Tuesday, August 31, 2010

mama salma kikwete ziarani mkoani singida leo

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mama Salma Kikwete akimtambulisha mgombea Ubunge kupitia CCM Kondoa Mashariki Mkoa wa Singida,Bw.John Lwaji leo mjini humo.Mama Salma yupo mkoani Singida kuwahamasisha wanachama wa UWT kuhusu uchaguzi utakaofanyika hivi karibini mwaka huu.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa amewabeba watoto mapacha Agost 31,20101 alipowasili katika kijiji cha Kinya Mshindi Mkoani Singida kuanza ziara yake ya kuwahamasisha wanawake kuhusu uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akikagua gwaride leo mara alipowasili Itigi Mkoani Singida katika shughuli zake za kuwahamasisha wanawake wa UWT kuhusu Uchaguzi Mkuu mwaka huu.Picha kwa hisani ya Mwanakombo Juma-MAELEZO.

Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

Samahani kaka michuzi;
Hivi Kondoa siku hizi ipo Mkoani Singida kama inavyoelezwa katika taarifa ya mama Salma Kiwete kwamba anamtambulisha mgombea wa Kondoa Mashariki mkoani Singida? Tafadhali tunaomba ufafanuzi. Nijuavyo mimi Kondoa ipo mkoani Dodoma.
Nawasilisha.

WAMA na CCM ni wamoja au Jakaya na Salma? ivi TAMWA, TAWLA, HAKIELIMU au wengineo wakiamua kuwapigia kampeni wagombea wengine tutasemaje? Mama Salma anatumia gharama za CCM au serikali kumpigia kampeni mumewe?