


Askari wa Usalama Barabarani akisaidia kuzima moto uliokuwa ukiteketeza sehemu ya jengo hilo huku mlinzi wa mahakama hiyo akiangalia.
Mlinzi wa jirani na jengo la Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akizima moto uliokuwa ukiteketeza sehemu ya jengo hilo huku mlinzi wa mahakama hiyo akiangalia wakati trafiki akifanya mawasiliano kwa ajili ya msaada zaidi.Picha na Robert Okanda.
Kuna Maoni 4 mpaka sasa.
Halafu wananchi tukilalamika kuwa hela yoyote ile inayoliwa na mafisadi inasababisha mambo kama haya, maana ebu fikiria hela ya EPA, KIWIRA, TAX EXEMPTIONS, RADA, DOWANS, RICHMOND, MAGEREZA, NDEGE YA RAISI, TRA, KAGODA, MEREMETA, MASHANGINGI, BAJETI YA CHAI NA VITAFUNIO, ATCL, TANESCO, BOT n.k.
Kama hela zote hizo zingetumika kwenye miundo mbinu, kununua magari ya fire na kuboresha jeshi la zimamoto, sidhani kama tungekua na majanga kama haya.
Hela yoyote inayoibiwa serikalini lazima utapata upungufu kwenye maisha ya mwananchi wa kawaida.
Ila kila tukilalamika hatusikilizwi na CCM bado wanapigiwa kura tu kuendeleza mambo kama haya.
Just on time. Kila siku Trafiki wantukamata hatuna vitank vya kuzima moto kwenye magari, Mbona huyu trafiki kasimama tu kama vile yupo kuhakikisha kila kitu kinateketea.
Inatia uchungu sana pesa ya mkulima.
mimi wasiwasi wangu ni huyo anayesemekana ni mlinzi wa jengo, mbona yeye ndio anauangalia tu moto kama vile kauwasha kuchoma takataka! au kuna walakini hapo. yaani mlinzi wa jengo jirani na trafiki ndio wanajituma sana kuzima moto, kulikoni hapo?
Afu mtoto wenyewe mbona unawakia nje?Huu lazima umawashwa huu. Huyu mlinzi lazima anajua. Mazingira yanatatanisha
Post a Comment