Ndani ya Jiachie leo King Kif kutoka www.kingkif.blogspot.com najiachia na madude ya muziki wa Hip-Hop ambao hapo zamani hapa Bongo tuliuita muziki wa kufokafoka , hiyo ilikuwa mwishoni mwa miaka ya themanini na tisini mwanzanzoni.Basi bwana, hapa kwanza kabisa kunahitajika kufahamu nini maana ya sayansi na nini maana ya Philosophy.
Science means a techinique to simplify work which includes branches such as mathematics anda Geography.
SAYANSI NA HIP-HOP
Sayansi na Hip-Hop ; Hip-Hop ni lazima iandikwe kwa kutumia mizani , hii ina maana lazima uwe na idadi maalum ya mizania katika mistari ili mashairi yako yaweze kuimbika(kuchanika).
Pia beats (midundo) ya Hip-Hop lazima igonge katika mahesabu maalum ambayo kwa Hip-Hop ni 4 (four) , hivyo hata mistari inahimizwa kuangukia kwenye hesabu hiyo hiyo ya vigawe vya 4(nue) yaani 4,8,12 na kuendelea .
Hapo tunaona wazi hesabu inavyotawala katika uhunzi mzima wa mashairi na beats(midundo) ili kufanya ama kujenga kitu kinachoitwa HipHop.
Means love anda wisdom (hekima na upendo ) , ni neno (lenye asili ya Kigiriki). Philo means love and Sophia means Wisdom.
Philosophy na Hip-Hop ; ni wazi kabia na haipingiki kwamba muziki huo unaleta upendo ikiwa ni pamoja na kutumika njia ya kuleta ama kudai haki , kukemea unyonjaji katika jamii na kadhalika.
Aidha, mistari ama mashairi bora ni yale yaliyo na hekima yasikilizwapo katika masiko ya watu na si vinginevyo , mfano ni mistari inayopatikana kwenye traki kali iitwayo " I know i can" ya Nas . Traki hii ina maneno ya hekima na upendo ndani yake juu ya maisha kuanzia utoto hadi utu uzima.
Hii hapa mifano mingine kadhaa ya watu ama niandike maemsii walioweza kujiita Hip-Hop mathematic ambao ni kama vile RZA ambaye ni kiongozi wa kundi mahiri la Wu Tang Clan , yupo Cani-Bus , yupo Mos Def .Pia yupo jamaa mmoja aitwaye Keith Muray wa kundi la DEF Squad na wengine wengi .
King kif kutoka www.kingkif.blogspot.com namaliza hapa huku nikisisitiza Hip-Hop bila Science $ Philoph ni pumba tupu na hata mashabiki hasa hapa Tanzania waufuatilie kwa undani muziki huu na waache ushabiki mandazi.













Kuna Maoni 5 mpaka sasa.
Kweli King Kif unainyaka HipHop.
Mwanangu!Leo umetoa somo kali sana.Sikutegemea!!!
samahani kaka angu,hebu fuatilia vizuri hiyo maana ya philosophy, ni kama haija kaa sawa.
ooh nilitaka kujiuliza kama El hadji Diofu ameacha soka na kuanza kurap.hehehe.
somo poa lakini umekosea,usiandike vitu kama ujui,rza hajawahi kuwa kiongozi wa wu tang clan,bali ni mdhamini wa kundi,rza ndo mwenye studio za wu tang na organisation zote za wu tang clan,maana wu tang clan asili ya ni black muslim,hawa ambao malcolm x pia alikuwepo lakini badaye alikuja kutoka,kiongozi wa wu tang clan alikuwa ODB or old dirty bastard,na baadae alivyofariki likawa linaongozwa na shameek a.k.a metod man,kwa sasa ni gosty face killer ambaye bado yuko kwenye game,wengine wamepoa kidogo,lakinisio kusema ndo wametoka kwenye music.
Post a Comment