
Paul James na shaffih Dauda wakijadiliana


Burudani ni Jadi yao na inazidi kuendelea.! Wana wa Clouds Media Group kupitia Clouds TV wanakuletea burudani ya pekee ya Soka la Ulimwengu,katika levo ya juu kabisa,Mchakato huo wa kuwaletea mpango mzima wa Kandanda unaanza rasmi hapo kesho,yaani Juni 1 kupitia Luninga yao ya Clouds Tv,kila siku saa 3:30 usiku.Watakuwa wanakuletea uchambuzi wa kina ukiambatana na matukio halisi kwenye picha za ubora wa hali ya juu kabisa.Wakiwa katika kipindi chao kiitwacho The road to South Africa 2010 kitakuwa kikichambuliwa na Watangazaji mahiri na wenye vipaji akiwemo Paul James (PJ) pamoja na Shaffih Dauda (Mzee wa number 10). Pichani ni Watangazaji Paul James pamoja na Shaffih Dauda wakiwa ndani ya Studio za Clouds TV tayari kwa kuwaletea mambo mazuri ya kiburudani katika anga ya kisoka zaidi.
Kuna Maoni 6 mpaka sasa.
Kaka ilipotea hewani Cloudz TV,Imesharudi manake mhh
ok mambo muswano tanawatakia kila rakheri
VP MAMBO YA ONLINE YANAPATIKANA, KAMA TUNAVYOISIKIA CLOUDS FM KUPITIA MTANDAO WA......??
.....????
Jina la kipindi kwa kiinglish, uchambuzi kwa kimatumbi. hapo tu ndo ninapowakoma wabongo.
Huo mpira bora mngeweka mpira utakaotumika kwenye World Cup mwaka huu na sio wa 2006, haileti picha.
Post a Comment