728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, December 2, 2010

  Breeking Newws:Clouds FM yaibomoa redio one.!

  Kutoka kulia ni Jimy Jam,Anord Kayanda,Milad Ayo (chuma kipya mjengoni),Zamaradi Mketema,Gea Habib,Sofia Kessy pamoja na pia tukiwa tumepozi katika picha pamoja leo chana ndani ya Mjengo wa Clouds Media Group mara baada ya kikao cha kuvitambulisha rasmi vichwa vipya kwa ajili ya makamuzi mapya ya Clouds FM 88.4
  Milad Ayo aliyekuwa mmoja wa watangazaji mahiri kutoka redio ONE,akiwa amepozi kwenye kikao rasmi cha utambulisho wake mchana huu mbele ya wafanyakazi wote wa Clouds Media Group.
  Kichwa kingine kipya rasmi ndani ya Clouds FM 88.4 Regina Mwalekwa a.k.a Mziwanda ambaye nae pia ametokea redio ONE,akitambulishwa mbele ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group mchana huu.
  Kichwa kingine mahiri kabisa ndani ya Clouds FM 88.4 Asmah Makau akiwa amepozi mchana wa leo wakati alipokuwa akitambulishwa rasmi na uongozi wa Clouds Media Group mbele ya wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.
  Mtangazaji mahiri wa Clouds FM Gadna G Habash ambaye jana ametangaza kuachia ngazi kazi ya utangazaji mjengoni hapo, akipongezwa na wafanyakazi wenzake mara baada ya kikao kifupi cha uongozi na wafanyakazi kufanyika mchana huu.
  Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wa kampuni hiyo leo mchana alipokuwa akimtaja Gadna G Habash kuwa ni mtangazaji mahiri ambaye atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa namna moja ama nyingine katika kampuni ya Clouds Media Group.
  Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua ambo mbele ya Wafanyakazi wa kampuni hiyo leo mchana alipokuwa akitoa tamko rasmi la mabadiliko mapya ya watangazaji wapya na mikakati mingine mipya kabambe kwa ajili ya kulisongesha guruduma la maendeleo la Clouds Media Group kwa ufanisi mkubwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  6 comments:

  1. Hongera sana mwana wa HABASH. Umetazama mbali na umeact. Mjengoni kwa sasa mmmmmmmmm! huku nje tunadhani ni mahali MAKINI but??????

   ReplyDelete
  2. Milad Ayo inaonekana ulikuwa unapeeenda sana kujiunga na CLOUDS?nilikuwa nakuona kwenye hafla mbali mbali za Clouds kumbe ulikuwa unajikomba kamba Zito anavyojikomba kwa JK....aya tena, mboga mboga Anti virus atawashika mwanzo mwisho.

   ReplyDelete
  3. Nasikia na Maulid Kitenge anataka kuhamia Clouds lakini kataka dau la one million ha ha haaa!

   ReplyDelete
  4. Asmah Makau umetuliaaaaaaaaa, Mash'Allah

   ReplyDelete
  5. Radio one hawana jipya sasa. Deo hawezi kitu na mtakalia majungu tu wenzenu wanasonga mbele.

   Lakini hebu tujiulize Radio one kuna nini hasa?? Manake watangazaji wengi wazuri wameondoka kwisha kazi.

   Poleni sana na hongereni clouds wafundisheni kazi hao radio one.

   ReplyDelete
  6. Anonymous: Wa juu hapo nakubaliana na wewe kwamba Radio One kuna nini? mimi nilishangaa kusikia eti jamaa (Rweyunga)ndo mkurugunze, kwanza shule hana na majungu kibao. Ila nakwambia ukweli pamoja na mambo yote, Radio One haijawahi kutetereka, so kuondoka hao wala si kitu, kuna vichwa vilikuwa hapo na viliondoka long-time na hamna cha ajabu kilicho tokea, so Clouds wala msijidai kama mmeibomoa Radio One, kwa kuwa haijawahi kubomolewa japo waliondoka watu kama Mikidad Mahmood, Taji Liundi, Mike Mhagama, Flora Nducha, Blandina Muongezi anti ndina,Huyo mkurugenzi wenu wa vipindi Sebastiani Maganga, Abobakar Lyongo, Sunday Shomary, Masoud Masoud, Charles Hilary, Julius Nyaisangah nyinyi...., eti kuondoka Reginna na Milad ndo mnaona mmemaliza,jamaa hao achana nao, ni jeuri, ukiondoka wanatafuta vijana wanapachika na kazi inaendelea mpaka nyinyi mnawaona na kuwatamani. Tena na kwambia hao wamechemka kuja hapo maana wameruka kinyesi na kukanyaga haja ndogo, maana watu wakiondoka hapo Radio One huwa kawaida wana kwenda level nyingine, kama kutangaza wanakwenda kutangaza vituo vya kimataifa,kama unabisha fuatilia hao nilio wataja wako wapi, ama fuatilieni vijana wadogo waliopita Radio One na kuondoka wako wapi sasa. Namuhurumia sana Regina kwa umri wake amesha haribu, sasa hapo atafanya nini HACHENI HIZOO?? alipaswa sasa hivi awe kwenye organisation ya maana kwa umri wake, afadhali huyo Milad bado mdogo ameona aende huko kwa sababu anadhani umjini lazima uwe na Clouds, na atapata mademu wengi n.k. na pia ana nafasi ya kurekebisha makosa yake, but Regina Mh! Kwa mshahara gani wanaopewa hapo Clouds. Nina uhakika hata milioni moja haifiki kudadadeki. Na wewe Michuzijr usibanie maoni yangu maana hata sijui unafanya kazi gani hapo.

   ReplyDelete

  Item Reviewed: Breeking Newws:Clouds FM yaibomoa redio one.! Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top