Salama kiongozi?
Hiyo picha ni jana majira ya saa kumi na moja jioni pale mlimani city mshkaji wangu kapigwa laptop kwa style ya kuvunjiwa kioo cha nyuma, alishuka kama dakika kumi tu kwenda kwenye ATM ya Exim bank na laptop akaificha chini ya kiti cha gari ile kurudi ndio akakuta ameshapigwa laptop na alivyowaeleza askari wa pale wakamjibu wao hawahusiki na issue za wizi sasa tukashindwa kuelewa kama hawahusiki na masuala ya wizi wako pale kufanya nini!!!!
Tukaambiwa na Taxi drivers pale kuwa last week alikamatwa mwizi ameiba laptop kwenye gari akapewa kisago askari wale wale wakamsaidia asiendelee kupigwa halafu akaachiwa na hakupelekwa hata polisi. TUTAFIKA???
Tukaambiwa na Taxi drivers pale kuwa last week alikamatwa mwizi ameiba laptop kwenye gari akapewa kisago askari wale wale wakamsaidia asiendelee kupigwa halafu akaachiwa na hakupelekwa hata polisi. TUTAFIKA???












Kuna Maoni 5 mpaka sasa.
mnakosea sana wabongo. Mtu akiibiwwa mnatakiwa mara moja mumkate mlizi mmoja na kumpa kisago na ikibidi mumuachie alama ya maisha ila msimtoe roho. Kama mnaogopa njooni tarime mchukuwe maujuzi. Kama wao wanashindwa kulinda mali za wateja wanaowapa kula then muzilinde wenyewe kwakuwapa kisago. Kalimakenge alipokataa kwenda shule hatua kadhaa zilichukuliwa na akaenda shule . Lets put this issue to rest now
Pole sana kwa kuibiwa laptop. Ila nadhani imesharipotiwa sana kuhusu wizi wa aina hii hasa hapo mlimani city.
Nitaendelea kumpa pole sana muathirika kama hakuwa taarifa kabisa kama hapo mlimani city kuna wizi wa namna hiyo vinginevyo naomba nimlaumu yeye mwenyewe muathirika.
Ilibidi awe na tahadhari kwa sababu ameingia eneo la wizi. Haikumbidi yeye kuacha laptop kwenye gari yake kabisa hata kama anashuka kwa dakika moja tu. kwa kifupi hautakiwi kuacha vitu vya thamani kwenye gari hasa ukiwa maeneo yenye wizi.
Unajua itailaumu sheria au watu watendi wajibu wao lakini wewe ndiye anayeathirika direct na tukio ni bora kuwa taadhari kuliko kuamini watendaji wasiotenda wajibu wao.
Pole sana once again na chukua tahadhari next time.
Vitu kama hivyo laptops. cameras hazipaswi kuwekwa sehemu za wazi kwani hapo ndo unawavutia wezi. kama unatoka kwenye gari kwanini usiweke kwenye buti la nyuma ambalo sio rahisi kwa mtu kupata access ya haraka? Tunawaendekeza wezi wenyewe, bongo njaa ni kali babu watu wanatafuta pesa kwa nguvu zote tuwe makini.
Uliyesema buti la gari,labda wasikuone kabisa wakati unaiweka,vinginevyo bado ni kazi bure.
ameshasema aliificha chini ya kiti.. tatizo ni uongozi wa mlimani city ni aibu sehemu kama hiyo kuwa na wizi. sasa inamaana kila mahali ukishuka uwe umebeba laptop hii ndio itarahisisha zaidi kuiba na pia wanaweza wakakupiga kisu ni bora uiache kwenye gari.
Post a Comment