Thursday, February 25, 2010

Utambaji wa Hadithi Jukwaani!

Karibu Soma mkahawani ukutane na Ghonche Materego mtambaji mahiri wa hadithi jukwaani…
Huu ni utanzu mkongwe ulioshamiri enzi za mababu na bibi zetu ambao umehuishwa kwa kutumia mbinu za sanaa za maonyesho.
Onyesho litasindikizwa na majadiliano, maonyesho ya vipaji vya papo kwa papo na ushairi wa kisasa.
Muda: 12:00 alasiri hadi 2:00 usiku
Tarehe: 26/02/2010 (IJUMAA).

Uenzi utamaduni wako, furahia utamu wa neno
Njoo pia uburudike kwa vinywaji moto na baridi, vitafunwa vya aina mbalimbali kwa bei sawa karibu na bure mkahawani.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.