PREDOCTORAL FELLOWSHIPS : International Security Studies at Yale (USA}

Sunday, January 31, 2010
International Security Studies, Yale University – International Security Studies at Yale
2010-11 SRF Pre-Doctoral Fellowship
Location: Connecticut, United States
Institution Type: College/University
Position Type: Doctoral Fellow

——————————

Main Category: Diplomatic/Military History
Secondary Categories: World History
Russian/Soviet History
Political Science/International Relations
Policy and Political History
Latin American History
Japanese History
Imperial or Colonial Studies
Global Studies
German History
European Studies
European History
Early Modern History
Classical Studies
British History
Atlantic Studies
Asian History or Studies
African and Middle Eastern History
International Security Studies at Yale (ISS) will award up to two Smith Richardson Foundation Predoctoral Fellowships in Security Studies beginning in the Fall semester of 2010, contingent upon available funding for this program. These fellowships will have a term of one academic year.
These Fellowships will provide an opportunity for advanced doctoral candidates from universities other than Yale in the field of security studies, with particular emphasis on international, diplomatic, and military history, to benefit from a year at Yale and involvement with the ISS community. Fellows must be in residence in New Haven or its environs. They must have largely completed the archival research for their doctoral dissertation: Fellows will be expected to use this Fellowship to make substantial progress in writing their dissertation. Applications from non-U.S. citizens are welcome, but successful applicants bear final responsibility for all immigration-related issues.


Fellows will have full access to Yale’s library and other academic resources, but they will not be eligible for Yale financial aid or degrees, nor will they be allowed to take or teach classes. The stipend will be $23,000 per year, with an additional $3,000 in research expenses. The Fellowship will provide shared office space and single membership in the Yale Health Plan if the Fellows home institution does not provide transportable health coverage.
Please submit a vita, a research proposal (describing how the Fellowship will be used), transcripts, a short (no more than 50 page) writing sample, and two letters of reference (one should be from the applicants dissertation advisor) to Susan Hennigan, Administrator, International Security Studies, Yale University, PO Box 208353, New Haven, CT 06520-8353. The deadline is March 1, 2010. Finalists may be asked to visit Yale for an on-campus interview, or to participate in a telephone interview. Yale University is an AA/EOE. Female, minority, and handicapped candidates, and veterans are encouraged to apply.
Contact Info:
Susan K. Hennigan,
Administrator International Security Studies
Yale University
PO Box 208353
New Haven, CT 06520-8353
MAKULILO, Jr.
San Diego, CA
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 6

sakata la jerry muro,taarifa kamili kutolewa rasmi kesho na jeshi la polisi


Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Jerry Muro (pichani juu kulia) kwa tuhuma za kudai fedha kwa njia ya vitisho.

Muro anadaiwa kumtisha aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo Michael Wage ambaye hivi karibuni alisimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa tuhuma za ubadhilifu pamoja na viongozi wengine wa Halmahauri ya Wilaya Bagamoyo.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Suleimani Kova alikiri jeshi lake kumshikilia Muro na kuwa alimtishia Wage kuwa yeye ni Ofisa wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) na kumtaka atoe fedha Sh milioni 10.

“Polisi inamhoji Muro dhidi ya tuhuma hizo na mahojiano yakikamilika taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na maelezo zaidi nitayatoa kesho wakati wa mazungumzo yangu na waandishi wa habari” Kova alisema.

Aidha blogu ya Watu ilimwona Bingwa huyo wa Tuzo za Uandishi wa Habari 2009 Tanzania akiwa polisi na mkononi ameshikilia bahasha tatu pamoja na kamera ya Video.

Ilipomhoji juu ya kuhusika na tuhuma hizo alikana na kudai kushangazwa kuwekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa alipigiwa simu na mtu kupewa taarifa kuwa kuna kazi katika Hoteli ya City Garden.

“Kaka nilitaarifiwa tu kama ujuavyo kazi zetu kuwa kuna kazi City Garden niakaamua kwenda, lakini baada ya kufika tu nilishangaa nawekwa chini ya ulinzi na askari kanzu ambao ndiyo walionifikisha kituoni hapa bila ya kunitajia kosa lanmgu. ” alilonga Muro.

Kwa upande wake Wage alidai kuwa mtuhumiwa anatumiwa na watu wengine ambapo juzi alimpandisha katika gari lake na kumfunga pingu kisha kumtaka atoe Sh milioni 10 na kwa kuthibitisha kuwa alikuwa ndani ya gari hilo alidai kuacha miwani yake yenye mikanda myeusi.

Polisi ilipomhoji Muro kama anazo pingu alikiri kumiliki pingu pamoja na bastola ambapo baada upekuzi katika gari lake lenye namba za usajili T 545 BEH polisi walikuta pingu hizo pamoja miwani iliyosemwa na mlalamikaji.

Muro ameibuka kuwa mtangazaji mahari kwa mwaka 2009 hadi kujinyakulia tuzo ya Mwandishi bora wa mwaka kupitia vipindi vyake vya Televisheni vya USIKU WA HABARI vinavyorushwa katika kituo cha TBC1 kila siku na kabla ya kuhamia hapo alikuwa kituo cha ITV na aliendesha kipindi cha RIPOTI MAALUM.

Miongoni mwa mambo aliyokuwa akirusha katika vipindi hivyo ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ukiukwaji wa sheria.

Polisi ni wahanga wakuu katika vipindi hivyo kwani mara mbili amewatoa Polisi Usalama barabarani wakiomba na kupokea rushwa hadharani kutoka kwa madereva wa malori na mabasi ya mikoani. Habari kwa hisani ya Fathere Kidevu
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 5

mhanjo wangu wa mwisho kiwekend wikend ufukweni

Hapa wadau msilete nongwa tena kama zile za yule dada nanihiiiii oohooo.!
Mie nikiwa nimepozi kimtindo nikicheki yanayoendelea ufukweni,ama kweli pwani rahaa.


Baada ya kutoka hapo kwenye michezo basi nikamalizia sehemu ya kupigwa upepo,ambako mara nyingi waubani huambatana huko kuliwazana kwa namna moja ama nyingi,kama uonavyo baadhi ya picha.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 5

mhanjo wa pili wa leo kiwikend wikend










Baada ya kuburudika Lidaz Club nikatia timu sehemu ya michezo mbalimbali katika viwanja vya Tanganyika Pekaz,nako kila jumapili huwa kunachangamka sana,kunakuwepo na michezo kibao kama uonavyo pichani,wikend inakwisha safi kabisa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

kumbe huwa pananoga hivi


Leo jioni nilipita Lidaz Club Kinondoni jijini Dar kujionea yanayojiri pale,kila jumapili kunakuwepo na bonanza la muziki,bendi ya muziki wa dansi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta ikitumbuiza jukwaani huku wapenzi wa bonanza hilo wakiburudika safi kabisa,offcoz kumbe panakuwa pananoga vile ebwanaee ,basi ntakuwa never miss kimtindo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

mdau noamba utafakari picha hii kwa makini

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

tuburudike basi na kibao hicho na jumapili wadau


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 2

last episode ya umodo na nyota wake wa mchezo ni happy witney

Huyu ndiye mshindi wa shindano la UMODOTZ,Happywitney Gumbo baada ya kuwatupa kule washiriki wenzake 11,onesho hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.Kimsingi ni shindano ambalo kiukweli lilifana na lilivutia sana,kikubwa Bro Taji ukumbuke kwamba mwanzo ni mgumu kwa unachokifanya,lakini naamini kwa juhudi na ubunifu wako ulioutumia na kuhakikisha onesho hilo linafana,basi safari yako bado ni ndefu lakini inaonekana kuwa na matunda matamu (ingawaje hakuna matunda matamu bila miba),ambayo hapo mbeleni hata jamii italikubali onesho hili na kulifanya liwe onesho mojawapo kubwa na lenye mafanikio kuliko mengine yote hapa Tanzania,kama kuna kasoro zozote zilizokuwepo basi ni kibinadaamu tu lakini naamini kabisa shindano litakalofuata wengi hawataamini.Bro Taji JIACHIE inakupa BIG UP sana kwa ulichokifanya,inasema SAFARI NI HATUA.
Mshindi wa shindano hilo Happywitney akihojiwa na mtangazaji wa kituo cha Mliman TV huku mama yake akimuangalia kwa msisitizo safi kabisa huku akiwa amemkumbatia
Mshindi wa onesho la UMODOTZ Happywitney Gumbo akikabidhiwa cheki yake la mbili nje ya mkataba wake wa kazi wa mwaka mmoja alioahidiwa kutoka Shear Illusions ambao ndiyo wadhamini wakuu wa onesho hilo,anayemkabidhi ni muwakilishi wa shear Illusions aitwaye Neema,shoto ni mratibu wa onesho hilo Magesa pamoja na mwandaaji kulia, Taji Liundi.Washiriki wengine walipewa vifuta jasho pamoa na vipodozi mbalimbali kutoka Shear Illusions
Happywitney Gumbo akilakiwa na washiriki wenzake mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mshindi wa onesho hilo
Mshindi wa jumla wa shindano la UMODOTZ,Happywitney Gumbo akiwa haamini masikio yake mara baada ya kutajwa kuwa yeye ndiye kinara wa onesho hilo usiku wa kuamkia leo
Pichani shoto ni Modo Nshoma akikabidhiwa shilingi elfu hamsini kumpongeza kwa kuwa msichana wa kwanza kukubali kwende kupima Ukimwi wakati wa mchakato wa shindano hilo likiendelea.
Muaandaji wa onesho la Umodotz Taji Liundi akiweka sawa mchakato wa kumtaja mshindi wa onesho hilo usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya GIRAFFE OCEAN VIEW
Pichani ni baadhi ya wadau ambao Blog ya Umodo ilipata ushauri kuhusu onesho hilo akiwemo Steven Kanumba(filamu), Slyvia Shao(Urembo) na mbunifu Kemmi Kalikawe (mitindo) ambao wanawakilisha nyanja mbalimbali zinazoshabiiana na maswala ya mitindo,wengineo pichani shot ni Yusuf,kulia Taji Liundi ambaye ndiye Muaandaji na mratibu wa onesho hilo,msaidizi wake Magesa wakiwa jukwaani kabla ya mshindi kuwekwa hadharani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 1

4rth episode ya umodo katika vazi la ufukweni

Mamodo wakiwa katika picha ya pamoja usiku wa kuamkia leo mara baada ya kukatiza jukwaani na vazi la ufukweni ambali lilionekana kuwavutia wengi.Lakini ukumbuke katika mchakato huu anatafutwa kinara mmoja tu ambaye ataibuka na mkataba mnono wa mwaka mmoja kutoka Shear Illusions pamoja na kupata fursa mbalimbali za matangazo kwenye magazine na hata kwenye mabango.










Mamodo wakipita jukwaani na kupozi wakiwa wamevalia mavazi yao ya ufukweni kama uonavyo pichani
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

3rd episode ya umodo katika vazi la uminifu tena

Mbunifu wa mavazi mzoefu kutoka Naledi Fashions,Kemi Kalikawe (njano masikioni) akiwa na walimbwende wa umodo jukwaani,wakiwa wamvalia mavazi yake ya ubunifu safi kabisa





Mambodo waki[ita jukwaani wakiwa katika vazi la ubunifu
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0

second episode ya umodo katika vazi la ubunifu

Pichani baadhi ya mamodo wakiwa wamepozi jukwaani na mavazi ya ubunifu yaliyobuniwa na mbunifu chipukizi wa mavazi aitwaye Mgesi pichani wa tatu kulia.





 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 31, 2010 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu