
Vumi akiwa amepozi na rafiki yake Godliva

Msanii Vumi akielezea ujio wake mpya katika anga ya muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva.Vumi anasema hivi sasa yuko kwenye harakati za kuikamilisha albamu yake itakayokuwa na jumla ya nyimbo nane,anazitaja baadhi ambazo tayari zinafanya vyema kwenye vituo mbalimbali vya redio kama vile Nenda,Utanikumbuka,tatizo umaskini pamoja na singali yake mpya aliyoitambulisha leo ndani ya kipindi cha Leo Tena iitwayo That Day.Vumi ambaye pia ni moja ya wasanii waliopikwa vyema na kituo cha THT kwa sasa yupo kwenye bendi ya Kimondo Sound a.k.a Kibajaji akijiendeleza zaidi.

Mtangazaji mwalikwa kwenye kipindi cha Leo Tena (kwenye chachandu la leo) aitwaye Husna B akitokea redio ya Coconut FM 88.2 a.k.a Mambo ya zenji,Zanzibar

Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Dina Marious kupitia redio ya Clouds FM 88.4 akifanya mahojiano mafupi na msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye vumi ambaye kwa sasa yupo ndani ya bendi ya muziki wa dansii ya Kimondo Sound a.k.a Wanakibajaji ikiongozwa na Richard Mangustino aliyewahi kuwika miaka ya nyuma kwenye bendi kadhaa ikiwemo ya Diamond Sound enzi zilee za Ikibonda Nkoi.
Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.
MICHUZI huyo rafiki wa vumi kaolewa?nipe namba yake nataka nipeleke posa ikiwezekana uwe mshenga wangu,sura nzur sana na tabasam mwanana sijui umbile lake
Post a Comment