Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva (Hip Hop),Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II ameachiwa huru kwa dhamana
Mr II alikamatwa mapema leo asubuhi
katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati wa kikao cha PRESS TALK akiwa anaongelea masuala ya muziki,Mr II alikamatwa mapema leo asubuhi
Akizungumza kwa njia ya simu Mr II amesema kuwa alikamatwa na polisi baada ya mmoja wa viongozi wa redio flani ya hapa jijini kumshitaki kuwa yeye (MR II) anamtishia maisha na pia kwenye wimbo wake wa AUNT VIRUS.
Mr II amesema baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo cha polisi cha upelelezi kwa ajili ya mahojiano,lakini baada ya muda Mr II aliachiwa huru kwa kujidhamini yeye mwenyewe.Aidha Msanii huyo ametakiwa kuripoti tena kesho kutwa katika ofisi hizo kwa mahojiano zaidi.













Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.
Mimi nina swali tu? Huu ndio ushindi wa kishindo tunaoambiwa kwenye tafiti mbalimbali kuwa utapatikana kwenye uchaguzi mkuu?
Ni swali tu.
Post a Comment