
Msanii wa hipo hop anaekuja kwa kasi katila anga ya muziki wa Bongofleva anaetamba na nyimbo zake kadhaa ukiwemo wa Mr President,Roma akikamua jukwaani usiku wa kuamkia leo katika tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 ndani ya Musoma Hotel,Roma ni msanii ambaye kwa kiasi kikubwa amewakuna vilivyo wakazi wa Musoma kutokana na mashairi yake yenye ujumbe wa kutosha.

Umati wa watu ulivyofurika ndani ya Musoma Hotel usiku wa kuamkia leo.

Wasanii wa kundi la TMK Wanaume Halisi likiongozwa na Juma Nature wakilishambulia jukwaa kwa kasi.

Wasanii Chege na Mh Temba wote kutoka kundi la Wanaume TMK wakikamua jukwaani,huku washabiki wao wakiweka mikono juu kuashiria kukunwa vyema na nyimbo zao.

Farid Kubanda a.k.aNgosha akishusha mistari ya nguvu mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,ambapo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya Bia ya Serengeti.

Anajiita Mwamba wa Kaskazini,Joe Makini jukwaani.

Msanii Hussein Machozi akiwambia wakazi wa Musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010.

Mkali wa Moro Bell 9 akiwaimbia wakazi wa Musoma wimbo wake wa Masogange uliowavutia washabiki wake,usiku wa kuamkia leo ndani ya Musoma Hotel.

Wakazi wa Musoma walikuwa live ile mbaya,full kujipangusa kila wakati huku mfalme wa raha kamili akipewa nafasi yaka kama kawaida.

Msanii chipukizi mahiri katika muziki wa anga ya bongfleva ,Diamond akiimba wimbo wake wa Mbagala kwa wakazi wa Musoma usiku wa kuamkia leo ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010.

Diamond akiwa amebebwa juu na mashabiki wake huku akiwaimbia mpango mzima wa Mbagala

Mkali mwingine wa hip hop bongo ,Godzilla kutoka Sala sala a.k.a Broklyn akiangusha mitindo huru kwa wakazi wa Musoma usiku wa kuamkia leo ndani ya musoma hotel,ambapo maelfu ya watu walijitokeza kujipangusa.

Wakazi wa Musoma wafunikana kwa kujipangusa,bila kucheza mbali na mfalme wa raha kamili

Msanii mahiri ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye ziara hii ya tamasha la Fiesta Jipanguse,Mwasiti akiwarusha mashabiki wake na wimbo anaotamba nao kwa sasa uitwao kisa pombe.

Full rrrhhhhaaaa kila mahali

Msanii Mataluma kutoka THT akionesha umahiri wake wa kucheza na kuimba jukwaani.

Washabiki wakiserebuka taratiibu.

Wakali wa Bata kutoka Zenj,Offside Trick wakiwarusha bata wao jukwaani kwa pamoja nao bila hiyana aah ni kujiachia tu kwa kwenda mbele huku mfalme wa raha kamili akiwa tayari amekita mahali pake.

Kutoka nyumba ya vipaji THT,Barnaba na Lina wakiimba wimbo wao wa Kisa meseji ambao umeonekana kukubalika vyema kabisa kwa washabiki wao.

Lina akimpagawisha shabiki wake jukwaani

Wakazi wa Musoma walivyojitokeza kwa wingi ndani ya Musoma hotel usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta jipanguse 2010,tamasha hilo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti.

Wasanii wenye vipaji vya kuimba kutoka THT,Amin na Barnaba wakiimba wimbo wao wa Robo saa.

Mfalme wa raha kamili tayari amedumisha raha zaid kwa washabiki hawa,ambpo mmoja wao alijifanya Chui Chui.

Msanii aliyewahi kufanya vyema katika shindano la Bongo Star Search,kutoka Mwanza,Beatrice akikamua hip hop lwa staili ya kipekee kabisa iliowavutia washabiki waliofurika ndani ya Musoma Hotel usiku wa kuamkia leo.

Kijana mdogo lakini mambo yake ni makubwa,anajiita Young D a.k.a Young Millionea akikamua jukwaani.

Ama kwa hakika wakazi wa Musoma bado wanazidi kuivunja historia yao ya kujitokeza kwa wingi kwenye matamasha ya Fiesta kila mwaka yanapofanyika,safari hii wamejitokeza kwa wingi na kuonekana live kushangweka kila wakati,huku wakiburudika na mfalme wa raha kamili,tamasha la fiesta Jipanguse mdhamini wake mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake mbalimbali ikiwemo Tusker,Uhuru bia,Villta Malt,Malta Guinnes na vinywaji vingine vikali.