Hongera kwa kutupa nafasi nzuri ya kuchangia mawazo katika ujenzi wa taifa letu.Leo jumapili natimiza miaka 44, lakini bado niko fiti, na ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema na masiha mazuri, pamoja na familia yenye amani. Swala ambalo limekuwa likinisumbua ni kuhusu hatima ya taifa letu lililokumbwa na ufisadi mkubwa kiasi kwamba walalahoi hawana sauti tena.
Ila vijana wachache mahiri kama nabii US-Blogger, Yohanna Mashaka, Dr. Shayo, Mwanakijiji lazima tuwape pongezi kwa jitihada zao za kuielemisha jamii ya kitanzania.Nimewasiliana na Nabii Yohanna Mashaka, kadhalika na His Chief of Staff Dr. Shayo, and Vice President Mwamvitta na wamekubali kushiriki katika mjadala wetu "live" hivi karibuni. Itatangazwa moja kwa moja kupitia EATV na Clouds FM. Bado nipo kwenye harakati za kukamilisha shuguli na kutangaza mjadala mzima. Nchi ni yetu vijana kwa hiyo lazima tushirikiane. alafu niko single, kwa hiyo kama ni sista eligible basi nishtue.
Kwa maana hiyo, nimeamua kujitambulisha rasmi kwa globu ya jamii na Tanzania kwa ujumla nikijitayarisha katika kinyang'anyiro cha jimbo la Temeke. Na pia ningependa kushirikiana na vijana wa kitanzania ili tuendeleze libeneke la kuborosha utalii wa kitanzania, hasa kuitangaza nchi yetu tukiwa ughaibuni. Kwa hiyo wote wanaoniita jini, hapana ni wenu mtiifu
Happi Besdei Yangu
Dr. Mohammed Hassan Mtoro












Kuna Maoni 3 mpaka sasa.
kaka,mlete us blogger kwa mzee kule (michuzi senior)na yeye ajadiliwe kama john mashaka please.
SIKU NYINGI NIMEPIGA KELELE KWANI US BLOGGER HAKUTANI NA ISSA MICHUZI NA MIE NAMFAGILIA NA KAZI ZAKE? ILA US BLOGGER UNAONAJE SUALA LA RUGE NA MR 2 USIJE KUGEUKA SABABU NAONA UNATAKAK UFANYA KAZI NA CLOUDS FM NA EATV NDIO HAOHAO KINA RUGE ANAPENDELEWA NA JANUARY MAKAMBA, INASIKITIKA WANAMUINGILIA KAZI YAKE MR 2 NINGEPENDA KUONA UNATOWA UKIMYA NA KUTETEA UKWELI. PAZI. SIWEZI KUSEMA MR 2 ANA HAKI HILO SIJUI ILA RUGE ANACHOFANYA SI VIZURI MPAKA KWA MICHUZI WAMETOA KUHUSU RUGE JE ANAOGOPEWA? PAZI.
kumbe huyu ndo US blogger?? lol!! nilitamani saana nikujue haki ya nani mlete kwa misupu mbona umekuja kujifich huku mlete kwa mkuu fasta yani kijiwe kitanoga kweli
Post a Comment