kwamba katika mchujo huo uliofanyika Via Via Club kwa siku moja,Jumanne, na baadaye kuelekea Karatu ambako mchakato huo ulikuwa ukifanyika mitaani (boma kwa boma), wasichana wengi walijitokeza kujaribu bahati yao, lakini ni hao tu waliokidhi vigezo vinavyotakiwa katika mashindano hayo.

“Tumefarijika mwitikio wa wasichana wa Arusha ulikuwa ni mzuri sana kwani tulipata wasichana zaidi ya 50 ambao wengi wao walikua katika ubora wa hali ya juu. Tunaamini mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake,” alisema Urio.Urio alivitaja vigezo vinavyotakiwa katika shindano hilo kuwa ni urefu wa sentimita 174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.

Alisema kuwa baada ya kufanya mchujo huo Arusha na Karatu, Jumanne na Jumatano, timu ya Kisura itaelekea mkoani Dodoma, kabla ya kuhamia Iringa, Mbeya na Ruvuma, Januari 3 hadi 7, ikiwa ni awamu ya tatu na ya mwisho.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa ni Family Health International (FHI), na wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

kumbukumbu ya mzee ibrahim hamis chimgege


MAREHEMU MZEE IBRAHIM HAMIS CHIMGEGE


MAREHEMU MZEE IBRAHIM HAMIS CHIMGEGE MMOJA YA WATANGAZAJI WA MWANZO KABISA WA ILIYOKUWA RADIO TANZANIA DSM (RTD) SASA HIVI TBC (TANZANIA BROADCASTING CORPORATION)

SIKU, WIKI,MIEZI NA SASA MIAKA MINNE TANGU UTUTOKE HAPA DUNIANI GHAFLA TAREHE 28/12/2006, UMETUACHIA MAJONZI MAKUBWA SANA KILA TUKUKUMBUKAPO.

UPENDO MKUU ULIOTUPA UNGALI UKIISHI HAPA DUNIANI HATUTAUSAHAU KAMWE, LAKINI BADO TUNAAMINI MAOMBI YAKO KWA MUNGU BABA, YANAENDELEA KUTUBARIKI.


KATIKA UHAI WAKO ULIWAGUSA WATU WENGI SANA KWA WEMA NA UKARIMU WAKO, BADO WANAKUONGELEA NA KUKUKUMBUKA SANA.

UKWELI UMETUACHIA PENGO KUBWA AMBALO HALINA MTU WA KULIZIBA KAMWE.


UNAKUMBUKWA SANA NA WATOTO WAKO HAMIS, AMIRI, OMARI, MOHAMED NA SALWA NA WAJUKUU ZAKO WOTE, NDUGU, JAMAA, NA MARAFIKI WOTE.

` RAHA YA MILELE UMPE EEEH MOLA . . . . . . .`

-AMIN

Familia ya CHIMGEGE
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, December 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

rais kikwete amuampisha jaji mkuu mpya ikulu leo.

Monday, December 27, 2010
Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu, Othman Chande, wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu, baada ya zoezi la kuapisha mapema leo mchana kwenye viwanja vya Ikujulu,jijini Dar.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mohamed Othman Chande, kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake, Agustino Ramadhani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 27, 2010 | | Permalink | Maoni 0

DK Shein azungumza na Wizara ya Nchi OFISI YA RAIS

Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na utawala Bora,Ikulu Mini Zanzibar,akiwa katika utaratibu wake wa kuzungumza na kila wizara.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 27, 2010 | | Permalink | Maoni 0

zawadi ya boxng day

Pichani ni msaniii wa muziki wa kizazi kipya kwa jina la kisanii aitwaye Quick Racka,akichagua kikapu kwa matumizi yake ya nyumbani,kama aonekanavyo pichani kwenye moja ya kijiji maeneo ya Morogoro jana jioni ambapo ilikuwa ni siku ya boxng day.Bei ya vikapu hivyo huuzwa shilingi 1,000 mpaka 6,000 kwa kila kikapu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 27, 2010 | | Permalink | Maoni 0

chagua na kujifunza hapa


www.saveimetalart.blogspot.com

Karibu katika blog yetu,hapa utachagua,jifunza na kuwasiliana na ofisi yetu
kwa ajili ya order ya kazi mbalimbali kama zilivyoonyeshwa.
Karibu sana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 27, 2010 | | Permalink | Maoni 0

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 27, 2010 | | Permalink | Maoni 0


Hasheem Thabeet: We’ve got a Problem!

Ushauri wa bure!!!


The Memphis Grizzlies refers him as Hasheem “Thabust” just to indicate their sentiments due to poor contribution he brings on the table for his organization. The atmosphere is not compelling at all; it won’t be a surprise to learn of another assignment that would send Hasheem Thabeet to NBA’s Development League.


Hasheem, who once was a hero in the college league when played at Uconn, is definitely doing nothing impressive to his team. The rage is on among intolerant fans that could not spare their sentimental feeling towards him, considering that they blew out a second overall pick to select Mr. “Thabust”.


Hasheem is among Tanzanians who could make us proud and yes he still can, but there is some sort of extra efforts need to be taken. NBA sio lelemama, big stars (Shaq, Olajuwon, Michael Jordan, Kobe etc) didn’t get there easily. There is a lot to give up, and yes a lot to work upon. Trips to Tanzania on every bit of NBA break will not help the process. You need to maximize the off season segment for an advancement of your career.


Hasheem Thabeet was drafted in summer 2009 as a second overall pick by the Memphis Grizzlies, to set a remarkable and landmark event to the country he was born in (Tanzania) and East Africa as a whole. I want to believe that every “bongoman” celebrated to the fullest…ooh it was a proud moment of our time. I remember inviting West African friends “Wapopo” at my house for nyama choma and drinks, as the banner waved in front of my house reading “CELEBRATING HASHEEM THABEET ACHIEVEMENT”.


The Memphis wants a trade! They want to…not as their wishes to throw away their own second pick No! But only to get rid of Mr. “Thabust” who has been not only less productive, but also a burden. Hasheem has established himself to be a liability on both offensive and defensive end on the court. The only thing he’s good at is fouling.

The problem they are facing is to find imminent deals to match up a “second pick” value.


Reports say that no team is willing to take Hasheem, unless packaged with other pieces for which Memphis is still contemplating the proposal. "The team is super disappointed in his lack of desire to get better. He is beyond bad, Yes he does nothing well. He doesn’t even block shots and he is not feared in the paint anymore" says one of the fans.


Hasheem has lost touch with the game. His performance is awful. He rarely score points (avg 1.4 per game), grabs rebounds (1.40 per game), and 0.0 assists. His playing time dropped drastically and fans expect anything when he enters the game.


Now, we all know that Hasheem came into the game with limited basketball skills, but that does not restrict him from excelling his potential. There are more qualities a player needs to have instead of just being tall and Hasheem just doesn't have those abilities right now. I will give him one small excuse; he didn't start playing basketball until he was 15.


Hakeem Olajuwon bears an identical background Hasheem has. He started playing at the age of 15, but Hakeem “The Dream” knew what was due to shape up his game. He did his assignments and achieved a major accomplishment in the league, two times NBA titles.


This article has nothing to do with malicious motive, but a wakeup call to reboot Hasheem’s intensity to press toward the original purpose and live up to the expectations. We (wabongo) are still living a hope we have in you. One day your game will turn around, if only some seriousness is attached to the process. I wish you all the best in your endeavor. Happy New Year kijana!

Mwanaspoti.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 27, 2010 | | Permalink | Maoni 25

NAOMBENI USHAURI KABLA SIJACHUKUA SHERIA MKONONI KWA MZUNGU HUYU..!

Wanajamvini,

Kwa masikitioko makubwa, nashindwa kuelewa kwamba NCHI yetu au dunia yetu inaelekewa wapi. Mdogo wangu ambaye yuko form 4 mwenye umri wa miaka 17 anayeishi nyumbani kwangu, siku ya ijumaa alinishingaza sana. Kwa muda mrefu amekuwa akizungumza na wenzie nyumbani kuhusu wazungu.

Basi siku ya ijumaa, binti huyo aliniambia kwamba anaenda kwa rafiki yake huko Bunju, nami nikampa nauli na kumwelekeza kwamba lazima arudi kabla ya saa mbili jioni. Kwa bahati mbaya au nzuri, mimi na mke wangu tukawa tuna safari yetu jioni kuelekea Sea-Cliff. Baada ya kufika huko, nikamkuka binti huyo amekaa na mzungu mezani wanakula.

Mzungu wa miaka 50+ nilisogea mezani kwao na hasira sana, ila kwa bahati mbaya mke wangu alinizuia kabla ya kumfikia huyu mzungu, ambaye alinyanyuka na kukimbia. Baada ya kufika nyumbani jioni, nilimuweka mtoto huyu kiti moto na baadae akakiri kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na huyu mzee kwa miezi minne sasa.

Babu huyu mzungu amekuwa akimpa vitu vingi vya thamani kama Nokia N70 ambayo alikuwa anatumia kwa kuficha pamoja na hela. Hapo hapo hapo akakiri kwamba amekuwa akiangalia blog moja inayohusudu wazungu na kuona kwamba maisha mazuri yanapatikana unapoolewa na mzungu. Huyu binti aliendelea kunielezea chini ya kibano kwamba wasichana wote warembo wameolewa na wazungu.

Siyo hiyo tu, marafiki zake wengine kama watatu pia wanatembea na wazungu, mbaya zaidi mmoja wao ana miaka 16 na anayewapeleka kwa wazungu ni dada mmoja ambaye yupo kwenye mambo ya U-miss. Wanajamvini, huu utumwa wa kimawazo ambao unaambukizwa kwa watoto wetu tunawezaje kuukemea? Nawezaje kuifungulia serikali na huyu mwenye blog anayewarubuni watoto wetu mashitaka? Vinginevyo itabidi nichukue sheria mikononi mwangu dhidi ya huyu mzungu wa Afrika Kusini.

Naombeni maoni yenu,
Mdau..Kawe Beach. DAR
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, December 27, 2010 | | Permalink | Maoni 25

jengo la mahakama ya kisutu lawaka moto jijini dar

Sunday, December 26, 2010
Askari wa Usalama Barabarani akisaidia kuzima moto uliokuwa ukiteketeza sehemu ya jengo hilo huku mlinzi wa mahakama hiyo akiangalia.
Mlinzi wa jirani na jengo la Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akizima moto uliokuwa ukiteketeza sehemu ya jengo hilo huku mlinzi wa mahakama hiyo akiangalia wakati trafiki akifanya mawasiliano kwa ajili ya msaada zaidi.Picha na Robert Okanda.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, December 26, 2010 | | Permalink | Maoni 4

CLOUDS MEDIA GROUP wafanikisha vyema tamasha la kumshukuru mungu.

Mwimbaji mahiri wa wa nyimbo za injili, Flora Mbasha akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa Kinondoni na vitongoji vyake kwenye uwanja wa Biafra jioni ya leo kwenye tamasha la pamoja la kuwashukuru wapenzi na wasikilizaji wote wa Clouds FM kwa mwaka wa 2010 na pia kufikisha miaka 11 katika burudani,na kuwakutanisha pamoja wasikilizaji wa redio Clouds FM 88.4.
Aboud kutoka Clouds Tv (kushoto) na Harris Kapiga Mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 kipindi cha Gospel Track ambaye ndiye alikuwa ni mratibu wa tamasha hilo la injili wakibadirishana mawazo na kiongozi wa kwaya ya Kinondoni Revival.Lengo kubwa la kuandaa tamasha hilo ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kufikisha miaka 11 katika burudani na pia kuwakutanisha pamoja wasikilizaji wa redio Clouds FM 88.4.

Katikati ni mkurugenzi wa Msama Promotions, Bw. Allex Msama akibadirisha mawazo na baadhi ya watu waliweza kufika katika tamasha la injili lililofanyika katika viwanja vya biafra.Lengo kubwa la kuandaa tamasha hilo ni kumshukuru Mungu kwa kuweza kufikisha miaka 11 katika burudani na pia kuwakutanisha pamoja wasikilizaji wa redio Clouds FM 88.4 . Mwimbaji wa injili, Miriam Rukindo Mauki akihojiwa na Clouds Tv, mwimbaji huyu nae alifanya vyema kwenye tamasha hili katika viwanja vya Bbiafra jioni ya loe jijini Dar.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege akizikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa injili jioni ya leo mbele ya umati wa watu ambao walivutiwa sana na uchezaji na uimbaji wa mwimbaji huyo.
.Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Jackson Benty kutoka mjini Arusha akiwapa neno watu waliohudhuria katika tamasha hilo.
.Kwaya ya Kinondoni Revival nao waliweza kuonyesha umahiri wao wa kucheza na kuimba kwa shangwe na vigeregere.
Kwaya ya Kinondoni Revival nao waliweza kuonyesha umahiri wao wa kucheza na kuimba kwa shangwe na vigeregere.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Jesca Honore akiimba katika tamasha la nyimbo za injili lililoandaliwa na Clouds Media Group katika viwanja vya Biafra injili jioni ya leo.
Mshereheshaji wa tamasha hilo, Hudson Kamoga akishusha vutu vyake.

Wakazi wa Kinondoni na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi jioni ya leo kwenye viwanja vya Biafra kwenye tamasha la injili kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kufikisha miaka 11 katika burudani na pia kuwakutanisha pamoja wasikilizaji wa redio Clouds FM 88.4.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, December 26, 2010 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu