
Pichani ni mgombea urais kwa Chama cha NNCR Mageuzi, Hashim Rungwe akionyesha ilani ya uchaguzi ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho leo jijini Dar.
CHAMA cha NCCR Mageuzi leo kimezindua ilani yake ya Uchaguzi huku kikitaja mambo 12 ambayo chama hicho kitaelekeza nguvu iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi.Wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa chama hicho taifa James Mbatia alisema chama chake kitazindua kampeni zake kitaifa Septemba 11 baada ya mfungo wa ramadhani ili kutowakwaza Waislam ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu.“Ajenda yetu kuu itakuwa ni katiba, tumeainisha mambo yatakayokuwemo kwenye katiba hiyo, hili ndilo nataka wagombea wetu mlizungumzie kwa kina,” alisema Mbatia.












Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment