Wednesday, June 30, 2010

soko la pamoja kuanza kesho

WAZIRI wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC),Dkt. Diodorus Kamala amewahakikishia watanzania kuondoa hofu ya kunyang'anywa ardhi yao kutokana na Tanzania kujiunga na Jumuiya hiyo.

Dkt.Kamala alisema kuwa ardhi ya Tanzania itabaki kuwa mali ya watanzania na haitaguswa na raia kutoka nje ya nchi kwa kisingizio soko la pamoja.

Hayo aliyasema Dar es Salaam juzi wakati akitoa ya utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuongeza kuwa Tanzania inatazamiwa kunufaika na soko la watu milioni 130 kwa kuuza bidhaa zitokanazo na kilimo katika jumuiya baada ya kuboresha mazingira ya uzalishaji.

Dkt. Kamala alisema kuwa Tanzania ndio nchi pekee inayotarajiwa kutoa chakula kwa nchi za EAC kutokana na kuwa na ardhi nzuri ya mazao hivyo hatuna budi kutumia nafasi hiyo kuimarisha uchumi na maendeleo kwa ujumla.

"Jumuiya ya Afrika Mashariki imejaliwa kuwa na vyanzo vya maji, nishati, ardhi na hata mbolea hivyo kupitia jitihada za kikanda;Sekretarieti ya EAC imejipanga kuibua mpango wa kupatikana kwa utaratibu wa kuvuna mbolea itakayosaidia utekelezaji wa mkakati wa maendeleo ya kilimo,"alisema. Habari zaidi Bofya Hapa

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.