Sunday, January 31, 2010

last episode ya umodo na nyota wake wa mchezo ni happy witney

Huyu ndiye mshindi wa shindano la UMODOTZ,Happywitney Gumbo baada ya kuwatupa kule washiriki wenzake 11,onesho hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.Kimsingi ni shindano ambalo kiukweli lilifana na lilivutia sana,kikubwa Bro Taji ukumbuke kwamba mwanzo ni mgumu kwa unachokifanya,lakini naamini kwa juhudi na ubunifu wako ulioutumia na kuhakikisha onesho hilo linafana,basi safari yako bado ni ndefu lakini inaonekana kuwa na matunda matamu (ingawaje hakuna matunda matamu bila miba),ambayo hapo mbeleni hata jamii italikubali onesho hili na kulifanya liwe onesho mojawapo kubwa na lenye mafanikio kuliko mengine yote hapa Tanzania,kama kuna kasoro zozote zilizokuwepo basi ni kibinadaamu tu lakini naamini kabisa shindano litakalofuata wengi hawataamini.Bro Taji JIACHIE inakupa BIG UP sana kwa ulichokifanya,inasema SAFARI NI HATUA.
Mshindi wa shindano hilo Happywitney akihojiwa na mtangazaji wa kituo cha Mliman TV huku mama yake akimuangalia kwa msisitizo safi kabisa huku akiwa amemkumbatia
Mshindi wa onesho la UMODOTZ Happywitney Gumbo akikabidhiwa cheki yake la mbili nje ya mkataba wake wa kazi wa mwaka mmoja alioahidiwa kutoka Shear Illusions ambao ndiyo wadhamini wakuu wa onesho hilo,anayemkabidhi ni muwakilishi wa shear Illusions aitwaye Neema,shoto ni mratibu wa onesho hilo Magesa pamoja na mwandaaji kulia, Taji Liundi.Washiriki wengine walipewa vifuta jasho pamoa na vipodozi mbalimbali kutoka Shear Illusions
Happywitney Gumbo akilakiwa na washiriki wenzake mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mshindi wa onesho hilo
Mshindi wa jumla wa shindano la UMODOTZ,Happywitney Gumbo akiwa haamini masikio yake mara baada ya kutajwa kuwa yeye ndiye kinara wa onesho hilo usiku wa kuamkia leo
Pichani shoto ni Modo Nshoma akikabidhiwa shilingi elfu hamsini kumpongeza kwa kuwa msichana wa kwanza kukubali kwende kupima Ukimwi wakati wa mchakato wa shindano hilo likiendelea.
Muaandaji wa onesho la Umodotz Taji Liundi akiweka sawa mchakato wa kumtaja mshindi wa onesho hilo usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya GIRAFFE OCEAN VIEW
Pichani ni baadhi ya wadau ambao Blog ya Umodo ilipata ushauri kuhusu onesho hilo akiwemo Steven Kanumba(filamu), Slyvia Shao(Urembo) na mbunifu Kemmi Kalikawe (mitindo) ambao wanawakilisha nyanja mbalimbali zinazoshabiiana na maswala ya mitindo,wengineo pichani shot ni Yusuf,kulia Taji Liundi ambaye ndiye Muaandaji na mratibu wa onesho hilo,msaidizi wake Magesa wakiwa jukwaani kabla ya mshindi kuwekwa hadharani.

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

Great start , and wonderfull models ,Include pictures from other sponsors asante