Tuesday, August 31, 2010
RAIS wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, akifungua mkutano wa Majaji wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi katika ukanda huo na uhalifu wa kimataifa,leo katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Augustino Ramadhani. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Washiriki wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa unaendelea nchini Tanzania wakimsikiliza Rais Amani Abeid Karume wakati wa sherehe fupi za ufunguzi uliofanyika katika Hotel ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment