Wednesday, December 29, 2010

andrew chenge ahukumiwa miaka 3 au kulipa faini ya sh.700,000/=

Mbunge wa Bariadi na aliyewahi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali Mh Andrew Chenge leo amehukumiwa kifungo cha miaka 3 au kulipa faini ya shilingi 700,000/= na mahakama ya Wilaya ya Kinondoni baada ya kukutwa na hatia ya kusababisha vifo kwa ajali. Hata hivyo Mh Andrew Chenge amelipa faini hiyo ya shilingi laki 700,000/= na kuachiwa huru. Hukumu hiyo imetolewa na hakimu wa mahakama hiyo Bw.Lusema na Mh. Andrew Chenge alikuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Simon Mponda.

Kuna Maoni 9 mpaka sasa.

Umesababisha Vifo, umeua... unaambiwa ulipe fine ya sh Laki Saba... kwakweli. vitu vingine viangaliwe.. nchi nyingine ukionekana umesababisha kuwapotezea watu maisha unafungwa kifungo cha maisha..

kweli Tanzania inaongozwa na kanuni, wala hamna katiba, Ingekua ya mkulima miaka 15 na faini ya milioni kadhaa. hapo sijui hiyo laki saba ni gharama za mazishi ya watu wawili au ni fidia yao, ama ni rambirambi kwa wafiwa. Wewe mwandishi wa habari hii tueleze hiyo laki saba hakimu kasema ni ya nini?

nchi gani hiyo, hiyo ni traffic case afungwe maisha kwa sheria ipi watu kudandia treni kwa mbele hata sheria hawajui, au tufanye kaua bila kukusudia je adhabu yake pia itakua kifungo cha maisha????? wacheni ushabiki mambo hamyajui kuleta fujo tu

at least tz wamejitaidi kumuadhibu mtu aliyeisababishia nchi hasara ya mabilioni ya fedha, japokuwa hakuna uwiano wa adhabu aliyopewa na makosa aliyotenda. Bado kuna kesi ya rada anatakiwa awajibishwe pia.

Traffic case gani wewe? Marekani kama uzembe wako umesababisha, unakuwa charged with involuntary manslaughter; kama ni bahati mbaya tu unapata ticket hata mahakamani hufikishwi. Faini ya laki saba kwa mtu ambaye Serious Fraud Office ya Uingereza waligundua kuwa ana Swiss bank account ya $1000000 ni kama unamtania tu.

Yaani mnampa adhabu ya hivyo VIJICENT tuu??? Hakika nchi yetu imefika mahala pabaya. Je hii ndio sheria imechukua sura mpya kwa watu wa aina hii? Je alivyosema jirani mmoja hapo juu, ingekuwa mtanzania mwingine si angeambulia MIONGO kadhaa ndani ya JELA?
Jamani hii kesi, inatakiwa kujadiliwa na watanzania wote wenye nia ya kutufikisha pazuri sisi sote na hii nchi yetu tukufu ya Tanzania...

YOTE MMEYATAKA WENYEWE MNALALAMIKA SIKU YA KURA HAMPIGI NISIONA MBWA AKILALAMIKA HAPO...

Mi nampinga jamaa aliyesema eti hatujui sheria, kwani yeye ameua bila kukusudia, ameuwa kizembe na hakika justice ilikuwa ni kumfunga maisha, bia kujali kwamba yeye ni nani. Kuwapotezea maisha watu wawili we unafikiri mchezo... mungu atalipiza kisasi.. je ingekuwa sheria ya an eye to an eye, si angetakiwa kufaa. acheni kusema sheria sheria... huyo alitakiwa kifungo cha maisha..... ama kifooooooooooooooooooo