Wednesday, March 31, 2010

sitoichukia nchi yangu tanzania,lakini kwa haya ntasema tu

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mateves iliyopo wilayani Arusha mkoani Arusha wakifanya mtihani wa majaribio wa nusu ya mwaka wakati wengine wakiwa wameketi chini kutokana na upungufu wa madarasa . Shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 910 ambao wanatumia madawati 320 tuuu katika madarasa hayo sasa hebu nambie upungufu uliopo. Piga picha hapo unambie wanasomaje hawa watoto wa A Town. Photo by Fredy Azzah

Kuna Maoni 9 mpaka sasa.

Duh jamani aibu kwa watanzania. Angalia magari wanaoendesha viongozi wetu? ilepesa iliyotumika kununua magari yakifahari shule ingepata madawati yakutosha shame on us.... vijana hawa ndiyo future viongozi wetu... inasikitisha

Itabidi walimu wakatae kufundisha madarasa ambayo wanafunzi wanasomea ktk hali hii. Kwani kama mazingira ya mwanafunzi ya kujifunza si mazuri basi mwalimu atakuwa anapoteza nguvu zake bureeee na pia inakatisha tamaa. Na pia hii itakuwa shinikizo kwa serikali ili waone umuhimu wa kuimarisha mazingira ya darasani. Si kweli kwamba serikali imeshindwa kuweka angalao madawati ya kutosha,mi naona kuna walakini ktk uongozi.


Walimu hawatendewi haki,wanafunzi vile vile, sekta ya elimu,nafuu ipo wapi? Kwa nini elimu inadharaulika hivi?

Nakubaliana nawe 100%
Jeee wasemaje kama kila mtanzania hapa ukerewe akitoa pound mbili au tano tu tuisaidie hiyo shule na future viongozi wetu....
Bwana mdogo anzisha paypal account ili tuanze mchango
Wakatabahu

Jamani hata madawati tungojee misaada kutoka nje. Kweli viongozi wetu hawana aibu. Wenyewe watoto wao wanapelekwa kusomea nchi za nje. Yaani hii picha inatia uchungu.

Jamani hata madawati tungojee misaada kutoka nje. Kweli viongozi wetu hawana aibu. Wenyewe watoto wao wanapelekwa kusomea nchi za nje. Yaani hii picha inatia uchungu.

Ndo maana wao wanapeleka watoto wao Private school, ni kiongozi gani wa sasa mwenye mtoto anayesoma Gvt school na awe wakwanza kujitokeza, watoto wa wa lalahoi watopata Elimu bora wapi hii ndiyo bongo yetu zaidi unavyo ijua, hatamkichangia zinaweza zisifike, cha umuhimu ni Gvt kujua wajibu wake kwa jamii ni welfare to the citizens and not welfare to mafisadi

watumie vizuri kura zao pindi uchaguzi unapofika, halafu hapa bado kunawapuuzi wanawaza kujenga maflyover

Maskini! Hii mpya kwa shule za sec nilikuwa sijaona! Karne ya 21 Mwanafunzi wa sec anakaa chini! Na kuna watu huko serikalini wanajiita viongozi Magaria ya Mil 150 ndio wanaendesha kama dawati 1 linagharibu tuseme 20000 hayo ni madawati 7500 zaidi ya shule 10
Huu ubinafsi ndio unaotuua

Maskini! Hii mpya kwa shule za sec nilikuwa sijaona! Karne ya 21 Mwanafunzi wa sec anakaa chini! Na kuna watu huko serikalini wanajiita viongozi Magaria ya Mil 150 ndio wanaendesha kama dawati 1 linagharibu tuseme 20000 hayo ni madawati 7500 zaidi ya shule 10
Huu ubinafsi ndio unaotuua