Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Mauritius Karl Auguste Offmann (kushoto) akisoma maazimio ya mkutano wa marais wastaafu wa Afrika juu ya maboresho ya ardhi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam . Katikati ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Msumbiji Luisa Diogo na kulia ni Mkurugenzi wa kuhifadhi Kumbukumbu za Marais Wastaafu wa Afrika Balozi Charles Stith.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa African Forum Dr. John Tesha mara baada ya kumaliza mkutano wa marais wastaafu na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo uliokuwa unaelezea mikakati ya maboresho ya ardhi barani Afrika.
Rais Mstaafu wa Zambia Dr Keneth Kaunda katikati akisalimiana naWaziri Mkuu mstaafu wa Mozambique Luisa Diogo kuliani Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Mauritius Karl Auguste Offmann.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa (kushoto) akitoa ufafaunuzi leo jijini Dar es salaam kwa wanahabari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Marais wastaafu wa Afrika uliokuwa unajadili juu ya maboresho katika sekta ya ardhi barani Afrika. Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.












Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.
kati ya MARAIS walio wahi kuiongoz a TANZANIA Benjamin William Mkapa nilimkubali mnooo.
Post a Comment