Thursday, April 29, 2010

FFU! wa The Ngoma Africa Band 8.May 2010 ndani ya Bayern,Munchen

FFU wa Ngoma Africa band,Kutumbuiza katika sherehe za washabiki wa

Wold Cup 2010,huko Munchen aka Bayern,Munich,
Onyesho litafanyika eneo la Pfarrheim.St.Joseph,Joseph Platz 1.München

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" aka FFU,
au "wazee wa kukaanga mbuyu",yenye maskani yake uko ujrumani.Kikosi iko
kinatarajiwa kuwasili mjini Munich aka Muchen siku ya jumamosi ya 8 May 2010
kwa ajili ya kufanya onesho la shamra shamra ya Sherehe za kombe la kandanda la Dunia,ambalo kwa mara ya kwanza litafanyikia nchini Afrika Kusini aka Azania.

Shamra shamra hizo zimeandaliwa na jumuiya za wafrika na mashirika yasio ya kiserekali pamoja na Chama cha urafiki kati ya Tanzania na Ujerumani.Sherehe hizo inasemekana zitaudhuriwa na mabalozi wa nchi mbali mbali.

Wakazi na washabiki wa mji wa Munich,ambako ndipo makao makuu ya klabu ya
mashuhuri ya kandanda "Bayern,Munich" ,watapata bahati ya kusakata mziki wa
dansi kutoka kwa mzimu wa dansi "The Ngoma Africa Band".

Bendi ambayo inasifa za tabia ya kuperekana mchaka mchaka na washabiki wake,kwa kutumia mdundo wake wa dansi.http://www.myspace.com/thengomaafrica
Bendi hiyo ni juzi tu waliachia singo CD yao iliyobeba jina la "Jakaya Kikwete 2010"
na kufanikiwa kuteka washabiki lukuki katika youtube!

Karandinga la FFU wa Ngoma Africa band litahakikisha limewasili mapema mjini Munich aka Munchen ,uku likiwa na mabox ya kutosha yaliojaa virungu vya mziki,
wakazi wa Bayern,Munich kaeni tayari tayari kwa kusakata magoma mpaka hasubui.

kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Temu ambaye ndie mratibu wa tamasha hilo kwa
simu +49(0)179 6661748 begin_of_the_skype_highlighting +49(0)179 6661748 end_of_the_skype_highlighting karibuni nyote

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

ffu aka watoto wa mbwa,kubwaka ndani ya munich,poa kabisa