Thursday, December 30, 2010

Bobby farrell wa Boney M afariki dunia.!

Bobby Farrell wa Boney M wakati wa uhai wake

Bobby Farrell wa Boney M afariki dunia mjini St.Petersburg ,Urusi


Bobby Farrell (61) alikuwa mwanamziki mashuhuri katika miaka ya 1970s kutoka kundi maarufu enzi hizo Boney M,Mr.Bobby Farrell amekutwa amefariki dunia katika chumba cha hotel aliyofikia mjini St.Petersburg,nchini Urusi.

Mwanamziki huyo alikuwa katika ziara ya kimziki nchini urusi,maiti yake iligunduliwa katika chumba cha hotel aliyofikia baada ya kumaliza show zake.idara ya usalama ya mji wa St.Petersburg umeunda kamati maalumu kuchunguza chanzo
cha kifo cha Bobby farrell.

Marehem Bobby Farrell (61) alikuwa mwanamziki anayeongoza safu ya mbele ya iliyokuwa bendi maarufu duniani Boney M,ambapo alifanyakazi na wanamziki Maisie Williams,Liz Mitchel na Marcia Barret.

Kundi la Boney M lilijizolea umaarufu kila kona duniani kutokana na umahili wa nyimbo zake kutingisha katika madisco na redio za kimataifa,Kundi hilo lilikuwa na maskani yake nchini Ujerumani na kuweza kupiga tour katika kila kona duniani.

Baada ya kundi la Boney M kusambaratika marehem Bobby Farrell alihamishia makazi mjini Amsterdam,nchini uholanzi.

Bobby Farrell mwanamziki mtanashati aliyetamba na kundi la Boney M hatunae tena!!!

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.