Mwanamuziki Mkongwe wa Mlimani Park Ochestra,Hassan Bichuka akitoa vionjo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo asubuhi katika ukumbi wa Flamingo wa Peacock Hotel.
Pichani kulia ni Meneja Masoko wa Precission Air Emilian Rwejuna, akisisitiza ushiriki wa0 katika tukio la kusheherekea usiku wa Mtanzania pale Karimjee Ground.
Peacock Hotel
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania.
Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu.
Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star. Kiiiingilio kimepangwa kuwa ni sh 40,000/=kwa kila mtu
Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi.
Washiriki wenzetu katika kuunga mkono U
siku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Damas Mfugale kwa namba 0789-280112
Asanteni












Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.
hiyo habari njema tutajikongoja but tunataka burudani na sio mc atuonyeshe ufundi wa kuongea kama yupo redioni
Post a Comment