Saturday, July 31, 2010

Watatu watuhumiwa na shambulio la Uganda

Watuhumiwa wa shambulio la Uganda

Wakenya watatu wameshtakiwa kwa mauaji ya watu 76 waliouliwa wakati mabomu yalipolipuka walipokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia kupitia televisheni mjini Kampala, Uganda.

Hussein Hassan Agad, mwenye umri wa miaka 27, Mohamed Adan Abdow, 25 na Idris Magondu, 42, nao walishtakiwa kwa ugaidi na mashtaka 10 ya jaribio la mauaji.

Bado hawajajitetea na wataendelea kubaki kizuizini mpaka wafikishwe tena mahakamani Agosti 27.Al-Shabab, kundi la wapiganaji la kisomali, lilisema lilihusika na mashambulio hayo.

Majeshi ya kutunza amani ya Uganda yapo Somalia, kusaidia serikali dhaifu, inayoungwa mkono na umoja wa mataifa dhidi ya al-Shabab, yenye uhusiano na al-Qaeda.

Umoja wa Afrika wiki hii iliahidi kuongeza majeshi ya kutunza amani Somalia kufikia majeshi 4,000, baada ya mkutano uliofanyika Kampala, mji uliokumbwa na mashambulio.

Mpaka sasa ni Uganda na Burundi tu ndizo zilizopeleka majeshi yake katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na al-Shabab ilitishia kushambulia nchi zote mbili.Chanzo BBC.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.