Clouds Media Group yapigwa msasa wa masuala ya ukimwi

Tuesday, June 30, 2009

katika semina hiyo,pia kulikuwepo na mgeni mualikwa, dada ambaye ni muathirika wa virusi vya Ukimwi,mkazi wa Tabata Kimanga (pichani) Bi. Dhamiri Mustafa (22) ambaye pia alitoa historia ya maisha yake namna alivyoambukizwa na hadi kujitambua kuwa na virusi vya Ukimwi, na ni jinsi gani anajilinda, na kwa namna gani anavyo pambana na suala la unyanyapaa kutoka kwa jamii inayomzunguka,yeye mwenyewe amekiri kuwa tangu ajitambue kuwa na virusi vya ukimwi yapata miaka kumi amekuwa akiishi navyo mpaka sasa,amekuwa akikumbana na suala unyanyapaa kutoka kwa watu mbalimbali ikiwemo familia yake.
Mtoa mada mkuu wa Semina Bi. Monica Tarimo akitoa maelezo ya kutosha kwa washiriki wa semina hiyo iliyofanyika leo mjengoni Clouds Media Group,Mikocheni jijini Dar.

Washiriki wa semina hiyo wakiwa makini kusikiliza mafunzo kutoka kwa mkufunzi wa semina hiyo.

Baadhi ya vijana wa mjengoni/Clouds Media Group wakiwa ndani ya chumba cha semina leo iliyokuwa ikihusu masuala mazima ya maambukizi UKIMWI/VVU na unyanyapaa kwa wenye virusi vya Ukimwi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 4

tamu ramba kidoogo ai


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 3

KAULI YA FEMACT KUHUSU TAMKO LA SERIKALI JUU YA MJADALA WA UFISADI UNAOHUSU MEREMETA, TANGOLD NA DEEP GREEN FINANCE LTD

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sisi mashirika yanayotetea Usawa wa jinsia, haki za binadamu na maendeleo na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FEMACT)na mtandao wa mashirika yanayotetea haki za binadamu kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (SAHRINGON) tumeshangazwa na kauli iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samwel Sitta na Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda kwamba tuhuma za ufisadi na/au wizi mkubwa wa fedha za umma unaoyahusu makampuni ya Meremeta Ltd., Tangold Ltd. na Deep Green Finance Co. Ltd. haziwezi kuzungumziwa ndani ya Bunge la Jamhuri kwa sababu tuhuma hizo zinahusu mambo ya jeshi na/au usalama wa taifa.
Aidha tunapenda kuweka msimamo wetu wazi kwamba hatukubaliani na kauli na/au msimamo huo wa Spika wa Bunge na Serikali kwa sababu zifuatazo:
Kwanza hatuamini kwamba ufisadi mkubwa unaotuhumiwa kufanywa kwa kutumia kivuli cha makampuni haya una uhusiano wowote na mambo ya jeshi na/au usalama wa taifa. Taarifa zilizoko hadharani zinaonyesha kwamba Meremeta Ltd. na Tangold Ltd. ni au yalikuwa makampuni ya kigeni na wala sio ya Kitanzania.
Taarifa hizo zinaonyesha kwamba wakati Meremeta Ltd. iliandikishwa nchini Uingereza mnamo tarehe 19 Agosti 1997 na kufilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006, Tangold Ltd. iliandikishwa nchini Mauritius mnamo tarehe 8 Aprili 2005 na kupewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20 Februari 2006.
Zaidi ya hayo makampuni hayo yalianzishwa na kuendeshwa kama makampuni binafsi ijapokuwa inaelezwa kwamba Serikali ya Tanzania kwa kupitia Hazina ilikuwa na hisa katika kampuni ya Meremeta Ltd.
Hakuna hata moja katika makampuni haya mawili ambayo imewahi kuwekwa katika orodha ya makampuni na/au mashirika ya umma na wala hesabu zake kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kama ilivyo sheria kuhusu hesabu ya fedha za umma.
Aidha Meremeta Ltd. kwa kipindi chote cha uhai wake iliendeshwa na wamiliki wa kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini iliyokuwa na hisa 50 katika Meremeta wakati Serikali ya Tanzania ikiwa na hisa nyingine 50 na makampuni mawili ya Kiingereza yakiwa na hisa moja kila kampuni. Msimamo wa Spika Sitta na Serikali una walakini mkubwa kwa sababu unaweza kutafsiriwa kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Idara ya Usalama wa Taifa ni kichaka cha kufichia ufisadi na wizi wa mali ya umma.
Kuhusiana na kampuni ya Deep Green Finance Co. Ltd., nyaraka zilizoko hadharani zinaonyesha kwamba Deep Green Finance iliandikishwa mnamo tarehe 18 Machi 2004 kwa madhumuni ya, pamoja na mengine, kufanya biashara ya wakopeshaji fedha.
Licha ya kutokuwepo kwa ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba Deep Green Finance iliwahi kufanya biashara yoyote na Serikali ya Tanzania, katika kipindi cha miezi minne tu kati ya tarehe 1 Agosti na 10 Desemba 2005, Benki Kuu ya Tanzania ililipa jumla ya shilingi 10,484,005.39 katika akaunti ya Deep Green Finance iliyokuwa NBC Corporate Branch, Dar es Salaam.
Aidha, kuanzia tarehe 11 Desemba 2005 hakuna fedha yoyote iliyoingizwa katika akaunti hiyo hadi tarehe 27 Februari 2007 kampuni hiyo ilipovunjwa ‘kwa hiari’ ya wanahisa wake. Inasemekana kuwa jumla ya fedha bilioni 155 ziliibiwa kupitia makampuni hayo.
Kwa miaka mingi kumekuwa na taarifa za utatanishi kuhusu umiliki wa makampuni haya. Kwa mfano, Serikali imekuwa ikitoa taarifa kwamba Meremeta Ltd. ilikuwa ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya mradi wake wa magari ya deraya ya Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006. Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005 inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi tarehe 3 Oktoba, 1997.
Taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd. zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini, hisa 50 nyingine zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha wakati makampuni mawili ya Kiingereza – London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. - yalikuwa yanamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd.
Kwa mgawanyo huu wa hisa za Meremeta Ltd., ni wazi kwamba makampuni binafsi ya kigeni yalikuwa yanamiliki sehemu kubwa zaidi ya hisa za kampuni hiyo.
Bunge limepewa wajibu wa kusimamia Serikali na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, 1977. Namna pekee ya Bunge kutekeleza wajibu wake wa kikatiba ni kutumia fursa ya wabunge kuuliza maswali kwa mawaziri na vile vile kwa kuunda Kamati Teule za Uchunguzi au kutumia Kamati za Kawaida za Bunge kuchunguza masuala mbali mbali yanayohusu uendeshaji wa Serikali.
Masuala yanayohusu makampuni ya Meremeta Ltd., Tangold Ltd. na Deep Green Finance Co. Ltd. yamejadiliwa sana na Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali tangu mwaka 2007. Kwa muda wote huu, Serikali ya Tanzania haijawahi kuzikanusha rasmi tuhuma za ufisadi zinazoyahusu makampuni haya. Kauli za Spika Sitta na Waziri Mkuu Pinda zinadhihirisha kwamba matumaini hayo ya Serikali hayajafanikiwa.
Msimamo wao wa sasa ni dhahiri unalenga kutumia kivuli cha usalama wa taifa au jeshi ili kuzima mjadala huu ndani na nje ya Bunge. Iwapo watafanikiwa kwenye jambo hilo hapana shaka kwamba watatumia kivuli hicho hicho kuzima mijadala mingine ndani na nje ya Bunge na uwezo wa Bunge wa kusimamia Serikali na uhuru wetu wa kushiriki katika mijadala inayohusu masuala mbali mbali muhimu kwa wananchi utafifishwa.
Ni dhahiri kuwa upotevu wa fedha bilioni 155 kupiti makampuni hewa ya Meremeta, Tangoald na Deep Green umeongeza kufukarishwa kwa wananchi walio wengi katika nchi yetu. Fedha hizo zingetosha:
•kujenga visima vya maji safi elfu kumi na tano (15,000) kwa thamani ya shilingi milion kumi (10 milioni) kila kimoja. Nchi yetu ina vijiji visivyozidi elfu kumi na mmoja. Kwa maana hiyo kila kijiji kingepata karibu visima viwili;
•Fedha hizi zinaweza kusomesha zingewezesha watoto zaidi la laki tano (500,000) kusoma bure shule za sekondari kwa gharama ya shilingi laki tatu kila mmoja;
•Kujenga zahanati 1,550 kwa gharama ya shilingi milioni mia moja kila zahanati. Kwa maana hiyo vijiji 1,550 hapa nchini vingepata zahanati;
•Fedha hizo zingeweza kutoa motisha kwa kulipa madaktari na watoa huduma katika sekta ya afya ili waweze kuwahudumia vizuri wagonjwa na hivyo kupunguza vifo visivyo vya lazima. Kwa mfano fedha hizo zingetosha kuajiri madaktari 6,458 kwa mwaka na kuweza kuwalipa shilingi milioni mbili kwa mwezi kila mmoja;
•Kadhalika fedha hizo zingeweza kujenga madarasa 17,222 kila moja kwa gharama ya shilingi milioni tisa. (9,000); au
•Kuajiri wauguzi 12,917 kwa mwaka na kila mmoja akiwa analipwa shilingi milioni mmoja (1,000,000) kwa mwezi
Kwa vile inaelekea Serikali haijawa tayari kuchukua hatua dhidi ya waliohusika na ufisadi uliofanywa kwa kutumia makampuni ya Meremeta Ltd., Tangold Ltd. na Deep Green Finance, tunadai mambo yafuatayo :
i.Bunge la Jamhuri liunde Kamati Teule ya Uchunguzi wa makampuni haya kama lilivyofanya kuhusiana na Kashfa ya Richmond;
ii.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano atumie uhuru na mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 kufanya uchunguzi maalumu (special audit) ya taarifa za fedha na/au mahesabu ya makampuni ya Meremeta Ltd., Tangold Ltd. na Deep Green Finance kwa nia ya kuhakikisha kwamba fedha zote zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa makampuni hayo ziliidhinishwa kisheria na kwamba zilitumiwa kwa ajili ya shughuli iliyoidhinishwa kwa mujibu wa sheria;
iii.Watakaogundulika kuhusika na kashfa hii ya fedha za umma wachukuliwe hatua zinazostahili; kisheria na kinidhamuiv.Waziri Mkuu Mizengo Pinda achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kupotosha bunge juu ya umiliki wa meremeta
v.Tunawahimiza wanachi wote wa Tanzania wadai uwajibikaji wa wabunge wao na serikali yao kwa ujumla kuhusiana na wizi/ufisadi uliyofanywa na makampuni ya Meremeta, Tangoald na Deep green kwa sababu ni wizi mkubwa unaochangia kwa kiasi kikubwa wananchi wengi kuwa na maisha magumu hivi sasa
Imetolewa na FemAct na kusainiwa na
1.Tanzania Gender Networking Programme (TGNP)
2.Legal and Human Rights Centre (LHRC)
3.Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA)
4.Youth Action Volunteers (YAV)
5.The Leadership Forum (TLF)
6.Coast Youth Vision Association (CYVA)
7.Walio Katika Mapambano na AIDS Tanzania (WAMATA)
8.Tanzania Media Women’s Association (TAMWA)
9.Youth Partnership Countrywide (YPC)
10.Tanzania Human Rights Fountain (TAHURIFO).
11.HakiArdhi
12.Women in Law and Development in Africa (WILDAF
13.Women Legal Aid Centre (WLAC)
14.Lawyers’ Environmental Action Team (LEAT)
15.Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG)
16.Life Skills Association (LISA)
17.Women Fighting Against Aids in Tanzania Trust Fund (WOFATA)18.Taaluma Women Group (TWG)19.Marcus Garvey Foundation (MGF)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

MISSA YA KUMSALIA MAMA YETU MPENZI MAREHEMU MAMA MARGARET KUMBUKA---LONDON UNITED KINGDOM

Marehemu Mama Margareth Kumbuka
KWA NIABA YA KHALID, ARAFA NA MAHADIA KUMBUKA, TUNAPENDA KUTANGULIZA SHUKURANI ZA DHATI KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WOTE AMBAO TULIOSHIRIKIANA NAO TOKA MWANZO HADI MWISHO WA MSIBA WA MAREHEMU MAMA.PIA TUNAWATAARIFU KUWA KUTAKUWA NA MISA MAALUM YA KISWAHILI YA KUMUOMBEA MAREHEMU MAMA MARGARET KUMBUKA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 5TH JULY 2009 LONDON UNITED KINGDOM KUANZIA SAA NANE MCHANA (2.00 PM) HADI SAA KUMI JIONI (4.00 PM) KATIKA KANISA LA ST. AGNES/MARGARET CHURCH,OPPOSITE #2 GRESHAM ST, EC2V 7QP,LONDON FOR MORE INFO CONTACT 07886897813, 07951503042 0R 07852289892
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Haya yote yanapatikana ndani ya duka la Manywele

Maimatha akionesha manywele ya ukweli yaliopo dukani kwake
Zipo za aina mbalimbali


Kofiazz,mikanda,vipodozi,mikoba na mengineyo ndani ya duka la Manywele

Maimatha wa Jesse akiweka sawa bidhaa zake ndani ya duka lake lililopo Kinondoni kwa manyanya,jijini Dar

Hereni,mikufu aina mbalimbali
Hizi pia zinapatikana ndani ya duka la Manywele
Maimatha akionesha nanihii kwa ajili ya kupunguza unene na kuwa slim,hata zile nanihiii za kuongeza hips,zinapatikana ndani ya duka la Manywele linalomilikiwa na mwanadada na mtangazaji mahiri wa kipindi cha afro beat kupitia chanel 5 alias EATV.Kwa mahitaji mengine ya urembo na ulimbwende basi wasiliana naye kwa namba yake ya kiganjani 0714 080880
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 7

ziara ya tamasha la WaPi - kuanza kurindima mikoani


Habari zenu ndugu jamaa na marafiki wa WaPi.


Tunayo furaha kuwasiliana nanyi tena na kukumbushana kinachoendelea kuhusiana na Tamasha letu WaPi.Wapi imebadilisha mfumo wake na kwenye awamu hii itafanyika kila baada ya miezi mitatu.


Tutakuwa na WaPi Mikoani kabla ya ya ile WaPi kubwa ya Dar. Kutakuwepo na ziara za mashuleni na vyuoni kipindi hicho cha miezi miwili kabla ya WaPi ya kuu.


Yajayo WaPi mkoani itafanyika Iringa tarehe 11-07-2009 Mada ya mkoani itakuwa WAPI MKoa?!


Kwa mara ya kwanza wasanii na wadau wa sanaa watafaidika na fursa hii ya kujumuika kwenye tamasha hili la WaPi mkoani. tayari tuna udhamini wa Eboni Fm, tunatarajia watu wengi kuwepo siku hiyo.
Wataarifu wengine tuifanikishe WaPi mkoani kwa dhati Ziara ya mashuleni Itakuwa tarehe 19-07-2009 Tutatembelea mashuleni ili kutoa fursa kwa wanafunzi kujumuika na kujiandaa kushiriki kwenye Tamasha kuu la Wapi Dar.
Vipaji mbali mbali vitaibuliwa na warsha kufanyika. WaPi Dar itakuwa tarehe 25-07-2009 Baada ya ukimya wa miezi 3 WaPi Dar itatujumuisha tena kwa kishindo kikubwa na mada yetu mara hii ni Mchango wa sanaa kwenye janga.
Hii imepelekewa na maafa mbali mbali yaliyojitokeza nchini na kwengine duniani haswa udhalilishwaji wa jamii ya mazeruzeru na milipuko ya mabomu Mbagala Dar. Tunaangalia jinsi invyotumika kwenye jamii wakati wa majanga.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

litakuwa mitaani wiki hii

Lile gazeti letu mahiri la nyewz tam tam za soka litakuwa sokoni ndani ya wiki hii,Kama utakuwa unahitaji kupata copy yako mapema tafadhali tuma txt/email kwenda kwa mdau mwenzetu kwenye 0713350833/Shaffih Dauda [shadaka20@yahoo.com] Pia kama unataka kuletewa ofisini kwako kumbuka kutoa physical address yako na namba ya simu then litakufikia popote pale ulipo hata kama upo mkoa. I hope wadau wa Mbeya, Moshi & Arusha mmetupata kupitia hapa.

Naomba kuwasilisha!!!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Ras Makunja kumfukuza "Kizabi zabina" na mbwa domo baya!


Kiongozi wa bendi ya The Ngoma Africa aka FFU, Ebrahim Makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu",juzi juzi amewaacha hoi mainjinia katika studio huko ujerumani baada ya kutinga na mbwa studio humo na kumshirikisha mbwa huyo aina ya "Domo Baya" katika kurekodi sauti!


Mmbwa huyo alibwaka sana na kurekodiwa vizuri! katika kuchangia wimbo wa "Kizabi Zabina"! Mzee Pazi! si mtu mwema!Wadaku wametonya kuwa hatua ya kumpeleka mbwa huyo studio,ilichukuliwa kwa hasira na Ras Makunja, baada ya mwanamziki huyo kumpokea ujumbe wa simu ya kiganjani kutoka kwa mtu asiyejulikana,ujumbe huo ulimuonya Ras Makunja kuwa aachane na wimbo huo,hapo kamanda wa kikosi cha Ngoma Africa au FFU,uzalendo ulimshinda akamua kukodisha mbwa aina ya Domo Baya,na kwenda naye studio kuzidisha vitisho!


Baadhi ya wanamziki wake walimsihi kuwa "Ras hapo huoni kuwa unamtishia mbwa kizabi zabina "Mzee Pazi"! Ras Makunja nae alilamika kuwa mbona yeye ananitishia maisha kwa ujumbe wa simu!?.Linaelekea song hilo lenye kutangaziana bifu katika Ras makunja na "Kizabi zabina! Mzee Pazi" linaingia sura mpya kabla alijatolewa hadharani!



Ngoma Africa wamesema Jamii ndio itakayo amua nani ?mchokozi kati ya Kizabi zabina na mtunzi wa nyimbo hiyo Ras Makunja,ambaye naye mara nyingi analalamikiwa kuwa mchokozi, lakini katika hili jamii ndiyo itakayo toa uhamuzi!.Ras Makunja anamkoromea "Kizabi zabina" Mzee pazi na kumwambia atakapokaribia nyumbani basi ajue atafukuzishwa na mbwa "Domo Baya"
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 2

why not Kigamboni?

Hii ni Bay Bridge maeneo ya Yokohama Port. chini meli zinapita kama zinalia, why not Kigamboni?

Picha kwa hisani ya braza Willy wa Wil'na International aliyeko Japan

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, June 30, 2009 | | Permalink | Maoni 3

mdau anaomba mijadala hii mitatu ijadiliwe hapa jamvini

Monday, June 29, 2009

Picha kutoka maktaba ya Jiachie;Hii ilipigwa mchana barabara ya Old Bagamoyo.

Habari yako michuzi?


Mimi naomba tujadiliane mambo yafuatayo na wadau wengine.
Kwanza kuhusu swala la foleni hapa jijini kwetu,mimi kwa maoni yangu baada ya miaka mitatu foleni zitakuwa almost masaa 12 yote ya mchana na pia kuna sehemu ndio itakuwa balaa sasa.


Mimi nadhani mikopo kwa wafanyakazi iongezwe riba na kila ofisi ijitahidi kuwa na mabasi ya ofisi hata kama ni ya kukodi ila wafanyakazi wake wasihangaike na pia ushuru wa magari bandarini ungeongezwa maradufu, maana sasa huko tunapokwenda sijui itakuwaje na pia hii iwe fundisho kwa serikali zetu kuplan miji sio kujengajenga.


Maana kama dar ingekuwa well planned siamini jinsi ilivyokuwa kubwa kama kungekuwa na foleni hata kidogo.Na pili nataka kujua wadau hivi mbona siku hizi kuna blog kibao na nyingine toka ilipofunguliwa ina kurasa moja tu sasa sijui watu wanaanzisha kitu ambacho hawakijui au ni aje??


Hili nalo lingefanyiwa kazi maana mambo ya utamu yanaweza kujirudia siku moja.Tatu na mwisho hivi kama mtu anakunywa pombe yeyote kama bia au Grants lakini sio mbichi (za kienyeji) hivi pombe zinamaliza pesa? na kama unakunywa weekend tu zinaweza kupunguza ufanisi wa kazi?


Asanteni wadau

Nnaombeni tujadiliane
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 29, 2009 | | Permalink | Maoni 2

ni sawa kumcheka mwenzio kwa vile amefulia ?

Wasanii mahiri wa Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhuvile a.k.a Joti na mwenzake Mjuni Silvester ‘Mpoki’ wameelezewa kuwa katika historia ya maisha yao waliwahi kufulia na kwamba wangekuwa na kumbukumbu nzuri wasingethubutu kuwadhihaki wenzao ambao kwa sasa maisha yao yametetereka.


kuna mdau kaleta haka kamjadala ka "KUFULIA" hapa Jamvini, anauliza hivii,Je,! suala la kumcheka na kumkebehi binadamu mwenzio tu ati kwa sababu "amefulia" ni SAWA.?je inaleta maana kweli ?!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 29, 2009 | | Permalink | Maoni 18

SUMMER FAMILY FUN DAY & BARBEQUE IN MILTON KEYNES

SUMMER FAMILY FUN DAY & BARBEQUE IN MILTON KEYNES, ON SATURDAY 11th July from 3:30pm to 11pm at CONNIBURROW PAVILLION,MILTON KEYNES,MK14 7AJ..Triple J'S Bring to you the best music varieties,family games,Along with BBQ (Nyama Choma) & Other foods. Entries £5 adults, Children Free. Food prices will start from £1, For more information please contact 07717624731 or 07946510798..

Thanks In Advance

Mdau
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ffu kuitikisa Goeppingen City,Germany jalai 4


The Ngoma Africa Band aka FFU!na mdundo wao wa "Bongo Dansi" wanatarajiwa kutingisha jukwaa lingine katika onyesho kubwa la Afrika Festival litakalo fanyika mijini Goeppingen,Ujerumani siku ya jumamosi ya 4 Julai 2009 saa 2.00 Usiku.


Bendi hiyo maarufu na dansi lake linalowatia kiwewe washabiki huko ughaibuni, wanasubiliwa kwa hamu na washabiki katika onyesho hilo.Wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica pia unaweza kuwasiliana kwa kupitia.ngoma4u@googlemail.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

mdau anaomba msaada wa jibu


Hii Picha nilipiga wakati Huyu Jamaa amelala? then akaishitukia Deal baada ya flash kuwaka. Swali. Kwa nini mtu akiwa amelala ukimpiga Picha anakua na sura tofauti na akiwa macho ?
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, June 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

wana wa kushoo love jamvini walikuwepo pia

Sunday, June 28, 2009
Mtangazaji wa kituo cha redio ya Times Fm ya hapa jijini dar,Tayanah Tibenda a.k.a Mis Tz akiwa amepozi mbele ya kamera ya jiachie huku akismile safi kabisa
Walimbwende hawa nao wakasema aakhuu ! na sie tutoe tulikuwepo
Msanii wa muziki wa bongofleva Q-Chila (kati) na washkaji zake wa magomeni a.k.a migo migo walikuwepo kumcheki Beenie Man.
Washkaji mbalimbali waliamua kutoa hii kwa wanajamvini wengine ambao hawakupata bahati ya kulishuhudia onyesho la Beenie Man usiku wa kumkia leo hapa jijini dar.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, June 28, 2009 | | Permalink | Maoni 1

vibwanga vilivyojiri kimtindo shoo ya Beenie Man usiku wa kuamkia leo

Hatimaye akaibuka nayo mwenye nguvu "Kidume",huyo anayeiweka sawa hiyo tai mara baada ya kuwashinda wote,ebwanaa jamaa limetanuka ile mbaya so ni haki yake kuinyaka,ilivyokuwa ngumu hiyo tai hata nusu kipande hakuichanika.
Ukishangaa ya mussa utayaona ya filauni,unajua nini hii mijamaa yote hii ilikuwa inagombania tai ya shingoni aliyokuwa amevaa mtu mzima Beenie Man,si ndiyo ikaleta sheshe ati kila mmoja anaitaka,hebu angalia wanavyoigombania.Mwanajamvini wewe unalionaje hili ?
Huyu naye alikuwa anazingua zingua watazamaji wengine,wakataka kumshushia zile za buuu baaa,mtuu chaaliii kama uonavyo pichani.lakini jamaa wa usalama walimuwahi kumdaka na kumuweka kati asiendelee kuleta songo mbingo.
Kama kawaida kwenye mkusanyiko watu wengi hakukosi vijitabia,huyu jamaa pichani alichomoa pete kubwa ya Beenie Man mara alipompa mkono kama kumsalimia hivi,si ndiyo jamaa baada ya kumvua ile pete akawa anataka kusepa nayo,Beenie Man akawa analalama jukwaani "nirudishie pete yangu,nirudishie pete yangu tafadhali" mara wakatokea mabaunsa (pichani) na kumbana na hatimaye kuirejesha ile pete.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, June 28, 2009 | | Permalink | Maoni 4

Beenie Man alivyokamua usiku wa kuamkia leo

Ilikuwa ni full kujiachia kwa nafasi huku mikono ikiwa hewani
Washabiki wa Beenie Man wakiwa bize kurekodi kama si sauti basi kideo chake.

Beenie Man akiimba pamoja na mashabiki wake

Ahhh! Bongo dai salamaa.! Akina dada taratiiibu kimtindo na kwa hisia.
Beenie Man akiimba wimbo wa hayati Bob Marley kwa hisia huku umati wa watu ukishangilia kwa mayowe na miluzi.
Beenie Man akijiachia kwa mauno laini mbele ya umati mkubwa uliofika kumshuhudia mkali huyo wa miondoko ya dance hall.
Beenie Man kwa mauno naye kumbe yumo ile mbaya,masistaa duu walikuwa haiwaishi kushangilia na kupiga mayowe ya hapa na pale kila wakati,jamaa alipojipinda.
Mashabiki wakiwa wamepagawa vilivyo na makamuzi ya Beenie Man jukwaani.Beenie Man akiwasalimia watazamaji waliofika kumshuhudia kwenye onyesho lake lililofanyika usiku wa kuamkia leo hapa jijini Dar.
Mfalme wa miondoko ya dance hall kutoka nchini Jamaica Beenie Man akijiandaa kupanda jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye onesho lake moja tu
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, June 28, 2009 | | Permalink | Maoni 3

yaliyojiri usiku wa kuamkia leo kwenye onesho la beenie Man

Masista duuu kibao walikuwepo na wala hawakujivunga kujiachia huku wakinesa nesa na miili yao kiulainiii,si unajua mambo ya dance hall tena.


Msanii mwingine kutoka Uganda alikuwepo kumpa tafu Beenie Man usiku wa kuamkia leo.
Albert Mangwea a.k.a Mimi naye alikuwepo kuonyesha umahiri wake wa kufloo mitindo huru mbele ya hadhara kubwa uwanjani hapi.
TID alimaliza sehemu ya shoo yake,akamuacha shabiki wake akiwa ameduwaa jukwaani kama umuonavyo pichani hata hofu hana, mbele ya umati mkubwa uliofika uwanjani hapo
TID akijiachia na shabiki wake vilivyo jukwaani
TID akiimba wimbo wake mpya wa Asha na shabiki wake aliyeamua kumpa tafu kwa namna ya pekee kabisa iliyowavutia watazamaji, msanii huyo mwenye swaga nyingi awapo jukwaani.
T.I.D akionesha umahiri wake wa kuyakata mangoma kama ya The Wacko Jacko,hii inadhihirisha wazi hayati Michael Jakson aliwainspire wasanii wengi hapa uliwenguni.
Umati wa watu ukishangweka vilivyo huku mikono ikiwa hewani.
Pichani baadhi ya mashabiki wakiendelea kupata raha ya wasanii waalikwa wa hapa nyumbani, wanaume TMK Family wakiongozwa na mh Themba.

Usiku wa kuamkia leo yule mkali na mfalme wa miondoko ya dance hall Beenie Man alifanya onyesho lake moja tu na kufanikiwa kuzikonga nyoyo za washabiki wake vilivyo katika viwanja vya chuo cha posta,sayansi kijitonyama jijini dar.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, June 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu