Friday, December 31, 2010

kizazaa cha wafanyabiasha wa mboga mboga mjini arusha leo

Wafanyabiashara wa mboga mboga na matunda wakitimka mara baada ya kuvamiwa ghafla na askari wa jiji leo asubuhi kwenye soko kuu la Kilombelo jijini Arusha.Wafanyabiashara hao wamekuwa wakitimuliwa sehemu ya eneo hilo kwa madai kuwa wanafanya biashara sehemu isiyoruhusiwa. Kwa mtazamo wangu wafanyabiashara hawa ambao wanaonekana ni wengi sana wanapaswa kutafutiwa eneo maalum la kufanyia shughuli zao ili kuepukana na adha ya kusumbuliwa kila siku na askari wa jiji.

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

Kama serikali inahitaji kuongeza makusanyo ya kodi,inampango gani?

Njia nyingi zipo za kukuza uchumi wa nchi,ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na ushindani wa soko la EA.

Wafanya biashara kama hao, wanaitaji kuwezeshwa kuendesha biashara zao kwa ufanisi, lkn cha ajabu serikali aifikirii hilo.

Serikali inapiga kelele kila siku kuhusu utoaji wa mafunzo na mikopo kwa wafanya biashara wadogo! kwanini wasiandalie sehemu na vitendea kazi pia?

Najua serikali italifumbia macho swala hilo sbb mbunge wa Arusha ni wa upinzani!

Serikali imeshindwa kazi, mawazo na itikati zao zimepitwa na wkt, tunahitaji mabadiliko makubwa ya kileo, acheni kulala