Wednesday, April 28, 2010

ajali mbaya usiku wa manane

kitambulisho cha marehemu
Polisi walifika sehemu ya tukio la ajali na kuuchukua mwili wa marehemu kwa taratibu nyingine mbalimbali.

Toyota Hilux yenye namba za usajili T 826 ADU,iliokuwa ikiendeshwa na Marehemu aliyetambulika kwa jina la Frank Kagangule kwa mujibu wa vitambulisho vyake.
Toyota Hilux ilipovaana uso kwa uso na Lori,baada ya dereva wa Lori kupoteza mwelekeo na kuhama barabara na kukutana uso kwa uso na hiyo Toyota Hilux,Ajali hiyo imetokea maeneo ya Supa-Mbezi Beach jijini Dar mnamo majira ya saa sita usiku kuamkia leo.
Yaani dah,halafu Lori lenyewe limechoka ile mbaya halafu limebebeshwa Kontena lenye mzigo
Baadhi ya wasamalia wema wakijaribu kuutoa mwili wa marehemu
Marehemu akiwa amebanwa vibaya na gari kwenye ajali hiyo mbaya kabisa
Msamalia mwema akijaribu kuuvunja mlango ili kumtoa marehemu
Baadhi ya watu waliofika kwenye ajali hiyo iliotokea maeneo ya Supa-Mbezi Beach jijini Dar mnamo majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo wakijaribu kufanya jitihada za kumtoa marehemu.Katika ajali hiyo mtu mmoja wa gari ndogo alipoteza maisha hapo hapo na waliokuwa ndani ya Lori pamoja na dereva walikimbia eneo la tukio baada ya ajali kutokea.
Lori hilo likuwa limebeba kontena lenye mzigo ndani,dereva baada ya kuona linamshinda akahama upande mwingine na kukumbana na hiyo hilux uso kwa uso

Kuna Maoni 8 mpaka sasa.

MASKINI FRANK.
NATOA POLE KWA WANANDUGU NA FAMILIA YA FRANK. HAKIKA HII NI MIPANGO AMBAYO MUNGU AMEPENDA IWE HIVO. JAMANI POLENI WADAU TOKA DODDOMA TUNAWAPA POLE.
HATA HIVO KWA MWONEKANO, GARI HILO LINAONEKANA NI CHAKAVU NA HALIONESHI KUFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU KATIKA BARABARA ZETU. CHA KUJIULIZA HIVI USIKU HUO POLISI WA DORIA HAWAFANIKIWA KUKUTANA NALO? NAAMINI JESHI LA POLISI HUWA NA DORIA KWENYE HAI WAY - SASA HAIWAGUSI CHOCHOTE? YAWEZEKANA KUNA UOZO MWINGI UNAOFANYWA UCKU NA WADAU WA UFISADI. NAAMINI KAMA INGEKUWA NI MCHANA HAKIKA GARI HILO LINGESHUGHULIKA IPASAVYO NA VIJANA WA IGP MWEMA. SASA JESHI LIJIPANGE VEMA KUDHIBITI HALI HII INAYOKATISHA MAISHA YA RAIA WEMA KAMA KAKA FRANK. REALLY POLISI ISEME KITU KATIKA HILI. ASANTE. PATRIQ JINGU - DODOMA.


POLENI SANA WAFIWA. NAKUMBUKA NILISHAWAHI COMMENT KWA MICHUZI KUWA KUNA MAROLI MENGI SANA MABOVU USIKU BARABARA YA BAGAMOYO. MAROLI HAYO HUWA YANABEBA SIMENTI TOKA KIWANDA CHA WAZO NI MAKUKUU KUU TENA MENGINE HAYANA TAA KABISA. MIMI NIMESHAWAHI PISHANA NAYO MARA NYINGI SANA, UNASHTUKIA TUU HILI HAPA UNAPISHANA NALO TENA LIKIWA NA TELA. HII NI HATARI NA WAO WANAJUA KABISA KUWA HAWATAKATWA KWA KUWA USIKU POLISI INAKUWA IMELALA! MAISHA YA WATU YANAPOTEA KILA SIKU SABABU YA HAYO MAROLI NA POLISI IKO KIMYA TUU. NADHANI WA KULAUMIWA NI KIWANDA CHA WAZO PIA. WAO WANAJUA KABISA MAROLI MABOVU YAKUJA KIWANDANI KWAO KUBEBA SIMENTI WAO WANAPAKIA TUU.KWA NINI WALE JAMAA KULE KIWANDANI WASIWASILIANE NA POLISI WAJE KUYAKAGUA HAYO MAROLI KAMA YANAFAA KUBEBA MIZIGO MIZITO NA YA HATARI KAMA SIMENTI? AU KWA NINI POLISI WASIWE NA KITUO CHAO CHA KUKAGUA HAYO MAGARI PALE KARIBU NA KIWANDANI. KWA KWELI POLISI WANASTAHILI LAWAMA NA UTASHANGAA HAKUTAKUWA NA UCHUNGUZI WA AJALI KAMA HIYO HATA KAMA ROLI LINAONEKANA KABISA KUWA NI BOVU.
NCHI YETU IKO NYUMA SNA KATIKA KUJALI USALAMA WA RAIA.

KWA WENZETU DEREVA ANASHAURIWA KAMA GARI LIKIMSHINDA ATAFUTE KUGONGA KITU AMBACHO HAKITEMBEI TENA IKIWEZEKANA AKIGONGE KWA PEMBENI ILI KUPUNGUZA DHORUBA SIJUI KAMA MADEREVA WETU WANA MAFUNZO KAMA HAYO. INAONEKANA DEREVA KAMUA KULIPELEKA GARI UPANDE WA PILI WA BARABARA INGAWA KIUSALAMA ALITAKIWA APELEKE NJE YA BARABARA UPANDE WAKE YEYE.. HALAFU SAA NANE HUWA HAKUNA MAGARI MENGI SIJUI ILIKUWAJE?

NAWAPA POLE SANA FAMILIA YA MAREHEMU,NAWATAKIA AMANI UMOJA NA UPENDO KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAJONZI..IMENIUMA SANA ITZ SAD NDUGU ZETU WANAPOTEZA MAISHA NA AJARI ZA MOTORWAYZ IN EVERY SINGLE DAY KWA UZEMBE WA WAHUSIKA TRAFFIC..DIZ IZ FKN JOCKING BORA KIFUTWE 2 KITENGO CHA USALAMA BARABARANI NAYAJUA VIZURI SANA MAROLI YA CEMENT,MCHANGA NA YA MATOFALI MBEZI BEACH YANAFANYA KAZI DAY&NIGHT NENDA GOIG UTAYAKUTA...UOZO MTUPU KWA WAHUSIKA ANYW WA TZ TUBADILIKE TUTAKWISHA KUKAA KIMYA. R.I.P FRANK

Duh!, Jeshi la polisi liwe na kikosi maalum cha "night traffic"

Unajua magari mengi yasiyostahili kuwa barabarani yanafanya kazi usiku. Malori kama haya ni mengi sana hapa nchi yaani yanaanza kufanya kazi kuanzia saa tano usiku mpaka saa kumi yanarudi kupaki.

1. Hayana bima

2.Hayana TRL

Madereva wake hawana leseni. Iwe likikamatwa tu linataifishwa na kwenda kuyeyushwa chuma chakavu na dereva wake kula mvua 14.

Ila wakati mungine pia ni muhimu kuendesha kwa tahadhari usiku, kwani wengi huwa tunachukua advantage ya barabara kuwa nyeupe kukanyaga mafuta.

R.I.P Frank

Hakuna aliye na akili timamu atakayeshindwa KUILAUMU SERIKALI MOJA KA MOJA KWA VIFO HIVI VISIVYO NA SABABU. Inashangaza na inasikitisha kwa kweli kwamba bado kama nchi hatujuwi kipi cha kufanya kuzuia vifo hivi vya kizembe kabisa. Yaani unaweza kukutana na mlori mbovu kupita kiasi ukipita mbele ya askari hakuna kupigwa mkOno wala nini mpaka unashindwa kuelewa inakuwaje kipofu au kalambishwa? Juzi rais amekwenda kutoa pole kwa watoto waliofariki kwenye ajali huko msoga. I was amazed kwamba kitendo kile kimeonekana cha kuungwa mkono ambacho hakina mfano. Ni kweli ni vizuri kutoa pole kama rais lakini pole yake hairudishi maisha yaliyopotea kizembe. Yeye kama rais anao uwezo wa kupunguza hizi ajali za kila mara. Amake sure wizara husika inafanya kazi zake ipasavyo full stop hata aipoenda kuhani hiyo misiba its ok. Lakini akihani na wengine wanaendelea kufa it doesnt help at all. Tuko wangapi atakwenda kuhani kote? Obvious no. President do s'thing tumechoka kuona watz wenzetu wakikatizwa maisha yao kwa uzembe wa wachache.

ooh LORD..tHIS IS SAD..MMMH MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI..AMIN

In a span of a week Taifa limepoteza vijana wawili kwenye barabara hiyo ya Bagamoyo maeneo ya Mbezi, na vifo vyao ni vya aina hiyo hiyo kugonga malori mabovu .... Kwa waliopita kwa Issa Michuzi watafahamu kuwa tulimpoteza bwana Dominic Mwita kwenye barabara hiyo ..

Raha ya Milele uwape ee Bwana na Mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani ... Amina.