wikend njema kwa wadau

Friday, July 31, 2009
Dada nanihiiii anawatakiwa Wikend ilionjema kabisa wadau wote wa Blog hii popote pale mlipo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 3

tano bora wenye vipaji redds miss ilala hawa hapa

Toka shoto ni Zena Rashidy (22), Slyvia Shally (19), Magreth Peter (21), Wa nne jina limenitoka kidoooogo wadau na Doris Jimmy (18)
Pichani ni washiriki watano bora wa Redds miss Ilala 2009 waliochaguliwa usiku wa kuamkia leo katika shindano la kuwasaka warembo wenye vipaji,lililofanyika ndani ya hotel ya Lamada Ilala,jijini Dar.Redds Miss Ilala 2009 inaandaliwa/ratibiwa na kampuni ya Dar Metropolitan kupitia kwa Mkurugenzi wake Jackson Kalikumtima
Mmetuona lakini ninyi warembo wa miss Kinondoni na miss Temeke tulivyofiti kila idara?
Baadhi ya walimbwende wa wakipata vinywaji jana usiku kwenye shindano la kuwasaka Redds Miss Ilala 2009 wenye vipaji vya kucheza na kuimba,shindano hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo katika hotel ya Lamada,Ilala jijini dar.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 1

galinoma amaliza vakesheni yake nchini italy


Msanii GALINOMA anaeishi na kufanya kazi nchini Uholanzi pichani akiagana na Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy leo mchana baada ya kumaliza mapumziko yake ya wiki tatu.GALINOMA katika mapumziko yake pia alimsindikiza msanii wa kizazi kipya (bongo flava) MAVUMBI katika track inayoitwa "UHAKIKA" . MAVUMBI ni msanii anaeishi Italy na kufanya shughuli zake za mziki chini ya SEEWEAR & GFAMILY PRODUCTION. Galinoma anategemea kurudi Italy kwa show ya uzinduzi wa album yake mpya "SAMAHANI" iliyoingia sokoni hivi karibuni.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

tshet za BIGG RESPECT CLASSIC WEAR zazidi kutesa bongo




Haya haya wadau popote pale mlipo BIGG RESPECT CLASSIC WEAR inawataarifu kuwa tshet zenye viwango na ubora bomba kabisa zenye maandishi ya kibongo zinazonunuliwa kama njugu kwa sasa zenye,kama vile:.PESA NDIO KILA KITU,PESA SIO KILA KITU,FITNA MWANZO MWISHO,ZIMEBAKI STORY,DUNIA NDIO MAMA,KAMA NOMA IWE NOMA,UMEFULIA,BADO SIJAFULIA MTU WANGU,NANI HATAKI ?,WA UKWELI ORIGINAL,NAJUTA KUKUFAHAMU,INABIDI WAZOEE,WANAKUBALI KIAINA,WEWE TU MIMI SINA HABARI,SAFARI SIO KIFO,BADO NIPO NIPO,FULL HANDAS na nyingnezo.
NB.RANGI ZOTE ZIPO UKITAKA KUAGIZA WASILIANA NA BIGG RESPECT CLASSIC WEAR kwa mawasiliano yake cheki bana lake hapo juu au mbonyezee kwa namba 0754 439502

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ama kweli pombe si juisi





Kuna picha hizi za kuvunja mbavu za walevi tungependa tushee na wadau waburudike
Picha zaidi unaweza ukawapa wadau link hii
http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=129431
NIFAHAMISHE.COM TEAM
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

sikiliza kila siku 102.6 choice fm


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

waraka kutoka kwa dada greta

Habari yako Michuzi Jr,

Pole na jukumu zito la kutuhabarisha, Mungu azidi kukubariki.
Mimi ni mwanamke umri wangu miaka 39, ni muathirika wa ukimwi yaani HIV positive.Nimejitoa hapa kwa ajili ya kutafuta marafiki wa kubadilishana nao mawazo, kwani najua kwa kupitia njia hii nitapata marafiki mbalimbali hata wale wenye hali kama yangu na tutaweza kuliwazana.
Ninaishi Dar na ninafanya shughuli zangu hapa Dar, pia afya yangu ni njema namshukuru Mungu kwa hilo.Wale wote watakaopenda kuwasiliana nami watumie email: gretageorge71@yahoo.com
Nawapenda wote na Mungu awabariki.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

muziki nauweka kando kwa muda,ukiritimba umezidi

Pichani ni Afande Sele akiwa amebebwa na mashabiki wake kwenye moja ya maonesho yake aliyowahi kuyafanya hivi karibuni .


Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya (hip hop),Afande Sele a.k.a Simba Mzee amesema kuwa kwa sasa ameamua kujiweka kando kwa muda katika kujihusisha na muziki kutokana na ukiritimba uiliopo kwenye vyombo vya habari hususani kwenye vituo vya redio.


Afande Sele ameyasema hayo hivi karibuni alipoongeza na gazeti la Tanzania Daima,akisisitiza kuwa,muziki wa bongofleva hauwezi kusimama ikiwa hip hop itaendelea kuyumbishwa kwa kubaniwa kweny vituo vya redio na wadau wachache ambao hawazichezi nyimbo za ukweli na kuzipa kipaumbele zile zisizo na maadili mema.


"Nipo Morogoro,nimeamua kufanya kazi zangu za shambani kwa muda,imeniuma sana kuona wimbo wangu wa zanzibar ni Nchi kubaniwa wakati hata viongozi wa siasa wa juu waliufagilia,wakati huo huo nyimbo za mapenzi zinapewa kipaumbele.Kwa hali hiyo ndiyo maana muziki wa bongofleva wa sasa imefunikwa bao na taarab na dansi"alisema afande Sele.


Habari kwa hisani ya gazeti la Tanzania Daima.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 0

miss kanda ya ziwa 2009 wako mnato ile mbaya.!

MIRIAM GERALD (21 ) MWANZA
MARY JOSEPH (19) MARA
Pichani ni warembo wa miss kanda ya ziwa 2009 watakaochuana siku ya tarehe 7/8/2009 ijumaa, pale Yatch Club jijini Mwanza kwa mpambano mkali wa kumsaka atakae mvua taji Miss TZ 2008 Nasreen Karim ambaye pia anashikilia taji la Miss Mwanza. Hakika mchuano unaonekana utakuwa mkali kwani washiriki woote wako bomba saaana!!
JE KANDA YA ZIWA INAWEZA KUTOA TENA MISS TANZANIA 2009? MATUMAINI YAPO TUNAWAOMBEA WAFANYE VUZURI HESHIMA IRUDI TENA KANDA YA ZIWA.
Kwa picha zaidi tembelea:
florasalon.blogspot.com

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, July 31, 2009 | | Permalink | Maoni 2

ukarabati wa kipita shoto chetu

Thursday, July 30, 2009
Kipita shoto chetu cha Posta Mpya kilichopo katika kati ya jiji la dar kikifanyiwa ukarabati mkubwa kama kinavyoonekana leo mchana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

baada ya tizi majadiliano kidoogo

Mkurugenzi wa Fitness Clabu, Kel Ken(katikati) akijadili jambo na wanachama wa Klabu hiyo,bigg Respect(Kushoto) na Issa Mussa, leo katika Gym ya Kel Ken, kuhusiana na Tamasha la Bonanza litakalofanyika siku ya agosti 8 2009 katika ufukwe wa South Beach Kigamboni,jijini dar
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

apata kipigo kwa kudaiwa kukwapua kipochi posta

Baada ya kula kibano kwa sana,akaachiwa atambae zake
anakula kibano laini

Nikapasuee eehh..!
Haya inuka tweeende,tumechoka na nyinyi alaa.!


Jamani mimi sijaibaaaa jamaaaaani..!
Mkazi wa Dar es Salaam ambaye alisadikiwa kuiba kipochi katika mitaa ya Posta Dar es Salaam, akiwa katika wakati mgumu baada ya kupewa kipigo na wasamalia wema, hata hivyo aliachiliwa baada ya kukosekana aliyeibiwa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 2

tizi la viungo


Mkufunzi wa masuala ya Viungo katika timu ya KelKen Fitness, Magnus Simon, (kushoto) akimfanyisha mazoezi ya Viungo mwanafunzi wa Timu hiyo, haruna shekena, wakati wa maandalizi ya Tamasha la Bonanza litakalofanyika tarehe 8 Augost mwaka huu katika Ufukwe wa South Beach Kigamboni,jijini Dar
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ayaaa..!! akadabra.!

Pichani ni mfanyabiashara wa machungwa ambaye alikuwa katika harakati za kuwakwepa askari Mgambo, akiokota machungwa yake baada ya kudondosha sinia lake katikati ya barabara ya Chang'ombe,jijini Dar, hali iliyopelekea pia kutishia usalama wa maisha yake na pia angeweza kusababisha ajali
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

abiria 45 wanusurika kufa kufuatia basi la mbilinyi express kuteketea kwa moto

Abiria 45 waliokuwa wakisafiri katika basi la Abiria kati ya SONGEA na MCHOMORO wilayani NAMTUMBO katika Mkoa wa RUVUMA wamenusurika kufa baada ya basi hilo kuteketea kwa moto.
Basi hilo Mbilinyi Express limeteketea kwa moto katika eneo la NONGANONGA lililopo katika barabara ya SONGEA NAMTUMBO majira ya saa saba za Mchana hii leo (30.07.2009) .
Mkuu wa kikosi cha Zimamoto katika wilaya ya SONGEA KELVIN MAPUNDA amesema abiria wote waliokuwamo ndani ya basi hilo walifanikiwa kujiokoa kwa kutoka nje mara baada ya basi hilo kuwaka moto isipokuwa bibi mmoja aitwaye MWANANURU HASSAN ambaye ameumia kutokana na kukanyagwa na abiria wenzake.
Hata hivyo MAPUNDA amekiri kuwa kikosi chake kilichotumia mitungi ya kuzima moto badala ya gari la Zimamoto ambalo ni bovu, hakikufanikiwa kunusuru mali yoyote.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

the sexiest man in dar akabidhiwa tita lake rasmi na clouds fm 88.4

Moracka hureeeee.....! Hebu mcheki Mchomvu alivyonuna
Mie nikimpongeza Moracka kwa ushindi wake mnono wa kuibuka na hilo titazzzzz leo jioni hapa mjengoni.
Adam Mchomvu baado tu anataka kuhakikisha..!
Hapa akiwa amepozi na mwanalibeneke mwenzangu Dj Choka
Baadhi ya vijana wa mjengoni Clouds Fm,kulia Dj Bulla,B 12 (xxl) pamoja na Adam Mchovu wakihakikisha mkwanja kama uko sawa,ila hapa Adam wamchunge sanaa....anaweza akananihiiiiii msimbazi mmoja oohooo.!

Moracka akifurahia kitita chake alichokabidhiwa leo jioni na Clouds Fm 88.4

Mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 Kapt G habash (kwa niaba ya Clouds Entertainment)akimkabidhi rasmi kitita cha shilingi milioni moja na laki tano mshindi wa shindano la The Sexiet Man in Dar,Moracka leo jioni mjengoni hapo,Mikocheni jijini Dar.Shindano hilo lilikuwa likiendeshwa na kipindi cha Ala Za Roho kikiongozwa na Loveness Love a.k.a Diva kirushwacho usiku na redio ya Clouds Fm.Moracka amewabwaga wenzake hawa hapa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 13

KUMRADHI WADAU WETU WA DULLONET

Habari za kazi wanamtandao wenzangu.
Kwanza tunapenda kuwaomba radhi kutokana na kutopatikana hewani kwa website yetu ya Dullonet, hii ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Naomba kwa muda muweze kutupata katika link ya
www.habarinamatangazo.net mpaka hapo tutakaporekebisha tatizo hili lililotupata. Tunaomba radhi kwa mara nyingine lakini kwa kupitia link hiyo mambo yataendelea kama kawaida. Dullonet Daima.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Mkutano wa kuanzisha jumuia ya watanzania katika Jimbo la Gauteng

Ndugu Mwanablogu,Watanzania waishio jimbo la Gauteng, Afrika Kusini wanatarajia kuanzisha umoja wao katika siku za karibuni. Blogu yako ni miongoni ya zile zinasomwa na watu wengi ikiwa pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi Afrika Kusini. Ninaomba utupatie nafasi ili tuweze kufikisha ujumbe huu muhimu kwa watanzania wengi zaidi.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.Mwenzenu
Dr Faustine
********************************************************
*******************************************
Mkutano
Mkutano wa kuanzisha jumuia ya watanzania katika Jimbo la Gauteng
Watanzania waishio katika Jimbo la Gauteng (Johannesburg na Pretoria) wanatarajia kufanya mkutano wa kuanzisha jumuia yao tarehe 22 mwezi wa Agosti 2009 jijini Johannesburg. Mkutano huu utatoa fursa ya kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu jumuia hii pamoja na kuchagua viongozi wa kudumu.
Watanzania wanaoishi kwenye miji ya Johannesburg na Pretoria ambao wangependa kuwa wanachama na pia kushiriki kwenye uchaguzi wa uongozi wa jumuia wanakaribishwa kuwasiliana na wajumbe wafuatao kwa maelezo zaidi:
Brian Mshana
Laurean Rugambwa bwanakunu@gmail.com
Faustine Ndugulile drfaustinen@aol.com
Shukrani
KAMATI YA MAANDALIZI
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

LIBENEKE LA ZIARA YA WANAUME TMK FAMILY NA TIP TOP INAENDELEA


SHOW INAITWA DOUBLE T KAZINI TOUR,NI UZINDUZI WA ALBUM TATU,YA KWANZA MHESHIMIWA TEMBA MTOTO WA KICHAGA,YA PILI MKUBWA FELA INAITWA MKUBWA NA WANAWE NA TATU PESA YA MADEE,SHOW ZILIFANYIKA TAREHE 24 SUMBAWANGA UKUMBI UPENDO HALL,TAREHE 25 MBEYA UWANJA WA SOKOINE TAR 26 IRINGA UWANJA WA SAMORA, TOUR ITAENDELEA TAREHE 8 MWEZI WA 8 KATIKA MKOA WA MOROGORO KWENYE VIWANJA VYA NANE NANE MCHANA NA USIKU KWENYE UKUMBI WA BWALO LA UMWEMA N TAREHE 9 MJINI DODOMA KATIKA UWANJA WA JAMHURI MCHANA,TAREHE 14 TOUR ITANDELEA MJINI MOMBASA KATIKA UKUMBI WA JAMBOREE,NA TAREHE 15 MOMBASA KATIKA UWANJA WA COAST CAR PARK TAREHE 16 MJINI TANGA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI,WASANII WATAOKUWEPO NI TMK WANAUME FAMILY,MH TEMBA,CHEGE,KR,STICKO,ZOZO,TRIPPLE,LAKEEZ,KICHWA NA MKUBWA FELLA,TIP TOP CONNECTION,MADEE,KASSIM,KEYSHA,TUNDAMAN,SPACK WATAKAOSINDIKIZA NI MANGWEA NA BERRYBLACK KUTOKA ZANZIBAR
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

hepi besdei ya miaka mitano ya globu ya jamii yanukia


anko nanihii akipeana mikono na mwana wa mfalme wa mambo ya globu ndesanjo macha septemba 8, 2005 kwenye ukumbi wa finlandia hall huko helsinki, finland, hii ikiwa ni taswira ya kwanza ya toka kuanzishwa kwa globu ya jamii ambapoo jumamosi baada ya hii ijayonitatimiza miaka mitano kesh! (vekesheni zilianza kitambo ati!!)

kunradhi wadau lakini naomba niseme wazi kwamba kama si ndesanjo macha hapangekuwa na libeneke na anko nanihii wala asingekuwa nanihii unayemjua leo.

kwa lugha ingine huyu ndiye aliyefanikisha kila kitu katika mambo haya. mtembelee uone vitu vyake kwa kubofya
HAPA na HAPA na HAPA.

ukishamtembelea kote huko utajua ni kwa nini nammaindi sana ndesanjo macha ambaye kwangu mimi ndio kama mama na baba wa libeneke. vile vile ukimsoma ndesanjo macha kwa makini utapata jibu la ufanyeje kuanzisha libeneke la globu pamoja na mambo mengine. huyu mwana wa mfalme wa libeneke hana uchoyo, anapenda kila mmoja wetu aendeleze libeneke...

endapo kama mambo yataenda kama anko nanihii alivyopanga basi kutaandaliwa bash la ubwete kusherehekea hepi besdei ya miaka mitano ya globu ya jamii. kama vipi angalau wadau walitambue hilo, kwamba globu hii inajihisi ina deni kubwa kutoka kwa wadau walioifikisha hapa ilipo.

si jambo dogo ama la masikhara kwani miaka mitano ya libeneke ni umri tosha wa mdau, na kama inavyoeleweka angekuwa mtu basi saa hizi angekuwa darasa la kwanza. na ndivyo globu ya jamii ianavyojisikia kwa sasa. yaani ndio kwanza safari imeanza, na miaka mitano ni cha mtoto.

siku ya siku ikiwadia ya hepi besdei anko nanihii atatoa hutba rasmi, lakini kwa sasa si vibaya kuwashukuru wadau wote kwa kampani yao muda wote huu, kwani safari ina mabonde, miteremko na kashkash kibao ambazo kama una roho ndogo unaweza kuachia bodi.

nawashukuru sana wadau wanaoendeleza libeneke kwa kutuma taswira ama lolote lile ili tushee nao kwenye globu ya jamii. na hapa anko nanihii anaomba kwa unyenyekevu kuweka jambo moja wazi. globu ya jamii haibaugui na wala haichagui. kama mdau una lako jambo ambalo hakichafui hali ya hewa basi litabandikwa tu. likitupwa kapuni ujue umenoa stepu.

hali hiyo ya kutochagua ama kutobagua inalenga sehemu zoteza itikadi iwe dini, siasa, jinsia na hata libeneke la kufurahisha baraza tu. nasema hivi kwa sababu kuna minongóngo kwamba globu hii inapendelea chama fulani tu cha siasa ama imani fulani tu ya dini.

naomba nikanushe tuhuma hizo nzito na kukazia kwamba endapo hao wanaoona hawapewi kipaumbele na globu ya jamii hawaleti taswira na khabari zao kifanyike nini???? hapa kwa ufafanuzi ni kwamba kila jamii iko huru kuleta wakitakacho kwa kutumia issamichuzi@gmail.com na kisha endapo kama kitaminywa (na hapa kiwe hakichafui hali ya hewa) ndipo mdau ama muosha kinywa ulalame.

ANGALIZO: globu ya jamii haibagui itikadi ya dini ama siasa, jinsia, aman mada ama libeneke lolote lile lisilochafua hali ya hewa. hivyo endapo wewe ni Mkristo, Mwislamu, Mpagani, CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, TLP na kadhalika lete tutaswira na khabari tuendeleze libeneke. Ila usilalamike wakati wenzio wanaleta wewe unakaa navyo huko uliko.
-Michuzi
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

raha ya ujasiliamali

Mjasiliamali mkimtajia bei ya bidhaa yake (mapapai) kwa mama mpita njia ambaye alionekana kuvutiwa na ubora wa mapapai hayo.
Mdau ameamua kuwa mjasiliamali,kwa kufanya biashara ya matunda,pichani ameyaleta leo mjini kutoka shamba ambako anaamini hakuna wateja kutokana na bidhaa hiyo kupatikana kwa wingi.kila moja analiuza kati ya 500 mpaka 1000.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

haya hapa nani anakiuka sheria za barabarani?


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 4

please vote for Mwana FA in Channel O Music Awards


Tanzanian Bongo Flava artist Hamis Mwinjuma aka Mwana FA has been nominated by Channel O Music Awards.Which is gonna be held in Johannesburg South Africa on 29th October 2009.


His video track name NAONGEA NA WEWE featuring AY has been nominated into two categories The Most Gifted Group (DUO) and The Most Gifted East African Video.



MwanaFa and Ay are begging you mdau to vote so as they can win the awards, as by winning this they will put up Bongo flava on the world map.



Take your time and remember to vote for our country and our music and our artistes:


HOW TO VOTE


To vote, MWANAFA The Most Gifted or Duo must SMS 4E to +27839208400


To vote, MWANAFA The Gifted East Africa Video must SMS 13B to +27839208400 (International SMS rates apply) or vote on http://www.channelo.tv/

You can vote as many times as you want!

RegardsMwanaFA & AY…

GOD BLESS BONGO FLAVA
-
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, July 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

laurence masha mgeni rasmi miss redds kinondoni 2009

Wednesday, July 29, 2009
Baadhi ya walimbwende wa redds miss kinondoni 2009 ndani ya mjengoni jioni hii
Moja ya kichwa mahiri kupitia fani ya utangazaji ndani ya Clouds Fm 88.4 alias Mjengoni Kapt Gadner G Habash akizungumza na walimbwende watakaoshiriki kuwania taji la Redds Miss Kinondoni 2009 leo jioni mjengoni hapo Mikocheni,jijini Dar kuhusiana na namna walivyojiandaa kwenye mchuano huo mkali na wa kuvutia.
Aidha shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Boy George Promotions limeweka bayana zawadi mbalimbali watakazozinyakuwa washiriki hao,ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha shilingi milioni moja na laki tano taslim,mshindi wa pili atanyakua kitita cha shilingi milioni Moja,mshindi wa tatu atapata shilingi Laki nane,mshindi wa nne na tano watajinyakulia kiasi cha shilingi laki tatu kila mmoja na waliobaki watapata kifuta jasho cha shilingi laki moja na nusu.
Onesho hilo litakalofanyika siku ya ijumaa pale Mlimani City-Mwenge jijini Dar,kiingilio kimepangwa kuwa ni 10,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu kwa shilingi 40,000/= kwa kila kichwa.Kwa upande wa burudani kundi la Wazee wa Ngwasuma litatoa burudani kambambe kwa wegeni mbalimbali watakaofika katika onesho hilo.
Katika onesho hilo mgeni rasmi atakuw ni Waziri wa mambo ya Ndani Mh.Laurence Masha
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, July 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

anaonekana anatamani sana kuwa mwanamuziki


Kijana anaonekana anapenda sana kuwa mwanamuziki na anatamani awe kama Marehemu Ndala Kasheba.! Mbali hiyo anatamani sana siku moja aifute dhana ya baadhi ya watu wanaoufananisha muziki wa kizazi kipya alias bongofleva kama BIG G au Badhoka.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, July 29, 2009 | | Permalink | Maoni 4

Twanga Pepeta 'Kusugua Kisigino' Kiwalani


BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta International' inatarajia kuwapa mashabiki wake wa Kiwalani, Dar es Salaam, burudani ya staili yake mpya iliyoshika kasi ya 'Sugua Kisigino' kwenye ukumbi wa Gaza Strip.



Mkurugenzi wa Kampuni ya First Entertainment iliyoandaa onyesho hilo, Victorian Nachenga 'Victor Buguruni', alisema Dar es Salaam jana kuwa bendi hiyo itafanya onyesho hilo Alhamisi (Julai 30, mwaka huu) kuanzia saa 3 usiku kwa kiingilio cha sh. 5,000.


Victorian alisema Twanga Pepeta itasugua kisigino kwa wakazi wa Kiwalani na vitongoji vyake, onyesho ambalo pia ni sehemu ya kuendelea kutambulisha albamu ya 10 ya bendi hiyo, Mwana Dar es Salaam iliyozinduliwa mwezi uliopita kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.


Alisema onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wengine wakiwamo Mrisho Mpoto 'Mjomba', Athuman Ford 'Wabogojo', Steve Nyerere na Sunche na Kapeto. Mkurugenzi huyo alisema katika onyesho hilo maalumu, bendi hiyo itatambulisha nyimbo zake saba mpya zikiwamo Sumu ya Mapenzi uliotungwa na Khalid Chuma 'Chokoraa', Mwisho wa ubaya ni aibu (Saulo John 'Ferguson'), Sintopenda tena (Saleh Kupaza), Nazi haivunji jiwe.


Nyingine ni Shida Darasa na Mwana Dar es Salaam uliobeba jina la albamu, zilizotungwa na Charles Gabriel 'Chalz Baba' na mwingine uliotungwa na Rogart Hega 'Katapila'. Albamu nyingine ambazo bendi hiyo imewahi kutoa na kutamba katika anga za muziki nchini ni Kisa cha Mpemba mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali uzeeni (2001), Chuki binafsi (2002), Ukubwa jiwe (2003), Mtu pesa (2004), Safari 2005 (2005) na Password (2006).
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, July 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

KAMPUNI ya New Habari (2006) Limited kudhamini shindano la vodacom miss tanzania 2009 mil 80.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Udhamini na Matukio wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Petter Mwendapole akibadilishana mkataba wa udhamini wa shindano la Miss Tanzania na mkurugenzi wa Lino Agency waandaji wa michuano hiyo, Hashimu Lundenga wakati wa hafla iliyofanyika leo makao makuu ya New Habari, Sinza Dar es Salaam.





KAMPUNI ya New Habari (2006) Limited, imejitokeza kudhamini shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka 2009.Akizungumza leo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya kampuni hiyo, Sinza, Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano, Udhamini na Matukio wa New Habari, Petter Mwendapole alisema udhamini wao utagharimu kiasi cha sh milioni 80.



“Hizi ni fedha ambazo zitahusisha mambo mbalimbali ikiwemo matangazo na promosheni ya shindano lenyewe, hapa tunazungumzia pia mavazi kama Tops, fulana na kofia kwa washiriki na watu mbalimbali,” alisema.



Mwendapole alisema kampuni yao imeamua kudhamini shindano hilo katika kuunga mkono juhudi za kampuni ya Lino International Agency kusaidia kumuwezesha binti wa Tanzania kujitegemea.



Miss Tanzania inadhaminiwa kupitia gazeti la Bingwa ambalo hutoka kila sikuMbali ya hilo amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakisha utalii wa ndani unakuwa na kupitia magazeti yao watasaidia kutangaza vivutio mbalimbali. Katika kuhakikisha shindano hilo linawafikia watu wengi, Mwendapole amesema watakuwa na kurasa maalum kwa ajili ya Miss Tanzania na pia watakuwa na matoleo maalum ya shindano hilo.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na Meneja Huduma kwa wateja wa Vodacom, Elihuruma Ngowi waliipongeza New Habari kwa udhamini wao na kueleza kuwa wana uhakika shindano la mwaka huu litakuwa na nguvu zaidi.

New Habari ni wachapishaji wa magazeti ya Bingwa, Mtanzania, Dimba, The African, Rai, Weekend African na Mtanzania Jumapili..
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, July 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

yote haya yanapatikana ndani ya ZIZZOU FASHIONS STORE

Dukani kwa ZIZZOU FASHIONS STORE
Mambo yetu ya sutizzz

Raba za uhakika na za kila aina kwa ZIZZOU FASHIONS STORE ndio chimbo pekee la kutoka kijanja.
Mashati yenye ubora wa kutosha kabisa,kwa wale wenye kupenda mmechisho wala usisite tia timu leo ndani ya maduka hayo

Ukitaka kutoka kijanja kwa vazi la jeans lenye kiwango na rangi mbalimbali,Kwa ZIZZOU FASHIONS STORE ndiyo sehemu ya majibu yako,kama vipi pitia kwenye maduka yake ya Afrika Sana-Sinza na Victoria-Kijitonyama jijini Dar

Shaving,Manicure,Hair Waves,Scrub,Facial Steaming na mengine kibao yanapatikana ndani ya ZIZZOU BARBERSHOP iliopo Victoria-Kijitonyama jijini Dar.
CONTACT:0774 770077
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, July 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1
Idadi ya watu