Tuesday, November 30, 2010

kilimanjaro stars yaibanjua somalia 3-0 CECAFA Tusker Challenge Cup 2010.

Mie nikiwa na Injia wa Blog zote zenye nembo ya MK,Kamanda Christofa ambaye kwa sasa yupo Bongo pamoja na kamanda wa Mtaa kwa Mtaa, sote tulikuwepo uwanjani kuonyesha uzalendo kwa timu yetu ya Kilimanjaro Stars ambayo imeinyuka timu ya Somalia goli 3 kwa 0 katika michuano ya CECAFA Tusker Challenji Cup 2010.

Ilikuwa patashika uwanja wa taifa leo.
nyomi la watu ambapo leo na mpaka jumamosi wameruhusiwa kuingia bure.
Majeruhi wa Somalia akitolewa uwanjani.
Mchezaji wa Kilimanjaro Stars akiwa amelala chini baada ya kugongana vibaya na mchezaji wa timu ya Somalia.
Refa akiwaelekeza jambo wachezaji wa Somalia.
Mchezaji wa Kilimanjaro Stars akijaribu kumchomoka mchezaji wa timu ya Somalia
Umati wa watu kutoka kila pande ya jiji la Dar lilijitokeza leo jioni kuishangilia vilivyo timu ya Taifa ya Tanzania Kilimanjaro Stars,ambapo timu hiyo imefanya kweli leo na kuwaletea raha upya Watanzania kwa kuibanjua timu ya Taita ya Somalia magoli 3 kwa 0,kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge Cup 2010.

Goli la kwanza limefungwa na mshabuliaji kiungo wa timu ya Taifa anayecheza mpira wa kulipwa nchini Sweden Hery Joseph alpofunga goli kwa njia ya penati, goli la pili limefungwa na mchezaji John Boko na goli la tatu lilitingwa kimiani na mshambuliaji Mrisho Ngasa.

Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

Naona wakwere wamempata kibonde na kumkandamiza tatu bila, hongereni vijana mwendo huo uendelee pia kwa timu nyingine.

michuzi junia naamini wewe ni mjanja sana hapo mjini kuliko kaka ako. sasa vipi mimi niko ughaibuni lkn nasikia t-pain alipiga show babkubwa ndani ya dar weka picha basi najua utazipata au kama huna tueleze twende wapi tukazione. maana kaka yako yeye ni siasa tu