Tuesday, September 28, 2010

dr gharib bilal atua mbeya,aanza kampeni zake mjini humo leo.

Mgombea Mwenza wa urais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Jeras Fungo, ambaye ni mlemavu wa miguu Mkazi wa Kijiji cha Ihai, Kata mpya ya Ihai, aliyefika katika mkutano wa kampeni kijiji cha Chimala, baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika katika eneo la Stendi ya zamani ya Mabasi Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya leo.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilala, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbalali, Modestus Kilufi, wakati alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni kwenye eneo la Stendi ya zamani ya Mabasi Wilaya ya MbalaIali leo.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa CCM wa Kijiji cha Chimala Isitu, wakati alipowasili kwenye eneo la Stendi ya zamani ya mabasi ya Chimala, Wilaya ya Mbalali Mkoa wa Mbeya kufanya mkutano wa kampeni leo.
Wananchi wa Kijiji cha Chimala Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya, wamsikiliza Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Chimala Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya, wakishangilia wakati Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.