Saturday, July 31, 2010

wasanii wa fiesta jipanguse 2010,kupitia kampeni ya zinduka watoa msaada wa vyandarua hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza.

Shoto ni B Dozen,Young D,Rebeca kutoka kituo cha THT,Mwasiti pamoja na waja wazito katika picha ya pamoja jioni hii,mara baada ya kuwakabidhi Vyandarua vya msaada kupitia mpango mzima wa kampeni ya kupambana na malaria nchini wa ZINDUKA.
Mabalozi wa Malaria nchini wakiwa wamepozi picha ya pamoja na waja wazito jioni hii mara baada ya kuwakabidhi Vyandarua vya msaada kupitia mpango mzima wa kampeni ya kupambana na malaria nchini wa ZINDUKA.
Mtangazaji wa Clouds FM B dozen kwa niaba ya wasanii wenzake akizungumza machache mbele ya Wazazi ndani ya wodi ya wazazi ndani ya hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure mara baada ya kuwakabidhi vyandarua leo jioni ,yote hiyo ikiwa ni kwenye mpango mzima wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria iliyozinduliwa hivi karibuni ya ZINDUKA.
Mtangazaji wa Clouds FM Hamis Mand a.k.a B Dozen akiwakabidhi Vyandarua Muuguzi mkuu (kushoto) Bi.Eva Mudayi pamoja na afisa muuguzi wa wodi hiyo Bi Adelina jioni hii,yote hiyo ikiwa ni kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kupitia mpango wa ZINDUKA.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao wapo kwenye ziara ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,ambao pia ni mabalozi wa Malaria hapa nchini,Mwasiti pamoja na Chege wakiwakabidhi Vyandarua Muuguzi mkuu (kushoto) Bi.Eva Mudayi pamoja na afisa muuguzi wa wodi hiyo Bi Adelina jioni hii,yote hiyo ikiwa ni kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kupitia mpango wa ZINDUKA.

Pichani kulia ni Muuguzi mkuu Bi.Eva Mudayi akitoa muongozo wa awali kwa baadhi ya wasanii nje ya Wodi ya Wazazi kabla ya kukabidhi msaada wa Vyandarua jioni ya leo ndani ya hospitali ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure.
Pichani kulia ni Muuguzi mkuu Bi.Eva Mudayi akiwaongoza baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya kwenda kukabidhi msaada wa vyandarua kwenye wodi ya Wazazi jioni hii.Mbele kabisa ni wasanii Godzilla na Chege wakiwa wamebeba vyandarua.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.