wasikilize wazee wa bata hawa.!

Wednesday, June 30, 2010
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mikoroshini street-Msasani

Maeneo ya mtaa wa Mikoroshini-Msasani unavyoonekana leo jioni
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

wako mjini wanapeana mawazo

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

serikali yaongeza muda wa usajili wa namba za simu

Pichani ni baadhi ya wakazi wa Msasani wakisajili namba zao simu leo mchana kama walivyokutwa na Jiachie


SERIKALI imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani ili kuwezesha wananchi wengi waweze kujisajili baada ` kusikiliza kilio chao ili kuwapa fursa zaidi ya kujisajili.
Hayo yalisemwa jana Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msollla wakati akiwasilisha hotuba yake ya makadrio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo. “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu imesikia kilio cha wananchi wengi.


Imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani hadi Julai 15, mwaka huu baada ya hapo simu zote ambazo hazijasajiliwa zitafungwa,” alisema Profesa Msolla .
Aidha Waziri Msolla alisema jumla ya kampuni 14 hadi sasa zimepewa leseni ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu. Aliongeza kuwa idadi ya watumiaji wa simu kwa kigezo cha njia za simu (line) zinazotumika imefikia 18,207,390, hivyo idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 400 ikilinganishwa na watumiaji 3,542,563 waliokuwepo mwaka 2005.


Alisema idadi ya simu za mezani hadi sasa ni 174,800 ilinganishwa na 154,420 zilizokuwepo mwaka 2005. “Hii ni sawa na ongezeko la la asilimia 13.2 . ukuaji huu umepanua wigo wa mawasiliano ya simu na kuongeza huduma nyingine zinazoendana na matumizi ya simu hapa nchini Alizitaja huduma hizo kuwa ni upatikanaji wa taarifa, huduma za mtandao, ulipaji wa Ankara za simu, maji, umeme na huduma za kibenki. Awali Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa nambazote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1, mwaka 2009 hadi Desemba 31, mwaka 2009.


Awali mamlaka hiyo iliongeza muda wa mara ya pili wa miezi sita wa kusajili simu hizo, kuanzia Januari mwaka 2010 hadi Juni mwaka huu baada ule wa kwanza kuonyesha watu wengi walikuwa hawajajisajili.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Bodi ya Biashara ya Nje imepiga marufuku maonyesho yote ya sanaa za Kitanzania ikiwemo ngoma, muziki na maigizo

Habari wa ndugu wapendwa.

Chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni Tanzania (CAJAtz) kimeshtushwa na kusikitishwa na uamuzi wa Bodi ya Biashara ya Nje (BET) wa kupiga marufuku maonyesho ya Muziki na Ngoma za Utamaduni katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kupitia waraka wake uliotolewa na UTAWALA, BET imepiga marufuku maonyesho yote ya sanaa za Kitanzania ikiwemo ngoma, muziki na maigizo eti kwa madai kwamba yanaleta kelele.


Wakati huohuo muziki unasikika ni ule wa wasanii kutoka nje ya nchi kwenye maspika makubwa. CAJAtz inatambua thamani ya sanaa na Utamaduni wa Taifa hili na inaamini kwamba sehemu kama hizo ndiyo muafaka hasa katika kutangaza shughuli za sanaa na Utamaduni wetu.

Tunaamini pia kwamba katika maonyesho hayo ya biashara makampuni na asasi mbalimbali huwatumia wasanii katika kufikisha ujumbe wao kwa watu mbalimbali hasa kwa kuamini katika nguvu ya sanaa. lakini tunashangaa leo hii kuona BET inawataza wasanii kutumia fani zao kutoa ujumbe kwa watu licha ya kuwa makampuni na asasi hizo zimetumia pesa kuwakodi wasanii hao. CAJAtz inaamini kwamba sanaa ni biashara hivyo kwanza ilipaswa kuachwa ili ijitangaze kupitia maonyesho hayo. Pia BET inapaswa kufahamu kwamba kwa miaka yote ambayo wameilezeza kuwa na Mafanikio makubwa katika maonyesho hayo, sanaa na hizo ngoma zilikuwa zinatumika sana katika kusherehesha, kutoa ujumbe na kuelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali ya washiriki. Kwa kitendo cha kupiga marufuku maonyesho ya sanaa BET imekosa UZALENDO na utamaduni wetu na pia imebana ajira ya wasanii wengi walikuwa wameajiriwa na makampuni kwa ajili ya kufanya shughuli za maonyesho kwenye mabanda yao.

Kwa Msingi huo kama wadau wa masuala ya sanaa na Utamaduni hapa nchini, CAJAtz tunalaani vikali zuio hilo ambalo halina tija na limeegemea zaidi ulimbukeni na Kasumba ya watu wa kuthamini sanaa za nje na kuwatukuza wageni wachache kwa visingizio visivyo na maana. Iweje sanaa za Kitanzania iwe kelele na hizo za magharibi iwe burudani? Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kulishughulikia suala hili haraka iwezekanavyo. Pia tunomba BET kutafakari upya zuio hilo.

Hassan Bumbuli
Katibu Mkuu CAJAtz
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

soko la pamoja kuanza kesho

WAZIRI wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC),Dkt. Diodorus Kamala amewahakikishia watanzania kuondoa hofu ya kunyang'anywa ardhi yao kutokana na Tanzania kujiunga na Jumuiya hiyo.

Dkt.Kamala alisema kuwa ardhi ya Tanzania itabaki kuwa mali ya watanzania na haitaguswa na raia kutoka nje ya nchi kwa kisingizio soko la pamoja.

Hayo aliyasema Dar es Salaam juzi wakati akitoa ya utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuongeza kuwa Tanzania inatazamiwa kunufaika na soko la watu milioni 130 kwa kuuza bidhaa zitokanazo na kilimo katika jumuiya baada ya kuboresha mazingira ya uzalishaji.

Dkt. Kamala alisema kuwa Tanzania ndio nchi pekee inayotarajiwa kutoa chakula kwa nchi za EAC kutokana na kuwa na ardhi nzuri ya mazao hivyo hatuna budi kutumia nafasi hiyo kuimarisha uchumi na maendeleo kwa ujumla.

"Jumuiya ya Afrika Mashariki imejaliwa kuwa na vyanzo vya maji, nishati, ardhi na hata mbolea hivyo kupitia jitihada za kikanda;Sekretarieti ya EAC imejipanga kuibua mpango wa kupatikana kwa utaratibu wa kuvuna mbolea itakayosaidia utekelezaji wa mkakati wa maendeleo ya kilimo,"alisema. Habari zaidi Bofya Hapa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mchanyato wa mr & Miss East Afrika UK 2010




Utawala wa Urban Pulse unapenda kuwaletea exclussive behind the scenne kwa wadau wote wa libenekene kuhusu matayarisho na maandalizi ya Miss & Mr East Africa Uk 2010 yaliyofanyika katika kitongoji cha Edmonton, Ukerewe jumamosi 26.6.10

Fainali ya kuwania Taji la U Miss na U Mr East Africa UK litafanyika Jumamosi Julai 3, 2010 katika ukumbi wa Central Hall,Westminister, London

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 30, 2010 | | Permalink | Maoni 1

TUMERUDI HEWANI - BACK ONLINE

Tuesday, June 29, 2010

Siku ya leo Tanzania ilipambazuka vibaya. Mtandao
wako uupendao
ulikuwa na ujumbe kuwa UKO KWENYE MATENGENEZO. Hilo
halikuwa tangazo rasmi, bali ilikuwa ni ishara kuwa kuna matatizo ya
kiufundi, ambayo tunasikitika kusema yalikuwa nje ya uwezo wetu na
yamechukua muda mrefu kuliko tulivyotarajia. Hata hivyo, baada
ya
jitihada kali kufanyika za kurekebisha hali hiyo, hatimaye
tumerudi tena hewani na tunaendelea kukuhabarisha
yote yanayojiri Bongo.


Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu, tunawaomba radhi
kwa usumbufu mkubwa
mlioupata. Hatuna la kusema,
zaidi ya kuwaomba radhi na kuwapa kile
mlichokikosa
kwa muda huo!


Asanteni sana

WEB MASTER
GPL.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga alazwa hospitalini


Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mwenye nguvu.

Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kimwili.

Kwa hiyo taarifa iliyotolewa hii leo na msemaji wake imewashangaza wengi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo madaktari wameamuru Odinga alazwe hospitalini kwa muda wakisema tu kwamba ana uchovu. Cha kukanganya ni kwamba taarifa hiyo iliwanukuu madaktari hao pia wakisema Odinga ana uwezo wa kufanya kazi kama kawaida ikiwa atajisikia kufanya hivyo. Japo hawatamruhusu kufanya hivyo.

Hadi sasa, maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa Rais Mwai kibaki ambaye baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi.

Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya.

Zaidi Bofya Hapa

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mr II atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la mbeya mjini,aweka wazi kukamatwa kwake na polisi

Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II

TAARIFA KWA VYOMBO HABARI

.NATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MBEYA MJINI KUPITIA CHADEMA

· NATOA TAMKO RASMI KUHUSU KUHOJIWA KWANGU NA POLISI

Mimi, Joseph Mbilinyi ambaye najulikana zaidi katika anga ya muziki kama “Sugu” ama “Mr II” leo tarehe 29 Juni 2010 natangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa muda mrefu katika maisha yangu ya kimuziki pamoja na kuimba nyimbo za kuburudisha nimekuwa zaidi mstari wa mbele kuimba nyimbo za kutetea haki za makundi mbalimbali katika jamii na taifa kwa ujumla.

Wakati umefika sasa wa kuhamisha jukwaa la mapambano ya kudai haki kutoka jukwaa la muziki mpaka jukwaa la siasa kwa dhamira ile ile ya kutumia kipaji changu alichonijalia Mwenyezi Mungu kuimba na kuhutubia kwa ajili kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa letu.

Nyimbo zangu zimekuwa zikibeba sauti ya watu wasio na sauti ili zisikike na watawala; lakini hata hivyo kwa kipindi chote ambazo nimekuwa nikifanya harakati hizi watunga sheria na wafanya maamuzi ya kisera chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kuongoza vizuri taifa kuweza kufanya mabadiliko ya kweli yenye kuhakikisha watanzania wananufaika na vipaji vyao ambavyo Mwenyezi Mungu amewajalia na taifa linanufaika na rasilimali na maliasili ambazo tumejaliwa kuwa nazo.

Hivyo natangaza nia ya kugombea ubunge ili kuchangia katika kuongeza nguvu ya chama mbadala katika Bunge letu; niwe sehemu ya sauti mbadala katika kutunga sheria, kuwawakilisha wananchi, kuandaa sera na kuiwajibisha serikali kuweza kutekeleza yale ambayo mimi na wanaharakati wenzangu katika sanaa tumekuwa tukiyapigia kelele muda mrefu kupitia muziki wetu na maisha yetu.

Uamuzi wangu wa kugombea ubunge Mbeya Mjini ni haki yangu ya kikatiba na natambua kuwa kwa kuwa mbunge nitafanya kazi ya kuwawakilisha wananchi wenzangu na kama ambavyo wakati wote nimekuwa nikipambana katika harakati mbalimbali ndivyo ambayo nataka niwe mstari wa mbele kupambana katika kuleta maendeleo.

Huu si wakati wa kampeni hivyo niwaahidi wananchi wa Mbeya kwamba nitaeleza mengi kuhusu sera zangu na ahadi zangu kwao mara baada ya kupitishwa na CHADEMA kugombea ubunge katika jimbo letu.

Hivyo, nachukua fursa hii kuwajulisha watanzania wenzangu kwamba siku chache sijazo nitachukua fomu ya chama ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.

Lakini kwa ujumla uamuzi wangu wa kugombea umesukumwa na harakati zangu za miaka mingi na ufahamu wangu kuhusu hali halisi ya maisha yetu wananchi wa Mbeya Mjini.

Natangaza nia ya kugombea nikiwa ni mgombea mpya kutoka chama mbadala ili kushirikiana na wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini kuondokana na siasa za makundi, ukabila, ubaguzi, na migogoro ambazo zimekuwa zikitawala katika Jimbo letu na Mkoa kwa ujumla na hatimaye kusababisha tuwe na uongozi mbovu unaokwamisha maendeleo.

Jiji la Mbeya linakabiliwa na ubovu wa barabara ukiondoa barabara kuu inayokwenda Tunduma; barabara za mitaani ni mbovu wakati ambapo kuna fursa ya kuwa mkoa wenye makaa ya mawe ambayo mabaki yake yangeweza kutumika kukarabati barabara za mitaani Uyole, Soweto na kwingineko.

Natambua kwamba wafanyabiashara wa Mbeya Mjini wanamalalamiko mengi kuhusu kubambikiziwa kodi huku wafanyabiashara wadogowadogo wakiwa wananyanyaswa katika maeneo wanayofanyia biashara kwa kuwa hata mimi mwenyewe nimewahi kuwa mfanyabishara katika soko letu la Mwanjelwa.

Natambua kwamba jiji letu la Mbeya ni kitovu cha elimu katika mkoa wetu hata hivyo lugha zinazotolewa na uongozi wa Mkoa zinawadhalilisha walimu wakati uongozi huo unashindwa kuweka mazingira bora ya elimu na kusababisha Mbeya mjini kuanza kudorora kielimu. Kwa upande mwingine, kadiri mji unavyopunuka ndivyo kero ya usafiri wa wanafunzi inakithiri na shule za pembezoni zinakosa walimu.

Natambua kwamba kwa muda mrefu Mbeya Mjini yetu ina kero ya umeme wakati ambapo tupo jirani na Mgodi wa Kiwira ambao ungeweza kuzalisha umeme wa kututosheleza lakini kutokana na ufisadi tunashindwa kuondokana na hali hii ambayo inasababisha ugumu na kupanda kwa gharama za maisha na kukosa taa za barabarani hali ambayo inaweka mazingira ya kuongezeka kwa uhalifu.

Natambua kwamba viwanda vyetu vya Mbeya Mjini vimeuzwa kwa bei chee na vingine vimeshindwa kuendeshwa na kubaki magovu na kusababisha vijana kukosa ajira na uchumi kuathirika kama ilivyokuwa kwa viwanda vya pamba, mafuta na nyama.

Natangaza nia ya kugombea ubunge wa Mbeya Mjini kwa kuwa naamini kwamba kero ya maji inayotukabili inaweza kuondolewa tukiwa na uongozi mbadala ambao utaweza kutumia vyanzo mbadala vya maji kama mto Mzovwe, Ivumwe na kutoka katika Mlima Igamba.

Natangaza nia ya kugombea Ubunge ili pamoja na kuingia bungeni niweze kuingia katika halmashauri ya Jiji la Mbeya nishirikiane na wananchi wenzangu kuibua ufisadi na udhaifu iliopo unaosababisha ubadhirifu wa fedha za wananchi na mali za umma kama ilivyotokea kwa milioni 68 zilizobaishwa kwenye ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2007/08; tuhuma za kutaka kuuza kiwanja cha wazi eneo la Sokoine na kushindwa kulipa fidia wananchi wa Kata ya Kalobe waliondolewa katika viwanja vyao.

Wakati huo huo; napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini, wapenzi wa muziki wangu, wanachama wenzangu wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla kwa jana tarehe 28 Juni 2010 nilikamatwa na polisi kwa kile walichonieleza kuwa kuna malalamiko dhidi yangu kuwa nimemtishia kwa maneno kumuua Ruge Mutahaba kupitia wimbo uitwao “Wanna Kill” uliopo kwenye album iitwayo “Anti Virus”.

Walinikamata saa 5 asubuhi nikiwa naingia ukumbi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya kutoa Mada kuhusu “Tathmini ya Muziki wa Kizazi Kipya na Hatma yake nchini” na kunihoji kwa takrabani masaa matano mpaka saa 10 jioni.

Wameniachia kwa kile walichonieleza kuwa ‘dhamana ya kujidhamini mwenyewe’ na kunitaka niripoti kwao siku ya jumatano tarehe 30 Juni saa 5 asubuhi siku ambayo nilipanga kwenye ratiba zangu kurejea nyumbani Mbeya Mjini kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kabla ya tarehe ya mwisho ya utoaji na upokeaji fomu ndani ya CHADEMA.

Katika mahojiano nao yaliyofanyika Makao Makuu ya Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani; maofisa usalama (CID) walionihoji walirejea mstari mmoja katika kiitikio cha wimbo husika wenye maneno “I Wanna Kill Right Now” na kusema kwamba mlalamikaji ameutafsiri mstari huo kuwa ni tishio la kutaka kumuua.

Napenda kuwajulisha mashabiki wangu na watanzania wenzangu kwamba nimelieza wazi jeshi la polisi kwamba hakuna wimbo wala maneno niliyowahi kutamka kwa lengo la kukusudia kumuua binadamu yoyote. Niliwaeleza jeshi la polisi kwamba sanaa ya muziki inalugha zake zake za kifasihi.

Maadhui ya wimbo mzima yamejikita katika harakati zangu za siku zote za kupambana na wanyonyaji dhidi ya maslahi ya wasanii Tanzania na wimbo huo una maudhui ya kutaka “Kuondoa ama kuiua dhamira ya mbovu na nia zao ovu”.

Ni vyema mashabaki wangu, wanachama wenzangu na watanzania kwa ujumla wakarejea katika Kamusi mbalimbali za kimataifa ambapoo neno KILL linamaana zaidi ya 10 zikibeba pia maana ya KUKOMESHA, KUONDOA nk.

Katika wimbo huo nimeghani kwa kutumia fasihi mambo ya ukweli yanayotokea katika sekta ya sanaa na wala hauna dhamira yoyote wala maudhui ya kufanya kosa lolote la jinai; hivyo kama kuna mtu ameguswa na ukweli uliomo katika wimbo huo na hakubaliani nao basi aupinge kwa hoja ama akafungue madai badala ya kukimbilia kutaka kuliingiza jeshi la polisi kwenye masuala ya sanaa.

Aidha nimeshangazwa na hatua ya jalada hilo la polisi kufunguliwa ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Wizara ya Mambo ya Ndani yaliyopo Wilaya ya Ilala wakati mimi na mlalamikaji wote ni wakazi wa Wilaya ya Kinondoni.

Baada ya maelezo niliyoyatoa ni matumaini yangu kuwa jeshi la Polisi ambalo lina kazi muhimu zaidi ya kukabiliana na ujambazi na vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vinazidi kuongezeka katika Mkoa wa Dar es salaam ambapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yapo litaelekeza nguvu zake katika kukabiliana na vitendo hivyo vya makosa ya Jinai badala ya kupoteza muda wake kushughulikia masuala ya kifasihi ambayo yana sura ya madai yasiyo na uzito wowote.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 5

video mpya ya jaffarai ft T.I.D

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 1

vumi aitambulisha singo yake ya nne leo,yuko mbioni kuikamilisha albamu yake

Vumi akiwa amepozi na rafiki yake Godliva
Msanii Vumi akielezea ujio wake mpya katika anga ya muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva.Vumi anasema hivi sasa yuko kwenye harakati za kuikamilisha albamu yake itakayokuwa na jumla ya nyimbo nane,anazitaja baadhi ambazo tayari zinafanya vyema kwenye vituo mbalimbali vya redio kama vile Nenda,Utanikumbuka,tatizo umaskini pamoja na singali yake mpya aliyoitambulisha leo ndani ya kipindi cha Leo Tena iitwayo That Day.Vumi ambaye pia ni moja ya wasanii waliopikwa vyema na kituo cha THT kwa sasa yupo kwenye bendi ya Kimondo Sound a.k.a Kibajaji akijiendeleza zaidi.
Mtangazaji mwalikwa kwenye kipindi cha Leo Tena (kwenye chachandu la leo) aitwaye Husna B akitokea redio ya Coconut FM 88.2 a.k.a Mambo ya zenji,Zanzibar
Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Dina Marious kupitia redio ya Clouds FM 88.4 akifanya mahojiano mafupi na msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye vumi ambaye kwa sasa yupo ndani ya bendi ya muziki wa dansii ya Kimondo Sound a.k.a Wanakibajaji ikiongozwa na Richard Mangustino aliyewahi kuwika miaka ya nyuma kwenye bendi kadhaa ikiwemo ya Diamond Sound enzi zilee za Ikibonda Nkoi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 1

Bonanza Nyama Chabezi Tegeta Jumapili.

-Mashujaa Musica kuwasha Moto

-Watoto kucheza kiduku

-Vimwana wa Mashujaa kupamba jukwaa

Bendi ya Mashujaa Musica (Watoto wa Cash Lady) siku ya jumapili itashuka katika viwanja vya Nyama Chabezi Tegeta kutumbuiza wakati wa Bonanza litakaloshirikisha vikundi mbalimbali vya Viduku, na Michezo ya watoto ikiwa ni pamoja na Pool, kuvuta kamba michezo yote itaanza saa nane mchana ikiwa ni pamoja na michezo ya watoto ya kukimbiza Kuku na watoto kushindana kucheza makirikiti.

Burudani hiyo itaanza saa nane mchana ambapo Mashujaa Musica watatumbuiza chini ya wanamuziki wake wote akiwemo Rapa Mahili Ibrahim Milinda Nyeusi(Vuvuzela), Kiongozi wa Bendi Jado Fidifosi, Mtalaam wa Masauti Pasia Budance na Raja Rada.

Kwa mujibu wa msemaji wa Mashujaa musica, Shaaban Mpalule, Maandalizi yote kwa ajili ya onyesho hilo yamekamilika

“sisi tumeshajipanga kwa ajili ya burudani hiyo, hivyo kazi imebaki kwa wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi ili washuhudie kazi mpya ya bendi yangu ikiwa ni pamoja na kupata radha mpya ya nyimbo mpya”alisema Mpalule

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa bendi ya Mashujaa kutumbuiza katika eneo la ukunda wa Mbezi ambapo wamesema wataonyesha miondoko mbalimbali ikiwemo kuchinja bata, Wamefulia, kwa kiingilio cha shilingi elfu tatu wakubwa na watoto shilingi mia tano.

Wakazi wa Tegeta na maeneo yanayokaribiana mmetakiwa kufika siku hiyo ili kushuhudia burudani hizo, ambapo zawadi mbalimbali zimeandaliwa kwa mashabiki 50 wa kwanza watakaowahi kuingia kukaa katika sehemu zao.

Mashujaa Musica kwa sasa imekamilisha kurekodi nyimbo sita ambapo wanatazamia kufanya uzinduzi wa Album yao ya kwanza yenye nyimbo Mwanike, Moshi wa Sigara, Safari ya Vikwazo, Deodata, Mama Mi Nashangaa, sambamba na Intro ambazo zinaendelea kutesa katika sehemu mbalimbali za vyombo vya habari, Radio, Magazeti, na Tv.

Ratiba ya wiki Mashujaa Musica

Jumatano –Mashujaa Pub Vingunguti Kiingilio Kinywaji

Ijumaa - woodland kiwalani kwa jimmy kiingilio 3000

Jumamosi –Mashujaa Pub Vingunguti Kiingilio shilingi elfu 2000

Jumapili - Nyama Chabez Tegeta Kiingilio Shilingi 3000 wakubwa na watoto 500.


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Balozi wa Uganda na India wakutana na Rais karume

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania,Ibrahim Mukiibi,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kuonana na Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akisalimiana na Balozi wa Ugana nchini Tanzania,Ibrahim Mukiibi,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akisalimiana na Balozi Mdogo wa India anyeishi Zanzibar,Rajender Prakash alipokuja kuaga kwa kumaliza muda wake wa kazi Nchini.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Breeeking neeeewwwws:Ndege yapata ajali maeneo ya kabuku.!



Update: ya ajali ya ndege

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea mkoani Tanga na inadaiwa kuwa ilibeba watu 5,Rubani ndiye alipoteza uhai,kwa mujibu wa shuhuda mwingine aliyepo eneo la tukio anasema kwa hali ya ndege ilivyo hakuna mtu aliyepona,na kwamba ndege hiyo ni ya JWTZ kituo cha Ngerengere mkoani Morogoro,mpaka sasa hali ni tete eneo la la tukio kwani hakuna gari linalokwenda wala kurudi kutokana ndege hiyo kuziba barabara.
============


Habari zilizoifikia Blog yako ya JIACHIE hivi punde imehabarishwa kuwa Ndege ndogo ambayo idadi ya watu waliokuwemo bado haijajulikana, imepata ajali kwa kugongana na basi iliokuwa imebeba abiria (watalii) ambao nao idadi yao haijajulikana kwa haraharaka,maeneo ya Kabuku Mkoani Tanga.



Aidha chanzo chetu cha habari ambacho kipo kwenye eneo la tukio kimeeleza kuwa ndege hiyo iko nyang'anyang'a na haitamaniki tena, imeziba barabara na kwamba mpaka sasa ni mtu mmoja aliyebainika kupoteza maisha,aidha wananchi walioko sehemu ya tukio wanaaendelea na juhudi za kuwaokoa majeruhi ndani ya ndege hiyo halikadhalika na kwenye basi pia.

Chanzo cha habari kinazidi kusema kuwa mpaka ajali hiyo inatokea , wananchi wanajitokeza kuwasaidia majeruhi hakuna chombo chochote cha usalama kilichkuwa kimekwisha fika eneo la tukio."kwa sasa kuna msongamano mkubwa wa watu na mabasi mengi yamekwama hapa kwa saababu ndege imeziba barabara na magari hayawezi kupita"kimesema chanzo chetu cha habari.

Wanajamvini habari ndiyo hiyo lakini tutazidi kuhabarishana zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 29, 2010 | | Permalink | Maoni 3

burudika na fleva yetu ya kibongo bongo.

Monday, June 28, 2010
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 1

mr ii aachiwa huru kwa kujidhamini


Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva (Hip Hop),Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II ameachiwa huru kwa dhamana

Mr II alikamatwa mapema leo asubuhi
katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati wa kikao cha PRESS TALK akiwa anaongelea masuala ya muziki,

Akizungumza kwa njia ya simu Mr II amesema kuwa alikamatwa na polisi baada ya mmoja wa viongozi wa redio flani ya hapa jijini kumshitaki kuwa yeye (MR II) anamtishia maisha na pia kwenye wimbo wake wa AUNT VIRUS.

Mr II amesema baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo cha polisi cha upelelezi kwa ajili ya mahojiano,lakini baada ya muda Mr II aliachiwa huru kwa kujidhamini yeye mwenyewe.Aidha Msanii huyo ametakiwa kuripoti tena kesho kutwa katika ofisi hizo kwa mahojiano zaidi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 1

Flora Florence ndiye kinara wa miss estern zone 2010

Pichani ni tatu bora ya Miss Estern Zone 2010 wakiwa katika pozi,. Kushoto ni mshindi wa pili kutoka Lindi,Mary Adam na kati ni mshindi wa kwanza aliyenyakua taji la shindano hilo Flora Florence akitokea Morogoro na mshindi wa tatu ni Cecilia Paul kutoka Morogoro.

Washiriki wa shindano la Miss Estern Zone 2010 wakiwa kwenye shoo yao ya ufunguzi,shindano hilo limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Lindi,ambapo mshiriki kutoka Morogoro aitwaye Flora Florence alilinyakua taji la shindano hilo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

tangazo


we have a company that deals with translation from Swahili to English or English to Swahili in moving pictures (video) also create visions of a song into video, choose appropriate clothing for a certain location during video shoots and direct video.

For more information contact us via mail saharrah_media@hotmail.com or our number begin_of_the_skype_highlighting +255713308490 end_of_the_skype_highlighting
+255713308490

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

miss temeke 2010 wajifua vilivyo,kinara wao kujulikana july 9 tcc chang'ombe

Pichani ni Washiriki wa Miss Temeke ambao nao walipewa nafasi ya kujinadi mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye shindano la Redds Miss Ilala lililofanyika mwishoni mwa wiki pale Ubungo Plaza.Shindano la kumsaka mlimbwende atakayelinyakua taji la Miss Temeke 2010 linalotarajia kufanyika pale TCC Sigara Chang'ombe Julai 9/ 2010, ambapo burudani itatolewa na kijana mahiri katika muziki wa bongofleva Banana Zorro na bendi yake ya B. Band.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 1

washindi wa Zain Africa Challenge wakabidhiwa zawadi zao leo

Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi walioshiriki mashindano ya Zain Africa Challenge (ZAC) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vitita vyao leo asubuhi,makao makuu ya Zain,kutoka kulia ni Justine Rwerengera, Delphinus Kalumuna, Rodnique Sakaya na Justine Mwakalinga.

Wanafunzi wa Chuo Kuu cha Ardhi wakipokea kikombe cha ushiriki mashindano ya Zain Africa Challenge (ZAC) kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) akimkabidhi Mratibu wa Chuo Kikuu Huria Bw. Salim Hamad, dola 1600 kwa ajili ya kutambua ushiriki wao katika mashindano ya Zain Afrika Challenge Dar es saam, jana.Zain imekabidhi zawadi ya pesa taslim kwa Vyuo viliyoshiriki ZAC.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) akimkabidhi Mratibu wa Chuo Kikuu ARDHI Dr. Mbura Omari dola 1600 kwa ajili ya kutambua ushiriki wao katika mashindano ya Zain Afrika Challenge Dar es saam.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mr ii adakwa na wanaodaiwa wanausalama !




Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,imeripoti kuwa msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II amekamatwa leo mapema asubuhi na watu wanaodaiwa kuwa ni wanausalama wakati anakwenda kwenye kikao cha press talk kinachofanyika kila siku ya jumatatu katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),sababu ya kukamatwa kwake bado hazijajulikana na haijulikani wamekwenda nae wapi.
Globu ya Jamii inafuatilia kutaka kujua mustakabali mzima wa kukamatwa kwake na italeta taarifa kamili hapo baadae.hivyo tuvute subira.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 5

rais karume akabidhiwa shahada yake ya kupigia kura

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume, akipewa maelezo na Afisa msaidizi wa Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Magharibi,Maalim Khamis Mussa,(wapili kulia) mara baada ya kukabidhiwa shahada ya kuandikishwa kuwa mpiga kura, katika kituo cha Skuli ya msingi ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja jana, (kulia) ni Afisa mwandikishaji kura za maoni wilaya ya magharibi Unguja,Ali Radhid Suluhu.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

homa ya fiesta 2010 kutikisa moro july 7



Barnaba
Belle 9
Diamond
Juma Nature
Kala Pina -Kikosi cha Mizinga
Joe Makini


Chege.
Offside Trick
Fid Q
Hussein Machozi
Godzilla
Mh Themba
Wadau Msimu wa tamasha la Fiesta 2010 linakaribia kuanza,na kama ujuavyo tamasha hilo husheheni mambo kibao kwa wapenzi/washabiki wao.safari hii kwa mara ya kwanza tena linagonga hodi ndani ya mji kasoro bahari,Morogoro.Wakazi wa Morogoro Fiesta hiyo 2010 inawajia mkoani mwenu ikiwa na kauli mbiu yake JIPANGUSE Rrrrrrrhhhhhhaaaaa..! Huku Mdhamini mkuu wa tamasha hio ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd.
Orodha ya wasaniii utakao Jipanguse nao ndio kama hao hapo juu,si hao tu na kuna wegineo kadhaa wa kadhaa akiwemo Mwana Fa,Amini na Linah kutoka THT.Kutakuwepo na michezo mbalimbali,Fiesta Jipanguse rrrhhhhhaaaaa 2010 itafanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri,July 7 kwa kiingilio cha sh 2000 kwa kila mmoja.Kama vile haitoshi July 9 tamasaha hilo litahamia mjini Arusha na kufanyika ndani ya Matongee .

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

tangazo


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

kazaula atoa msaada kwa hospitali kuu mkoa wa kagera

Mdau mwanaharakati Peter Kazaula (kulia) akikabidhi mashine ya kuchuja maji aliyoitoa kwa hospitali kuu ya mkoa wa Kagera yenye thamani ya zaidi milioni 8 yenye uwezio wa kuchuja lita 6,500 kwa siku ambayo haitumii aina yoyote ya nishati. Anayepokea ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa Dr Amri Byalugaba na kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya mkoa Johansen Rutabingwa. Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Bukoba

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

je wewe umeisajili modem yako?

Sunday, June 27, 2010
Mie nikiisajali Modem yangu ya Zantel leo,wewe je.! umekwishasajili Modem yako? kama bado ni vyema ukawahi mapema,kwa sababu siku ndiyo zinayoyoma hivyo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, June 27, 2010 | | Permalink | Maoni 1

shoo love na miss ilala 2010


Vijana wa kazi wa Clouds TV wakiwa wamepozi na mshindi wa Redds Miss Ilala 2010,Bahati Chande,Bahati ameibuka na taji hilo kwa kuwapiku walimbwende takriban 17 waliopanda jukwaani na kuonyesha manjonjo yao,shindano hilo limefanyika jana usiku katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Diwani viti maalum wilaya ya Ilala,Ritha Kabati
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, June 27, 2010 | | Permalink | Maoni 1

timu ya ghana ilivyowapa raha waafrika wenzao ulimwenguni jana

Shabiki wa Ghana akifanya vitu vyake
Mpaka Ndinga zilipakwa bendera ya Ghana
Furaha kwa kila mtu

Shangwe na Nderemo kila Kona
Hongera Ghana
Go Go Ghana
Kila mtu akikuwa akisherekea kwa staili
Washabiki wakumwaga
Washabiki wa Ghana wakirusha Nyuki za Nguvu
Tottenham London kulikuwa hakutoshi
Taswira ya Tottenham jana usiku saa sita usiku


Salam kaka,

Kwa mara nyingine tunapenda kuwaletea wadau wote wa libeneke yaliojiri hapa ukerewe katika kitongoji jana usiku cha Mji Tottenham kususiana na ushindi wa Ghana.

Washibiki wote wa mpira walikusanyika pamoja na kusherekea ushindi wa Ghana kwa staili ya kipekee.

Haya ndio mambo ya Waghana na wadau wa mataifa mengine wakisheherekea na kurusha nyuki kushangilia ushindi wa timu yas taifa ya Ghana THE BLACKSTARS dhidi ya timu ya Marekani kwa Obama.

Bofya link chini kuangalia video.


Habari ndio hiyo

Mungu Ibariki Africa,

Urban Pulse Production
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, June 27, 2010 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu