Wednesday, September 29, 2010

vodacom miss tanzania 2010 akabidhiwa bendera ya taifa leo jijini dar,kutimka kesho kwenda china

Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel akiwa amepozi kwa picha huku akiwa ameishikilia bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha katika mashindano ya Miss World yatakayofanyika hapo baadae mwaka huu nchini China.
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi kinyago Miss Tanzania 2010 Geneviev Emmanuel kama sehemu ya kwenda kuitangaza nchi yetu,Mlimbwende huyo anatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China ambako mashindano hayo yatafanyika.
Miss Tanzania 2009 na Miss Tanzania 2010.
Kushoto ni Mama mzazi wa Miss Tanzania Genevieve wakiwa na aliyekuwa mgeni rasmi Mkuu wa Sekta Binafsi nchini Ester Mkwizu na baba yake Emmanuel Mpangala katika picha ya pamoja na Miss Tanzania 2010.
Kutoka kushoto ni mlezi wa Miss Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji nchini (TIC),Emmanuel Ole Naiko,Mkuu wa Sekta Binafsi nchini Bi. Ester Mkwizu, Genevieve,
Mkurugenzi wa Utamaduni na Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Prof Helmas Mwansoko pamoja na Mkurugenzi wa Udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.
Pichani kati ni mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania,Martina Nkurlu na wadau wengine wakifuatilia kwa makini hafla hiyo ya kukabidhiwa bendera ya Taifa,Vodacom Miss Tanzania 2010 Geneviev mapema leo asubuhi jijini Dar.
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali akiwemi Miss Tanzania 2009,aliyemaliza muda wake Miriam Gerald pia alikuwepo kumsindikiza mlimbwende mwenzake.
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akizungumza kwenye hafla fupi ya kumkabidhi bendera Miss Tanzania 2010 kwenye viwanja vya TIC mapema leo asubuhi jijini Dar.

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

you deserve to be miss world
haki ya mungu unakwenda kushinda
you have all the criteria .you are the champion!
agu