Monday, November 29, 2010

hali ya gurumo bado si shwari,ahamishiwa icu.

Galacha Mkongwe wa miondoko ya muziki wa dansi hapa nchini,Maalim Muhidin Gurumo ambaye wiki iliyopita alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar hali yake bado si nzuri.

Maalimu Gurumo ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa Dansi,Msondo Music .alifikishwa hospitalini hapo Alhmisi na kulazwa wodi ya Mwaisela namba 5 akisumbuliwa na mapafu kujaa maji.

Akizungumza jana jijini Dar,mmoja wa ndugu wa Mwanamuziki huyo alisema kuwa Gurumo baada ya hali yake kuwa mbaya ijumaa mchana alihamishiwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa matibabu zaidi.

Alisema Mwanamuziki huyo kwa sasa hawezi kuzungumza kutokana na hali kuwa si nzuri,ndugu huyo alisema anawaomba Wadau wa Muziki nchini,kujitokeza kumsaidia kwa hali na mali na kumuombea ili aweze kupona maradhi yanayomsumbua.Habari kwa hisani ya gazeti la Majira.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.