Tuesday, August 17, 2010

masikini unamuua mwenzio kama nyoka.! kuna fukuto gani ndani ya jamii yetu tunayoishi.?!

Kutona hasira za watu hao walioamua kujichukulia sheria mkononi,sidhani kama alipona kwani baadaye walitokea mgambo wa jiji na kumuokoa, Wakati wakielekea katika kituo cha Polisi cha Karume Kibaka huyo alianguka na kupoteza fahamu kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi kichwani.
Mmoja wa wananchi mwenye hasira kali akimponda na tofari Kibaka ambaye jina lake halikujulikana mara moja baada ya kudaiwa kumkwapua abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari akisafiri kuelekea Mwenge akiwa ametokea Tandika.Kibaka huyo inadaiwa alimkwapua simu abiria huyo na kukimbilia katika eneo la makaburi yaliyopo Karume na ndipo lilipoibuka kundi la Watu na kuanza kumfukuza na hatimaye kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshushia kibano cha nguvu kama uonavyo pichani.Blog ya Jiachie inalaani na itazidi kulaani matukio kama haya,ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kupoteza uhai wa wenzao kirahisi hivi,ilhali sheria zipo.Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania.

Kuna Maoni 14 mpaka sasa.

Hii inatokana na ukatili alionao mtu, kuna watu wengine hatuwezi hata kuchinja kuku sembuse kuua mtu

INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJIUUN, SASA ONA BADALA YA KUKATWA MKONO ANAUWAWA, SHERIA ZA KIDUNIA TAABU SANA

HAKIKA DUNIA IMEKARIBIA MWISHO. HAIWEZEKANI MTU AKOSE HATA CHEMBE YA HURUMA KATIKA ROHO NJEMA ALIYOUMBIWA NA MUNGU. JE PICHA KAMA HII YA HUYU KAKA ALIYEINUA TOFALI HAIWEZI KUTUMIKA KUMFUNGULIA MASHTAKA? JAMANI WANASHERIA SAIDIENI KATIKA HAYA. HUYU KAKA ANAONEKA SI MKRISTO KABISA KWANI HURUMA ANGEKUWA NAYO. PIA SI MWISLAMU KWANI KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU ROHO INGEMSUTA. HAKIKA HUYU HANA DINI KABISA. KWANI HATA DINI YA ASILI HAIKUBALI. PATRIQ

Mungu wanguu!! Duniani ubinadamu unazidi kutoweka kidogokidogo. Yaani huyo jibaba alivyobeba jiwe huwezi kuamin anapiga binadamu!

Na unaweza ukakuta uy aienyanyua jiwe yupo ndani ya swaumu,kwa kweli matendo ya binaadamu yanasikitisha mno.

WaBongo sote tu wendawazimu!!! Kama tuna uchungu na hasira za kuchukia vibaka na tuna akili timamu mbona hatuwapondi MAFISADI wanaosababisha ugumu wa maisha kwa jamii nzima - na hapa simaanishi kuwaponda kwa matofali bali kwa kutumia haki yetu halali ya KURA!!! Ni sisi juzi tumewapigia kura za maoni za kishindo watu kama mzee Pesambili na mzee wa Vijisenti (ambao sio ubishi -weka kando mchakato wa kimahakama - walishiriki kuitafuna nchi wakati wako madarakani). Ninasema watanzania wote - mafisadi na wafisadiwa - tumekuwa vichaa. PERIOD.

jamani hawa wanaotuibia simu na vipochi tunawauwa mbona mijambazi inayovunja nyumba na kuuwa watu hatuwapi hiyo adhabu? then na mafisadi wanaojichotea mapesa ya wananchi bureeeee mnawafanyaje???acheni hizo. mi nitafurahi nione jambazi lililovunja/kuvamia mahali na kuathiri maisha ya wengine nalo linauwawa kama huyu kijana ambaye umaskini ndo unaomfanya haangaike huku na kule ajitafutie japo mlo wa siku....

@mzee wa Bunju, mimi nimeshangazwa mtu kupinga kuuwawa kwa kibaka lakini angekatwa mkono, nashukuru Tanzania hatuna sharia law, la sidhani kama tutakuja kuwa na sharia law. Two wrongs dont make it right. Jamani, kuna jela, ukishamkata mtu mkono ndo itamsaidia nini, zaidi ya kumrudisha nyuma.

Huyo aliye kwenye picha akitupa tofali, angekamatwa kwani tayari kuna ushahidi wa yeyey pichani. Nadhani imefika wakati wa kukamata baadhi ya watu wanaofanya vitendo hivi vya ukatili. Watu kadhaa wakishatiwa nguvuma, mimi naamini wananchi wendawazimu kama hawa watatulia

PICHA KAMA HIZI WAONYWESWE HAO VIONGOZI ILI WAONE UFISADI WAO UNA TIA HASARA KWA JAMII NA KUUWA JAMII. HII YOTE NI UMASIKINI NA SHIDA. LAKINI AKILI IKO WAPI KAMA WAO NI FUNDI WA KUADHIBU WATU MBONA MAFISADI WANAWAPIGIA KURA? TANZANIA TANZANIA?

Hongera Michuzijr kwa kulivalia bango hii issue,hii tabia imezidi kwenye jamii yetu, najiuliza huyu njemba mwenye kitofali ni yeye aliyeibiwa? inabidi huyu njemba atafutwe na apelekwe mahakamani na kufunguliwa shitaka la kushiriki katika mauwaji ya kukusudia na adhabu yake afungwe maisha, bila kuwasweka ndani watu dizaini hii unyama kama huu utazidi kuendelea.

wakati nikiwa high school shule moja maeneo ya upanga inastart na herufi S mwaka 2006 kama ckosei kuna mwanafunzi mmoja ndo alikuwa amemaliza form six kwa bahati mbaya kuna siku jioni akiwa anasubiria basi maeneo ya ubungo akaitiwa mwizi from nowhere then watu wakampiga akaja kufariki akiwa anapelekwa hospital mwananyamala , he was bright,waiting to join University but ndoto zote zikapotea ..naandika this comment machozi yananitoka,ila ukweli is ni wengi hawana hatia tunawapoteza hivi na uhai wa mtu co thamani ya cmu..
Mungu Ibariki Tanzania

Mosi, wanaouliwa ni walalahoi...mbona watoto wa wakubwa na wakubwa wenyewe wanaiba lakini hatuoni hayo yakitokea?

Pili, kama mtoto wa mkubwa akiuliwa hivyo, Polisi itakuja juu kasi moja! yale yale ya Musa na Firauni...hadi kifo cha mzaliwa wa kwanza!

Tatu, haya mauaji, kama yalivyo ya maalbino, ni kaama yanapewa baraka na Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Usalama wa wananchi! Kwa nini hao mawaziri hawajajuzulu mpaka sasa. watakufa wangapi ndipo mawaziri wawajibike?

Jamani binadamu hatufanyiani hivyo hatumwadhibu binadamu namna hiyo.Kuna vyombo vya sheria mngemchapa hata viboko matakoni ingekuwa adhabu tosha au makofi na kuwachia vyombo vya sheria kutoa adhabu.Na hivi vyombo vya sheria vinahitaji kutoa adhabu kali kwa hawa vibaka ambao wanaturudisha nyuma sisi walala hoi.Kwa nini hawaendi sehemu za wanaokaa matajiri na kufanya hivi vitendo vya wizi.

Jamani, utu mbona umetukimbia??

Naomba msaada kuwasilisha ujumbe ufuatao!

http://vijana.fm/2010/08/20/huu-ni-ufedhuli/