Sunday, October 31, 2010

KALAle MAHALI PEMA PEPONI ELVIS MUSIBA

Lukwangule:Mguu ndio uliomuua Musiba
Elvis Musiba enzi za Uhai Wake.
----
Kwa taarifa zilizopatikana,zinaeleza kuwa marehemu Elvis Musiba alifariki katika hospitali ya TMJ leo saa nne asubuhi.Taarifa zinazidi kueleza kuwa Musiba alilazwa jana katika hospitali hiyo akisumbuliwa na mguu ambao ulifanyiwa operesheni hivi karibuni nchini India.

Mipango ya maziko inafanywa nyumbani kwake Mikocheni na wanafamilia wanajadiliana kuhusu mazishi na maziko ya mpendwa wao.

Mungu ailaze roho ya mahali pema peponi-AMIN.

Kuna Maoni 7 mpaka sasa.

aah jamani huyu baba kafariki, rest in peace musiba na poleni sana wana familia na marafiki katika kipindi hiki kigumu sana katika maisha yenu, Mungu awatie nguvu, jamani mie nakumbuka vitabu vyake vilikuwa na hadithi za kusismua ambapo humo ndani vilikuwa na mbabe willy gamba, njama, kikosi cha kisasi, kufa na kupona, kikomo ama kweli alijaaliwa kipaji cha hali ya juu,

poleni sana

Poleni wana familia Tanzania tumepoteza mtu muhimu sana.

mtunzi wa NJAMA na KIKOSI CHA KISASI. alinifanya kwa umri wangu mdogo enzi hizo nipende riwaya za kiswahili... wakati huo ulikua unaamini kabisa mtu anaeitwa WILLY GAMBA yupo. poleni sana dr zumbi na ndugu zako. bwana ametoa bwana ametwaa...jina la bwana libarikiwe

Alianza shujaa Ben R Mtobwa......sitakusahau na vitabu vyako vya WILLY GAMBA! Tutakukumbuka Musiba.

I.W.R...Aristablus umeondoka...tangulia baba njia yetu sote

Ohhh imeniuma sana aisee its like a dream to me,i lost my dady on july I can feel the pain from the family,R.I.P dady,many pole to my cousin Mohamed Murebere Musiba,ull make it hun,i understand he is gone while u needed him,inshaaaalah u gonna b ok.jus pray n knw that ur beloved dady is in peaceAmen.