Wednesday, March 31, 2010

tid ajitoa tuzo za kili music awards ?!


Wanajamvini nimeshitushwa kidoogo na taarifa hii ya msanii Khalid Mohamed a.k.a Top in Dar a.k.a T.I.D,kwamba amejitoa kwenye tuzo kubwa kabisa za muziki hapa Tanzania za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010,kwa mujibu wake na maandishi yake,ametoa sababu zake hizo hapo chini.

======= ======= ========== ==========


Naomba radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka pande zote za sayari hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye hiki kinyanganyiro cha award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka kwangu kujitoa kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za msingi:


1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.


2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwene same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!


3.Kwa sababu hizi ambazo mimi naona kwangu hazinijengi sioni sababu ya kuwepo kwenye TUNZO hizi tena kwani sidhani kama ni wakati wa kuwaangusha mashabiki wangu ambao natumia muda mwingi na effort binafsi bila ya mdhamini kuwaunganisha na muziki wangu basi nisameheni kama nimewakosea lakini hainisaidii chochote endeleeni na hao mnaowapa kila category i will never stop making good music for my country surely i wont,i was born to do


THIS,.. THANKS.


NB:Taarifa hii iko HAPA

Kuna Maoni 9 mpaka sasa.

TID stop being big head, how do you know that your music or videos are the best ? If you dont get the awards then there are some weakness on your production you need to assess your weakness and come up with a remedies to win the fun. There is no point of withdrawing from competition because you were not nominated, this show how immature your, you may be making a good music/videos but you dont know how to connect to the fun that is why they dont vote for you

Jela imekuharibu au umechanganyikiwa! Hizo sababu ulizotoa ni ufyolo mtupu, yaani ni upuuzi kupindukia! Kama video zako unasema ni za hali ya juu na hazipigiwi kura na wapenzi wako basi inakuonyesha kuwa labda pengine video zenyewe si lolote si chochote.

Grow up, son! Otherwise you will turn out to be another "has been" bongo flavor artists out there. Waulize akina Mr. Nice, Akil "The Brain", K-Lyn, Mez B, Nura, Ngwea, Sister P, Zay B etc, who, after much success, have fallen into oblivion.

Mara zote nimekuwa nikijiambia kuwa kuna TATIZO KUBWA kwa baadhi ya wasanii wetu, Leo nimeamini kuwa nilikuwa sijidanganyi...TATIZO LIPO.HIVI NI NANI KAKUDANGANYA KUWA WEWE NDO UNASTAHILI KULIKO WENGINE????!!! NDO TATIZO LENU WENGI MKISHALEWA VISIFA. we jitoe tu, sidhani kama itasaidia au kuathiri chochote kwa wewe kujitoa!!!!!! usiangalie ulipoangukia, angalia ulipojikwaa.....

chiggs

acha uwoga wewe unakimbie nini sasa mbana pua we

amshakundua hawezi pata tunzo kuna wakali zaidi yake ndio maana kasepa

TID!
Umefanya uamuzi wa busara kujitoa japo sababu zako ni nyepesi sana. Kwa kweli huitaji kupigiwa kura kupitia tuzo hizi maana ninaamini ubora wa kazi zako unapimwa kwa kipato unachopata na wala sii kwa kupitia kura za kili. Tulia fanya kazi na ubunifu kwa bidii sana na matokeo utayaona. Kikubwa hapa fuata nyayo za wakongwe kama njenje the kilimanjaro music band. They are making money, hawashiriki tuzo finyu na kazi zao ni zaubora wa hali ya juu na hawapigi kelele ya njaa hata mara moja. so kuwa makini na kazi zako zinalipa brother

mh! wadau kabla sijachangia naomba mnipe majina ya wanamuziki walioshindanishwa na tid,na walioshinda tuzo

Huyu anatumbuiza UK leo lakini mimi nina mada yangu kuhusu hizi trip za Ulaya. Tunafurahi sana kuona Ali Kiba, TID, Ray C, Mr Blu wanatumbuiza ulaya KILA SIKU.

Lakini pia muwe mnawapa chance kuleta vifaa vingine vipya kama kina Marlaw, Hussein Machozi, Baby J, Mwasiti, Maunda Zorro, Rama Dee.

Pia ningeomba BWANA MICHUZI uweke hii kama habari, mapromota wa Ulaya wamezidi kuleta wasanii hao hao kila mwaka, hii ni TOO MUCH.

We got new talent with songs to entertain the whole night, tunakubali mnatengeneza hela ya kutosha kwa kumleta Ali K.

Lakini itakuwa vizuri mki-balance kidogo na wasanii wengine wanaowika kwenye Bongo Flava

Pia msisahau kuwapeleka kwenye radio, tv, magazine, nk kwa ajili ya promo. (sio mnawabwaga kwenye klabu za uchochoroni tuu kila siku).

Ahsanteni

lol mambo ya kanye west....hahaha, who said u the best ?