Futa kumbukumbu kabla ya kuiuza kompyuta
Unataka kuuza kompyuta yako na kununua mpya,lakini kwenye kompyuta yako kuna kumbukumbu nyingi za muhimu ambazo usingependa mtu mwingine yeyote azipate wala kuziona.Je utafanya nini?

Jinsi gani kompyuta inahifadhi kumbukumbu?
Wengi wetu wanaweza wakawa wameshaanza kujiuliza,inakuwaje sio salama wakati nimeshafuta kila kitu toka kwenye kompyuta? Je mtu ataweza vipi kuona mafaili ambayo tayari nimeshayafuta? Ukweli ni kuwa,kwa mujibu wa uhifadhi wa kumbukumbu kwenye kompyuta.Pindi unapofuta au kufanya format(kuweka mtambo endeshi(OS) mpya),sio kweli unayafuta moja kwa moja mafaili na kumbukumbu toka kwenye kompyuta yako.Kitu kinachofanyika ni kuwa unaondoa taswira yake kwenye uso wa mbele wa hard disk hivyo kukufanya wewe uone kama umeyafuta ila bado yanaendelea kuwepo kwenye disk yako.Na hii ndio maana kama kunatokea kesi,wataalam wa uchunguzi wa makosa ya kompyuta(Computer Forensic) huchukua kompyuta yako kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi.

Siku hizi kuna program nyingi sana ambazo zina uwezo wa kurudisha mafaili hata yale yaliyokuwepo kipindi ulipoinunua kompyuta kwa siku ya kwanza, mara nyingi jinsi gani unaweza kuyarudisha hayo mafaili hutegemea elimu ya mtu anayefanya hizo kazi ya kuyarudisha,kwani kazi ya kuyarudisha haya mafaili huwa ngumu kutegemeana na jinsi mafaili hayo yalivyofutwa.Mfano faili lililofutwa kwa kubonyeza "Delete" ni rahisi zaidi kulirudisha kuliko lile lililofutwa kwa kuformat kopyuta, vilevile huwa ngumu zaidi kama mtumiajai alifanya mgawanyo wa hard disk (partition) baada ya kuformat. Hivyo leo hii nitakuonehsha njia thabiti za kufuta kumbukumbu toka kwenye kompyuta unayotaka kuiuza ili kuhakikisha unakuwa salama zaidi.
Nitafutaje kumbukumbu moja kwa moja toka kwenye kompyuta ?


Kama unataka kujaribu mwenyewe,basi kompyuta inapowaka tu bonyeza "Delete",baada ya hapo fuata maelekezo na kuingia kwenye "Boot Sequence",iweke CD or DVD kuwa ya juu kabisa kabla ya Hard drive,hapo mambo yatakuwa sawia. 4.Fuata maelekezo utakayopewa na hiyo programu,mara nyingi huchukua masaa kadhaa hadi siku mpaka kufuta kila kitu kilichopo kwenye kompyuta yako.
Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto. Baada ya hapo basi kompyuta yako itakuwa mbichi kabisa na unaweza kuiuza bila utata wala hofu juu ya kumbukumbuku wala usalama wako.
Zaidi Bofya Hapa












Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment