EPI BESDEI YA US BLOGGER NA KUJITAMBULISHA RASMI

Sunday, February 28, 2010
Hongera kwa kutupa nafasi nzuri ya kuchangia mawazo katika ujenzi wa taifa letu.Leo jumapili natimiza miaka 44, lakini bado niko fiti, na ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema na masiha mazuri, pamoja na familia yenye amani.

Swala ambalo limekuwa likinisumbua ni kuhusu hatima ya taifa letu lililokumbwa na ufisadi mkubwa kiasi kwamba walalahoi hawana sauti tena.
Ila vijana wachache mahiri kama nabii US-Blogger, Yohanna Mashaka, Dr. Shayo, Mwanakijiji lazima tuwape pongezi kwa jitihada zao za kuielemisha jamii ya kitanzania.Nimewasiliana na Nabii Yohanna Mashaka, kadhalika na His Chief of Staff Dr. Shayo, and Vice President Mwamvitta na wamekubali kushiriki katika mjadala wetu "live" hivi karibuni. Itatangazwa moja kwa moja kupitia EATV na Clouds FM. Bado nipo kwenye harakati za kukamilisha shuguli na kutangaza mjadala mzima. Nchi ni yetu vijana kwa hiyo lazima tushirikiane. alafu niko single, kwa hiyo kama ni sista eligible basi nishtue.

Kwa maana hiyo, nimeamua kujitambulisha rasmi kwa globu ya jamii na Tanzania kwa ujumla nikijitayarisha katika kinyang'anyiro cha jimbo la Temeke. Na pia ningependa kushirikiana na vijana wa kitanzania ili tuendeleze libeneke la kuborosha utalii wa kitanzania, hasa kuitangaza nchi yetu tukiwa ughaibuni. Kwa hiyo wote wanaoniita jini, hapana ni wenu mtiifu
Happi Besdei Yangu
Dr. Mohammed Hassan Mtoro
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 3

ujumbe toka kwa mdau kwenda kwa wadau


Picha hii ilinaswa hivi karibuni na Bro Willy waWilna Int'l alipokuwa vakesheni hapa bongo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

hali ilivyokuwa tete huko london




Picha kwa hisani ya mdau mdau. eddy from birmingham london
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 5

jumapili nyingine na tuburudike na wimbo huu kutoka kwa solomoni mukubwa

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 3

kwa mazingira haya nani wa kulaumiwa.?

Pichani ni sehemu ndogo ya clip inayoonyesha mfumo mbovu wa maji taka ulioikumba sehemu kubwa ya Mikocheni,Mvua ikinyesha kidogo tu basi si balaa hilo la maji machafu/taka,kila uchochoro mimaji michafu inatiririka ile mbaya,unajiuliza mvua kidogo hivi haya maji yanatoka wapi,mbaya zaidi afadhali yangekuwa ya mvua asilimia mia,ebwanaee maji yananuka,harufu mbaya yakiwa yamechanganyikana na kinyesi,kuna sehemu nikakatiza nikakutana na watoto wanayachezea yale maji,kiukweli nilishikwa na hasira sana,kwa sababu yale maji yalikuwa yananuka vibaya sana,Nikawatimua.!

Je.! Kwa mazingira hay ni nani wa kulaumiwa.?

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 2

msikilize gie manie pia


Mambo vipi , Nilikuwa nataka kuwajulisha wapenzi wangu wote kuwa sasa hivi unaweza kudownload single yangu GO HARD - Gie Manie ft LBT online kupitia link hiyo hapo chini:http://www.mediafire.com/?mwmmyj1yy2z
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 1

Bendi ya mashujaa yaanza kwa kasi.

Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa, ELYSTONE ANGAI , akicharaza Solo Gitaa wakati wa Onyesho katika Ukumbi wa MaelezoVingunguti mwishoni mwa wikend
Baadhi ya Wacheza Shoo wa Mashujaa Band, wakati wa Onyesho lililofanyika Mashujaa Pub , Vingunguti
Baadhi ya waimbaji wa Mashujaa Band, wakati wa Onyesho lililofanyika katika Ukumbi wa Mashujaa Pub Vingun guti

Bendi ya mashujaa yaanza kwa kasi.
Na Neema Mkama Gumzo
Bendi mpya ya muziki wa dansi nchini MASHUJAA BAND, jana iliweza kushambulia jkwaa la ukumbi wa Mashujaa Pub uliopo Vingunguti Dar es Salaam ambapo Wimbo Mpya wa Moshi wa Sigara ulionekana kuwavutia mashabiki walioweza kujitokeza kutokana na kuwagusa wengi hasa mwanamuziki kijana mdogo mwenye kipaji cha hali ya juu PATIENCE NSIMBI (pasia budance) unaongelea mapenzi namna ambavyo yanaweza kutoweka kama moshi wa sigara.
Bendi hiyo ambayo ilikaa kambini kwa zaidi ya siku 40 maeneo ya kigamboni ambako walikamilisha nyimbo mpya 6 ambazo zimeanza kuwa na mguso kwa jamii kutokana jinsi zilivyoimbwa, na hivyo kudhihirisha kwamba kimya walichokuwa wamekiweka kilikuwa na mafanikio.

mkuu wa bendi hiyo ELYSTONE ANGAI ambaye ni mzoefu katika fani ya muziki alizikoga nyoyo za mashabiki mara kwa mara kutokana na uhodari wake wa kulicharaza gitaa la solo huku akisaidiwa na mwanamuziki mkongwe EDWARD ANTONY MALIKIDOGO (jadol feed force), katika kukoleza kutokana na Sauti yake kuwaingia wote walioweza kushuhudia burudani hiyo.

Aidha katika Wimbo wa pili, MWANIKE ulioimbwa kwa mchanganyiko wa lugha 3 yaani Kiswahili,Kisukuma na Kihaya pia ulionyesha kuwavutia wengi walioweza kufika katika ukumbi wa makumbusho ikiwa ni katika onyesho maalum.

“kanda ya ziwa kaeni mkao wa kula” alisema Shaaban Mpalule ambaye ndiye msemaji wa Bendi hiyo, wimbo huo umetungwa na Mwanamuziki na rapper wa bendi SIMON NGOSHA (ngosha masanja) .
Bendi hiyo inaundwa na Wanamuziki wengi wazoefu na chipukizi jumla wakiwa 25 wakiwemo 7 wenye uraia wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na wengine watanzania ,wamo pia kina dada wanaopamba jukwaa la bendi hiyo,yaani wacheza shoo,idadi yao ni 8 amabao pia ni wazoefu.

“Kazi ndiyo imeanza, ila inaonyesha matumaini makubwa kutokana na kile ilichowapa leo mashabiki waliofika hapa Mashujaa Pub, si tu kwamba nyimbo zimewakoga mashabiki wa Dansi bali pia wacheza shoo wanao mvuto kitu kilichopelekea mashabiki kuwa na hamu ya kutaka kuwaona wakiselebuka, kama ulivyowasikia mashabiki wakimwagia sifa kemukemu mcheza shoo wa kike Neema kutokana na Uhodari wake wa kuzungusha nyonga, ni chipukizi ambaye bila shaka anaweza kuwa tishio katika medani ya muziki wa Dansi ususani katika eneo lake la kujidai(Unenguaji) huyu anafananishwa na nyota wa miondoko hiyo hapa nchini Aisha Madinda”alisema Mpalule.

Na kuwataka mashabiki kujitokeza katika maonyesho yake ili waweze kushuhudia ikiwa ni pamoja na kupata baadhi ya nyimbo zilizokwisharekodiwa, ambazo tayari ziko sokoni.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 1

in memorial of alfred lukes lukumai

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

bango la mdau akiomba kura

Saturday, February 27, 2010
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 27, 2010 | | Permalink | Maoni 1

Rais jakaya Kikwete ashiriki Mazishi ya Balozi Daudi Mwakawago

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Seif Shariff Hamad wakati wa mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia Marehemu Balozi Daudi Mwakawago yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni.Katikati ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Wiliam Mkapa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Balozi Daudi Mwakawago wakati wa mazishi ya Mwanasiasa huyo mkongwe yaliyofanyika katika makaburi ya kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha kwa hisani ya Freddy Maro)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 27, 2010 | | Permalink | Maoni 0

hitma ya mzee kawawa yafanyika leo nyumbani kwake madale

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisamiliana jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Captain John Chiligati na Kingunge Ngombale Mwiru. Rais Kikwete alikutana na viongozi hao katika hitma ya Mzee Rashid Kawawa nyumbani kwake Madale jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa kwenye hitma ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa leo jijini Dar es salaam , wengine ni Mtoto wa Marehemu Vita Kawawa(kulia) na kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Mussa Salum.

Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria hitma ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete.

Baadhi ya wakina mama wakiwa katika hitma ya hitma ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa iliyofanyika leoa jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete.Picha zote kwa hisani ya Tiganya Vincent-MAELEZO
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 27, 2010 | | Permalink | Maoni 1

msikilize nyota ndogo kutoka kwa watani zetu

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 27, 2010 | | Permalink | Maoni 2

SHEREHE ZA MIAKA 33 YA CCM KUADHIMISHWA UK

      CHAMA CHA MAPINDUZI

TAWI LA UINGEREZA

SHEREHE YA KUZALIWA KWA

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

MIAKA 33 YA CCM

Wanachama Wote - C C M

Wakereketwa Wote - C C M

Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote

Tarehe: 06/03/2010 Saa: 10 jioni Hadi Saa 5 usiku

WAPI:

UKUMBI WA: THE WAREHOUSE

1 CUMBERLAND ROAD

READING

RG1 3LB

Mgeni Rasmi

Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara: Mhe Pius Msekwa

Watanzania ambao wangependa kujiandikisha, mnaombwa kuleta picha zenu za passport size mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya uanachama ya mwaka mzima).

Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:

Moses Katega - 07727475313

Victor Mgoya - 07501083328

Maira Migire - 07799212095

Wote Mnakaribishwa - Kutakuwa na Vinywaji, Vitafunio, na Muziki Baada ya Shughuli Zote.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, February 27, 2010 | | Permalink | Maoni 3

Mwanamziki Hamisi Kitambi ! Hatunae Tena!

Friday, February 26, 2010


Mwanamziki mkongwe HAMISI KITAMBI amefariki dunia leo 26 February 2010 Dar-es-salaam,
MAZISHI YATAFANYIKA JUMAMOSI saa 7.00 mchana 27-02-2010 MAGOMENI,Ifunda ,jirani na shule ya
Mzimuni,Jijini Dar-es-salaam.
Mwanamziki mkongwe wa dansi Bw.Hamisi Kitambi,amefariki dunia siku Ijumaa alfajiri ya tarehe 26/02/2010
katika Hospitali ya Muhimbili.
Marehemu aliwahi kupigia bendi za Msondo Ngoma ,kabla ya kupata maumivu ya mguu yaliotokana katika ajali
alipokuwa safarini na bendi ya msondo ngoma .
marehemu pia alikuwa mwanamziki nyota enzi za Tabora jazz,ambako alipigia bendi ya Tabora kabla ya kuhamia
Juwata Jazz sasa Msondo Music band.
Kwa taarifa zaidi tafadhali mnaweza kuwasiliana kwa simu na familia ya marehemu kwa simu namba 0713 802370 Almasi Kassanga.
au Bi.Mwamini Kitambi simu namba 0712 217740
Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi
Amin
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 26, 2010 | | Permalink | Maoni 0

rais jakaya kikwete aifariji familia ya marehemu balozi daudi mwakawago

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia marehemu Balozi Daudi Mwakawago nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi.Daisy Mwakawago mjane wa Marehemu Balozi Daudi Mwakawago aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam.Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho jijini Dar es Salaam.Rais alikwenda nyumbani kwa marehemu kuifariji familia yake.Marehemu ameacha mjane na watoto watatu Lulu Mwakawago,Kie Mwakawago na Mtage Mwakawago (picha na Freddy Maro)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 26, 2010 | | Permalink | Maoni 0

kamuzi la twangazz.!

Enzi hizo wakati bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta ilipokuwa imetimia kikweli kweli,hapa ilikuwa ikitumbuiza kwenye tamasha la siku ya Ukimwi Duniani,lililofanyika katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 26, 2010 | | Permalink | Maoni 2

jiachie kijanja na bongo street wear,mzigo mpya umeingia

T-shirts & Tops
T-shirts
Toka chicha na mwenye furaha na Bongo Street Wear



Wakali wa Bongo Street Wear wamekuja na mzigompya kabisa, wanapatikana kwenye duka lao jipya linalopatikana Mwenge Opp na kituo cha Polisi.Unaweza kuwapata kwa mawasiliano yao hapa chini :
SHOPING INFORMATION
Dar es Salaam-0713 49 40 49/0784 752515.
Morogoro mjini:Super Tech 0718 015 532.
Mzumbe University:0715 335 555.
UDSM (Aru) 0715 658 198.
Arusha 0715 655 559

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 26, 2010 | | Permalink | Maoni 1

rais kikwete arejea dar

Rais Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka nje ya nchi ambapo alikuwa katika ziara ya kikazi Mashariki ya Kati. Mwingine katika Picha ni Kingunge Ngombale Mwiru.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, February 26, 2010 | | Permalink | Maoni 0

kanumba kutikisa tena anga ya filamu na "THIS IS IT".

Thursday, February 25, 2010
"Mashabiki wangu na wadau mbalimbali hii ni Filamu yangu mpya itakayotoka hivi karibuni, imetengenezwa chini ya kampuni yangu ya Kanumba The Great Film, hivyo kaeni mkao wa kula mengi nitawajurisha hivi karibuni, hii si ya kukosa. Akhsanteni sana",hayo si maneno ya JIACHIE bali ni kutoka kwa The Great mwenyewe ukitaka kufahamu kuhusu ujio wa filamu yake na mambo mengine yahusuyo tasnia ya filamu basi bofya Kanumba The Great
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

rais kikwete afungua mkutano mkuu wa PCCB jijini Mwanza

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo unaofanyika mjini Mwanza leo asubuhi.Picha kwa hisani ya Freddy Maro.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 1

chagua chagua leo jioni mwenge


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 1

INFINITY ENT'S pres, SWAGGA NIGHT

INFINITY ENT'S pres, SWAGGA NIGHT. Sat 13th, MAR 2010 at SPICE LOUNGE, 3 Savoy Crecent, Theatre District, MILTON KEYNES. mk9 3pu,DJ DOUBLE T & Dj BILLY will make it happen.BONGO FLAVAS, R&B, RAGGA, OLD SKOOL. Dress Smart to impress. 10Pm till Late, Admission: £5 B4 12.VIP TICKETS AVAILABLE AT THE DOOR. Mishemishe sio mchezoo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Utambaji wa Hadithi Jukwaani!

Karibu Soma mkahawani ukutane na Ghonche Materego mtambaji mahiri wa hadithi jukwaani…
Huu ni utanzu mkongwe ulioshamiri enzi za mababu na bibi zetu ambao umehuishwa kwa kutumia mbinu za sanaa za maonyesho.
Onyesho litasindikizwa na majadiliano, maonyesho ya vipaji vya papo kwa papo na ushairi wa kisasa.
Muda: 12:00 alasiri hadi 2:00 usiku
Tarehe: 26/02/2010 (IJUMAA).

Uenzi utamaduni wako, furahia utamu wa neno
Njoo pia uburudike kwa vinywaji moto na baridi, vitafunwa vya aina mbalimbali kwa bei sawa karibu na bure mkahawani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mjadala wa kichapo cha chelsea !

Vichwa mahiri vya Mjengoni "Clouds Fm", toka shoto ni mtangazaji wa kipindi cha michezo Sports Extra na pia ni mchambuzi wa masuala mbalimbali ya michezo Shafii Dauda,kati ni mtangazaji wa kipindi cha Jahazi akiwa sambamba na swahiba wake Gadna G Habash,Ephrahim Kibonde pamoja na Dj wa kitambo Dj Venture ambaye pia hukamua mangoma pale Mzalendo Pub.Pichani walikuwa wakijaribu kubadilishana mawazo kuhusiana na gemu ya jana kati ya Chelsea na Inter Milan
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

miss vodacom tanzania 2009/10 miriam gerald apandishwa tena kizimbani


Miss Vodacom Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na mpenzi wake Kenedy Victor ‘Kenny’, leo wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni kwa mara nyingine, ambapo kesi yao ya kushambulia na kuharibu mali na vyombo vya muziki vya bendi ya Volcano Sound, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba ilitajwa.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21 na watuhumiwa hao wanaendelea kuwa nje kwa dhamana.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

hussein machozi aibuka na za mwizi 40



Mambo vipi? Napenda kukufahamisha kuwa Hussein Machozi ametoa tena singo yake nyingine inayoitwa ZA MWIZI 40, ambao umeachiwa rasmi hivi karibuni katika radio stations. wimbo huu unapatikana katika album yake ya KWA AJILI YAKO.
Hii ni single yake ya 3 kutoka katika album hiyo, single mbili zilizotangulia ni pamoja na KWA AJILI YAKO na UTAIPENDA. Kwa sasa tuko katika hatua za mwisho za kushot video ya wimbo huo, na tunategemea kuifanyia Dar es Salaam na Adam Juma wa Visual Lab wiki ya kwanza ya March, na video itatoka mara tu tukikabidhiwa na Adam.
SONG'S DETAILS
Track Name: ZA MWIZI 40
Singer: HUSSEIN MACHOZI
Produced by: AMBA & KID BWOY
Written by: HUSSEIN MACHOZI
song arranged by: HUSSEIN MACHOZI & KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ / AB RECORDS
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Mabalozi wamuaga Rais Karume

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akizungumza na mabalozi wateule wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi za nje,(katikati)Prof Abillah Omar,Balozi nchini Saudi Arabia na(kushoto)Dr James Mwasi nchini Bujumbura-Burundi,waliokuja kumuaga Rais jana,Ikulu Mjini Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman Ikulu Zanzibar.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Shaggy alipotua bongo

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani/Jamaica Shaggy alipotua jijini dar na kufanya bonge la shoo ndani ya viwanja vya Lidaz Club,hii ilikuwa mnamo mwaka 2008,ambapo pia alifanya uhamasishaji mkubwa kwa wadau wa muziki hapa bongo namna ya kukisaidia kituo cha watoto wenye vipaji cha THT,ikiwemo na suala zima la kuwapatia vyombo,yote hiyo, Shaggy alikubali kufanya kwa moyo mmoja baada ya kuona juhudi kubwa zikifanyika za kukuza vipaji katika kituo hicho ambacho kwa sasa,ama kwa hakika kimekuwa mfano wa kuigwa.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 2

MPIGIE KURA MDAU MAKULILO, Jr. KATIKA SHINDANO HILI

Mdau,
Kuna mashindano yafahamikayo kama DELL SOCIAL INNOVATION COMPETITION ambayo yanashindanisha social issues (ideas) ambapo mshindi atapata dola 50,000 kuweza kutimiza project yake ambayo ameelezea. Mimi ni mmoja kati ya washindani.
Hivyo naomba watu waweze kunipigia kura na kutoa maoni yao ambayo yatasaidia kuingia katika 10 bora na hatimaye kuinuka kidedea. Unachotakiwa kufanya ni fungua tovuti hii hapa chini, na kisha jisajiri ili uweze kutoa maoni yako na kupiga kura yako (Join the community to vote and comment on your favorite ideas! )
Unaweza kuona ideas za watu wengine pia hapa http://www.dellsocialinnovationcompetition.com/apex/ideaList?lsi=1
MAKULILO, Jr.
San Diego, CA
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 1

tuburudike na fleva toka kwa qchilla

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mtoto wa kiafrika emepoteza haki yake ya msingi?


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, February 25, 2010 | | Permalink | Maoni 0

MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA NA VIKOSI WAAGIZWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI

Wednesday, February 24, 2010

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi hapa nchini, wameagizwa kutoa ushirikiano na kujenga ubia na Waandishi wa Habarí ili kuwawezesha kutekeleza wajibu wao kama wadau muhimu wa kiutendaji Kitaifa.


Agizo hilo limetolewa na Makamishna wa Polisi kwenye mkutano wa Maafisa Wakuu wa Jeshi hilo mjini Dodoma wakati wa mjadala juu ya ushirikishwa wa Vyombo vya Habari katika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mpango wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi.


Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai nchini Kamishna Robert Manumba, amesema kuwa ni wajibu wa kila Kamanda wa Polisi hapa nchini, kuhakikisha kuwa anatoa ushirikiano unaostahili kwa waandishi hao ili nao wawezesha kutimiza wajibu wao wa kuwaelimisha wananchi juu ya yale yanayotokea kila siku.


Naye Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Paul Chagonja, amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa waandishi bandia maaruka kama Makanjanja, ipo haja ya kila mmoja wao kuwa na Kitambulisho cha Chombo anachokifanyia kazi pamoja na kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) ili kuondoa utata.


Amesema utaratibu huo ukifuatwa kutapunguza furusa ya kuwepo kwa waandishi bandia ambao wamekuwa wakichafua uhusiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi na Biombo vya Habari kwa waandishi wasio wajibika popote kuandika abarrí za uchochezi ama zinazowachafua vatu fulanifulani.


Kwa upande wake Mkuu wa Mipango na Bajeti kwenye Jeshi hilo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP John Masawe, amesema ipo haja ya Waandishi wa Habari nao kupewa mafunzo juu ya mpango wa Polisi jamii ili waweze kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya mpango huo.


Kamanda Masawe amesema kuwa waandishi wakielimishwa itakuwa ni msaada mkubwa kwa Jeshi la Polisi katika kueneza mpango wa Polisi Jamii kwa wananchi katika kutoa taarifa za kihalifu.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amewataka Makamanda kutogombana na Waandishi wa Habari na badalayake wahakikishe wanashirikiana kwa kuwapa taarifa sahihi na kwa wakati muafaka.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, February 24, 2010 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu