MSAADA TUTANI
Nina msaada ninaotaka kusaidiwa na watanzania wenzangu hasa walio Tanzania japokuwa hata wanje ya Tanzania nao waweza changia. Mim nipo huku ughaibuni kwa mda mrefu kidogo ila kwa sasa nataka nirudi nyumbani na kuanzisha biashara zangu binafsi ambazo zitakuwa zinahusika na uingizaji wa bidhaa ndani ya Tanzania kutoka USA, Je ni aina gani ya bishara ninayoweza kufanya yenye manufaa kwangu na watanzania?, ambayo itahusu mambo makuu matatu MAVAZI, CHAKULA NA MALAZI
Nitashukuru kwa mawazo na michango yenu!!!!!












Kuna Maoni 5 mpaka sasa.
biashara ya fasta fasta itakayokulipa mdau ni kuuza pombe tu au lah bas lete unga-cocaine
Nikuambie ukweli Tanzania haina fomula, utaratibu wa nje ambapo unaweza ukaweka makadirio plus muda hapa Tz sahau.
Kama unataka kuwekeza, we njoo na kila aina ya bishara kutegemeana na mfuko wako. Usiseme aina fulani, we jaribu zote, halafu itakayojipa basi unaenda nayo.
Wewe vipi mbona sikuelewi, mbona tayari unajua aina za biashara unazotaka kufanya, si umetaja aina za biashara, nguo, chakula nk. Au ndio kusema hata kujieleza huwezi? unachotaka hapa ni market analysis kujua ni biashara gani italipa kati ya hizo au? rephrase your information please!
fungua gesti inalipa sana
Hakuna biashara halali, kila mfanyabiashara ni mwizi. Kama unaona unaweza kujiunga unakaribishwa. Kuna walipa kodi na wasiolipa hata sent lakini wote mnapigania soko moja. Kwa kuwa wewe ni mlla hoi na sio kama wenzetu wazungu, wao wanpewa tu kila kitu. Utasota kidogo kidogo wafanyakazi wezi, ndugu wezi, sasa hata hiyo biashara inabidi usitowe macho. Ukitowa tu jicho huna faida.
Post a Comment