ati mkubwa fella fisadi wa bongofleva.?.!

Friday, January 30, 2009
Y-Dash akizungumza kwa hisia na uchungu mkubwa kuhusiana na tuhuma kubwa wanazomtupia Mkubwa Meneja Fella kwamba amewanyonya vya kutosha na sasa kilichobaki ni zamu yake kuwalipa kila alichowanyonya kwa kufuata sheria
Wasanii wa kundi la TMK UNITY linaloongozwa na Jebby (kulia pichani) wakifanya mahojiano yao leo mchana na kipindi cha XXL kinachotangazwa na B 12 kupitia redio ya Clouds, mara baada ya kujiengua kutoka kundi la TMK wanaume Family ambalo liko chini ya Mkubwa Said Fella.Wasanii hao ambao wamemtupia lundo la lawama na hata kuthubutu kumuita FISADI wa muziki wa bongofleva meneja huyo ,wakati huo wakiwa ndani ya kundi la WanaumeTMK Family kuwa amewazulumu pesa nyingi kiasi cha kuwafanya wasiendeleze maisha yao vizuri.Kundi hilo la TMK UNITY linaundwa na wasanii watatu ambo ni Y-Dash,Y-P na Jebby wakiwa na meneja wao mpya Abdalah Issa (mwenye kofia ya kaki pichani).
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, January 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

full mabodizz

KATIKA ENZI ZA UJANA TUKIJALIBU KUKAZA MIILI NI MSHAM,MANGILILE KILAMBO,JUMA,GASTO,SEBA,JORAM NA WAWILI MAJINA YAMENITOKA KATIKA GYM MAHARUFU NYUMBANI KWA SEBA ILALA.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, January 30, 2009 | | Permalink | Maoni 1

kp leo

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, January 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

MWANAFUNZI ALIEYETOWEKA NYUMBANI KWAO TANGA AMEPATIKANA DAR



Ndugu zangu katika jamii, Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, familia ya mtoto Mbarouk H. Massoud ambaye alitoweka nyumbani kwao huko Mikanjuni, Tanga tokea jumatatu 26/1/2009 bila taarifa yoyote, inayo furaha ya kuwajulisha kuwa mtoto wetu amepatikana huko Dar jana alhamisi 29/1/2009 akiwa salama.


Bado hatujajua sababu za mtoto wetu kuondoka bila kuaga na hilo tunalifanyia kazi kifamilia. Tunashukuru kwa msaada mkubwa tulioupata kutoka kwa ndugu,wadau, marafiki,jamaa na taasisi mbalimbali walioshiriki katika kumtafuta mtoto wetu bila kuchoka hadi alipopatikana.
Kwa ujumla wenu nyote tunawashukuru na kuwatakia mafanikio makubwa katika maisha yenu ya kila siku. Shukrani za pekee kwa wanablog na vyombo vya habari vifuatavyo:
Issa Michuzi
Maggid Mjengwa
Michuzi Jr
Haki Ngowi
Tanga TV ITV
Mwambao Radio


Asanteni sana.
Massoud Hamim,
Mzazi wa Mbarouk
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, January 30, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ukiwahitaji

Thursday, January 29, 2009



Pichani ni kikundi cha matarumbete,ukiwahitaji Katika shughuli zako za matarumbeta kwenye mambo ya harusi,send off,kipaimara na mambo mengine yahusianayo na hilo wasiliana na Bw.Ismail Maneno kwa namba 0713 449852 ambae ndiye kiongozi mkuu wa kundi hilo la SUMA GROUP
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

papo kwa papo ya waziri mkuu leo

Habari za kazi wanamtandao wenzangu.

Leo napenda kuwaarifu wasomaji wa website na blog zetu kwamba maswali yaliyokuwa yakiulizwa kwa waziri mkuu ya papo kwa hapo toka kwa wabunge na majibu yake leo yanapatikana katika website yetu www.dullonet.com.

Wasomaji wanaweza kusikiliza kwa utulivu zaidi.

Dullonet Daima.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kp leo

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 2

Blogu Ya Profesa Matondo

Wapendwa wanablogu;Kwa heshima kubwa na taadhima tele nabisha hodi tena kwenu mliotangulia. Naomba mnifungulie mlango na kunikaribisha tena. Safari hii nakuja na blogu ya kuchangamsha fikra na uchambuzi. Blogu hiyo inapatikana hapa www.matondo.blogspot.com
Natanguliza shukrani zangu kwani najua mmeshanikaribisha.
Wenu;
Dr. Masangu Matondo Nzuzullima

Chuo Kikuu cha Florida



"Baadhi ya sura hapa ni za manabii wetu wa kweli waliotukomboa (au wanaopigania kutukomboa) kutoka "Misri" yetu ya umasikini, magonjwa, dhuluma na kutuahidi kutupeleka katika nchi ya ahadi. Mbona safari yetu inaonekana kama vile imekwama?"
kwa habari zaidi ingia www.matondo.blogspot.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

Ujumbe kwa wadau wote wa FotoBaraza.Net


Nakushukuru sana kwa muda wako uliochukua na kumchagua mwanakijiji mwezetu Ritha Tabaro, almaarufu kama RT, kutuwakilisha katika ofa yetu ya kwanza tuliyopatiwa na mhisani wetu mkuu wa kijiji, ya kuhudhuria kwenye Usikuwa wa Chakula cha Mwafrika pale Mwanzo Park Lodges, Mkuranga, Dar es Salaam.

Mwanzo Park Lodges ndie mhisani wa kwanza kabisa na wa pekee wa kijiji chetu. Mhisani huyu ndiye anayetuwezesha kuwa hewani kwa kulipia gharama zetu za internet za kila mwezi tangu kuanza kwa mwezi huu, na ametuhakikishia uhakika wa kulipia huduma hiyo kwa muda wa miezi mitatu. Tunamshukuru sana.

Napenda pia kuchukua nafasi hii kumpongeza mwakilishi wetu, RT. Napenda ifahamike kuwa huyu ni mwakilishi na si mshindi, kwa sababu hakushindania nafasi ile bali alipendekezwa. Hongera RT.

Tuzidi kushirikiana katika kila linalojiri humu kijijini. Nawaomba pia tupunguze masihara kidogo kwenye masuala ya kimaendeleo kama ya jambo hili, maana kuna baadhi yetu tulikuwa tukipendekeza kimasihara kidogo kwenye mjadala ule japo tulikuwa tukifahamu maelekezo yote.

Nawashukuru pia walioona dosari za tarehe za shughuli hii, niliandika 2008 badala ya 2009. Nakushukuru Lucie, Dismas, na msaidizi wangu mkuu Michuzi Jr. kwa kuliona hilo mapema na kunistua. Unajua tena vidole bado vilikuwa vimelewa 2008.

Basi tuzidi kutakiana heri kwa mwaka huu wa 2009 kwani umeanza vyema.

Wale wanakijiji wa Dar es Salaam, tunawakumbusha tena kwamba kikao cha mwisho cha ukusanyaji wa michango ya shilingi elfu 10 kwa kila mmoja kwa ajili ya pati la kukaribisha mwaka 2009 kitakuwa Jumapili hii, 1/2/2009 pale Chaga Byte, Makumbusho na tarehe 7/2/2009 ndio pati lenyewe pale Soma Mgahawa wa Vitabu.

Tuko kwenye mchakato mkubwa wa kuona namna ya kuwawezesha walioko mikoani na ughaibuni kuweza kuendesha vijishughuli kama hivi. Hatujawatenga jamani, tuko pamoja sana.

Mtumishi wako,
Babukadja Sankofa
+255 713 223 345

Nenda FotoBaraza.Net katika: http://fotobaraza.ning.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

MBAROUK MASSOUD AMETOWEKA NYUMBANI


Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Mkwakwani, Tanga MBAROUK MASSOUD ametoweka nyumbani kwao huko Mikanjuni, Tanga tokea jumatatu tarehe 26/1/2009na hajulikani alipo mpaka wakati huu na kusababisha huzuni na simanzi kubwa kwenye familia yake.

Jitihada za kumtafuta sehemu mbalimbali hazijazaa matunda hadi sasa, hivyo tunaomba msaada kwa yeyote atakaypata taarifa za kijana huyu awasiliane nasi kwenye namba za simu zifuatazo:

1. 0717 998 082 - Mrs.Massoud
2. +1 614 584 2321 Mr. H massoud( massoudhmj@hotmail.com)
3. 0754 336 128 Abdallah Massoud - Baba Mdogo
4. 0732 302 591 Moh'd Massoud - Baba dogo
5. 0713 770 191 Halima Abdallah - Mama mdogo
6.0713 475 155 WP Mwanaidi - Mama mdogo wa Iringa
7.0774 600 700 Uncle Kimolo wa Arusha
8.0715 260 377 Uncle Arch
9.0754 378 519 Uncle Japhet Makau
10. 0714 648 666 Muddy Massoud - Kaka wa Mbarouk
11. Mkuu wa shule Mkwakwani -0784 947 284

Pia taarifa inaweza kutolewa katika kituo chochote cha polisi ambacho kipo karibu.
Familia inatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano utakaotolewa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ndege huyu na ujenzi wa nyumba yake


Ndege huyu,lakini ana juhudi kubwa ya ujenzi wa nyumba yake,tena anaijenga vizuri ipendeze ili hata wakati wa mvua nae apate pa kujisitiri mahali pazuri,Vipi kwa sisi wakazi ambao tunaishi mabondeni tumejizatiti vipi na mvua hizi zinazonyesha kila mara,nasema hivi inawezekana baadhi yetu tumejisahau kuzikarabati nyumba zetu hasa kutokana na kipindi kirefu cha jua,tunakumbusha tu wadau
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

The Ngoma Africa Band,Kupeleka "mzimu wa Dansi" Finland!


Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" inatarajiwa
kuwadatisha washabiki wa mziki katika onyesho kubwa la "Fest Africa" litakalo fanyika mjini Tampere,Finland siku ya tarehe 7 February 2009,katika ukumbi wa Klubi,
Bendi hiyo inayoongozwa na mwanamziki mashuhuri Ebrahim Makunja aka Ras Makunja
"Bw.Kichwa Ngumu" yenye makao yake nchi ujerumani,hitaupeleka "mzimu wa
dansi la bongo" huko Ufini,Ngoma Africa ni maarufu kwa tabia za kuwadatisha hakili washabiki kwa kutumia mdundo wao "Bongo Dansi".

Bendi hiyo ambayo imetajwa katika maonyesho mengi ya kimataifa kuwa ni bendi bora
kutokana na tabia zake za kuwaridhisha washabiki kwa kuwapa burudani ya kufa mtu!
Kikosi hiko cha Ngoma Africa kinatarajiwa kuruka kuelekea Tampere,Finland bila ya
kuchelewa kwa hajili ya Onyesho hilo .

Ngoma Africa ambayo pia imepachikwa majina mengi ya kiusanii na washabiki kutokana na tungo zao!pia mdundo wake! ambao mara nyingi unawapeleka mchakamchaka washabiki! majina kama FFU,wazee wa kuziwia rushwa,watoto wa uswahilini n.k hayakwepeki kwa bendi.

Bendi hiyo pia inataraji la "The Golden Voice of East Africa".
Ngoma Africa kwa mara ya kwanza kutumbuiza nchini Finland,na watarajiwa kukonga
nyoyo za washabiki wote wa kimataifa katika mji wa Tampere.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 29, 2009 | | Permalink | Maoni 1

tigo yakabidhi madawati shule ya msingi yona

Wednesday, January 28, 2009

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia), akikabidhi madawati
24 kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Upendo Elizabeth Yona yenye
thamani ya shs milioni 3 yaliyotolewa na Tigo kwa ajili ya shule hiyo,
iliyopo Kongowe, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.
Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa sule hiyo, Maureen Chiwela.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, January 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

zavara asaka pesa


Kwa mara nyingine Zavara, mlokuwa mkimtambua kama Rhymson mwasisi wa Kwanza Unit na fani ya hiphop hapa nchini na Afrika ya mashariki. Anayo furaha kuwakilisha wimbo mpya kabisa uliopakuliwa toka studio ya Sabatatu iliyopo Iringa. Wimbo unaitwa Saka pesa umetayarishwa na Zavara (zamani Rhymson wa Kwanza Unit) na kufanyiwa mixing na mastering na mtaalamu Ozzey.

Natarajia ushirikiano wenu kuendeleza fani hii. Nakaribisha maoni yenu, maswali na nasaha. Isambaze kwa vichwa wote
Pamoja

Ra
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, January 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

inspekta haroun kuzindua ndoa haina doa februari


Mwanamuziki matata wa bongofleva anayetambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun a.k.a Babu hivi karibuni aliibuka na singo yake ya kwanza iliyoitwa NDOA HAINA DOA,ambayo ilionekana kukubalika kwa jamii,kama vile haitoshi Haroun ameangusha tena singo yake ya pili inayoitwa HAINA NGWASU ambayo inaonekana kufanya vyema kwenye vituo mbalimbali vya redio hapa bongo.

Akizungumza kwa njia ya simu na JIACHIE leo mchana Haroun amesema ule ulikuwa mwanzo tu, na sasa amekwishikamilisha albamu yake yenye jumla ya nyimbo 12,amesema albamu yake inatwa NDOA HAINA DOA,ambayo amewashirikisha wasanii mbalimbali wakali akiwemo Q-J,Lina kutoka Machozi band,Wanaume TMK Halisi,Juma Nature,Luteni Kalama,Hussein Machozi,Tekla pamoja na Ray C.

Haroun amesema kuwa anatarajia kuizindua albamu hiyo mnamo februari 21,na sokoni itakuwa imeingia mapema mnamo februari 2.Amesema kuwa mbali ya uzinduzi wa albamu yake pia atatambulisha mavazi na nembo/logo mpya ya 555 gear.

"kwa sasa nipo kwenye maandalizi makubwa ya kurekodi video ya zile singo zangu mbili ambazo nilikwisha zitambulisha hapo awali,hivyo wapenzi na wadau wangu wakae mkao wa kula nakuja kivingine mtu wao",alisema Haroun
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, January 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

au mnasemaje wadau?


Maisha ya Mtanzania yako mikononi mwake kiukweli,vinginevyo hutoki au mnasemaje wadau
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, January 28, 2009 | | Permalink | Maoni 1

kikwangua anga cha kampuni ya nanihiii


Kikwangua anga kingine cha kampuni ya nanihii kikapandishwa taraatibu,ebwanaee bongo imecharuka kwa vikwangua anga si mchezo
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, January 28, 2009 | | Permalink | Maoni 5

pamoja na kupigwa marufuku.!


Pamoja na kupigwa marufuku na serikali,lakini bado mabango ya matangazo yao yamejaa tele mitaani likiwemo hili kama lilivyonaswa na kamera ya Jiachie leo mchana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, January 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

rais jk amtembelea athuman Hamisi


Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali mpiga picha wa magazeti ya Serikali ya Daily News na HabariLeo, Mpiganaji Athuman Hamisi Msengi, wakati alipomtembelea kwenye Hospitali ya Milpark ya mjini Johannesburg, Afrika Kusini jana baada ya kikao cha wakuu wa nchi za SADC. Mpiganaji Hamisi amelazwa baada ya kupata ajali ya gari huko Kibiti, Mkoa wa Pwani, takriban miezi mitatu ilopita na kupata majeraha kwenye shingo na uti wa mgongo. Hali yake inaendelea vizuri japo maungo bado hayafanyi kazi sawasawa. Picha na mdau Juma Kengele wa Ikulu
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, January 28, 2009 | | Permalink | Maoni 0

albamu ya shangwe yazidi kununuliwa kama njugu

Tuesday, January 27, 2009

Hii ndio kava ya album ya SHANGWE 2008 yenye CD mbili ambapo kila moja ana jumla ya nyimbo 15, ndani ya album hii ina Biography ya wasanii mbalimbali walioshiriki kuikamilisha albamu hiyo,wasnii hao ni kama vile AY, Lady JD, Mwana FA, Joe Makini, Afande Sele, Q. Chilla na Chidi Benz.


SHANGWE CD 1.
1. Uko juu – Lady Jay Dee ft, Chidi Benz
2. Taxi Bubu – Matonya ft, Fid Q.
3. Nipe Deal – Mangwea ft, Dark Master
4. Ngoma Itambae – Chidi Benz
5. Linawachoma – Bushoke
6. Price Waweru – Ali Kiba ft, Mwasiti
7. Ningejua – PNC
8. Wakibana Sana – Ferooz
9. Tatu Bila (RMX) – Wanaume Halisi
10. Mama Mia – Q. Chief ft, Mangwea
11. Njoo – Prof. Jay ft, Kleptomaniax
12. Ni Aje ni Vipi – Joe Makini ft, Nick
13. Nibebe – H.Baba ft, Pasha
14. Piece & Love – Ins. Haron
15. Nasema Nao – AY ft, Chameleone

SHANGWE CD 2.
1. Tunaonana Wabaya – Q.Chief
2. Nihurumie – Ray C ft, Chidi Benz
3. Bado nipo nipo – Mwana FA
4. Mbele yako, Nyuma yangu – Afande Sele
5. Mwaah – Nizzo
6. Bila wewe – Kassim
7. Mapinduzi – Prof. Jay ft, Ngoni
8. Mida Mibovu – Mangwea, Jay Moe, P-Funk
9. Shangwe – Watoto wa Maghorofani
10. Watasimuliwa – Dully Sykes
11. Wakinuna – Mr. Nice
12. Kukaa Nyumbani – Juma Nature
13. Bounce – Jay Moe
14. Kila Kipindi – Ferooz
15. Usiende kwa Mganga - Kassim

Kwa mawasiliano zaidi ukihitaji albamu hiyo wasiliana na Balozi wa Prime Time Promotions kwa namba 0784 318032 au 0715 318132 au wasiliiana na Dj Mully B wa Clouds Fm kwa namba 0754 747024
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, January 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

la kagoda si gumu,nani alichukua fedha benki ?


Toleo hili lina habari nyingi na za kina na nyingine za kudodosa tu. Tunaamini tutakuwa chombo cha kwanza cha habri kuuliza swali sahihi kuhusu Kagoda badala ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa kwa muda mrefu. Tunaamini majibu ya swali hilo ndiyo yanashikilia ufunguo wa nani yuko nyuma ya Kagoda. Pia tunatafakari kauli ya Waziri Mkuu kuhusu mauaji ya Albino na pia tunagusa mada nyingine nyingi na habari nyingine kem kem.

Tuendelee kuwa pamoja.

Twende na tuwe Cheche
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, January 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Ras Makunja wa "THE NGOMA AFRICA BAND" kumpeleka" Mama Kimwaga"



Wazee wa baraza wa mji wa Tampele,Ufini! kusikiliza malalamiko ya Ras Makunja !juu ya mchezo mchafu wa "Mama Kimwaga" sijui wazee watahamua vipi? juu ya malalamiko hayo!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, January 27, 2009 | | Permalink | Maoni 3

Karibu TanzaniaYetu.com

Salaam,
Tunakukaribisha www.TanzaniaYetu.com ambapo tovuti zote zinazohusu
TANZANIA zinaandikishwa bure.
Wako,
Uongozi,
www.TanzaniaYetu.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, January 27, 2009 | | Permalink | Maoni 0

ama kweli duniani kuna mambo.!

Monday, January 26, 2009
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 2

filamu ya mwanzo mpya ya tht iko juu


Pichani ni baadhi ya wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ya mwanzo mpya ambayo imepokelewa vyema kwa jamii na hata sokoni kwa ujumla

Taasisi ya kukuza na kuendeleza Vipaji vya wasanii wachanga, Tanzania House of Talent ‘THT’, tayari imeingiza sokoni filamu yao mpya inayojulikana kwa jina la MWANZO MPYA, ambayo imewashirikisha nyota kibao wakiwemo wasanii wenye uwezo wa kutosha.

filamu hiyo ikiwa imefanyika kupitia Kampuni ya Bani Vision, inafanya vyema sokoni tangu ilipoingizwa siku chache zilizopita.Ndani ya filamu hiyo wamo washiriki mahairi kama vile Banana Zorro, H. Baba na Dj Mully B ambaye pia ni mtangazaji maarufu wa Redio Clouds FM.

Mratibu wa Maonesho na Masoko wa THT, Michael Nkya, amesema kuwa filamu hiyo pia imewashirikisha wasanii chipukizi wanaotisha ndani ya tasnia hiyo ambao ni Islam Awadh, Kauye Dotto, Stephen Joseph (Jobiso) na Msami, ambao wameonesha uwezo wao mkubwa wa kuigiza na ujuzi wa kutosha yakiwemo yale waliyofundishwa na waalimu wao.

“Maudhui ya filamu hiyo yanagusa maeneo mengi yakiwemo Mapenzi, Ushirikina, Umuhimu wa Urafiki, Usaliti na mambo mengi kibao, nawataka Watanzania waichungulie ili wajifunze mambo mengi zaidi, ikiwa ni pamoja na kupata burudani,” alisema
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 2

mkubwa fella aja na singo yake kuleta heshima


Anaitwa Said Fella lakini unaweza ukaanza kumuita kwa jila la Mkubwa Fella nae bila hiyana huitika kwa bashasha kabisa.Kwa wale wasiomfahamu vyema ni yule meneja wa kundi la Wanaume TMK Familly lenya makao yake makuu kule kule Temeke jijini Dar.

Mkubwa Fella amenitonya hivi punde kwa njia ya simu kwamba ameingia studio ya Sound Crafterz kwa ajili ya kurekodi singo yake ya kwanza itakayoitwa 2009.Amesema kuwa anataka kuwaonesha baadhi wasanii ambao wamekuwa wakimfuata wakati wa shida na kusaidiwa, wakishiba wanakuja na maneno ya kashfa na kiburi kama baadhi ya wasanii wengine ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa maneno ya hapa na pale.

"Nataka kuwaonesha baadhi wasanii kuwa hata mimi na naweza,ili kuthibitisha hilo wakae mkao wa kula nakuja na singo yangu ya kwanza itakayoitwa 2009, sasa nipo studio ya Sound Cfafters kwa ajili kurekodi hiyo singo,ambayo anaamini itawashtua wengi,kwamba aalahh hata Mkubwa Fella anaweza"alibainisha Mkubwa Fella
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 1

benki ya wanawake kuanzishwa nchini


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa MARGRETH SITTA amesema wizara yake inaendelea na mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya wanawake TANZANIA ili benki hiyo ianze kutoa huduma zake kuanzia mwezi ujao wa Februari.

Amesema benki hiyo itakuwa ikitoa huduma zake katika jengo la BENKI YA POSTA, lililopo katika mtaa wa MKWEPU, jijini DAR ES SALAAM.

Waziri SITTA ameyaeleza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kuhusu mafanikio ya wizara yake Mheshimiwa waziri SITTA amesema ongezeko kubwa la ushiriki wa jamii na taasisi katika masuala ya maendeleo ya jamii,uzingatiaji wa Usawa wa kijinsia na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanawake nchini ni moja ya mafaniko makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa shughuli za wizara yake kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Amesema hata hivyo wimbi kubwa la vitendo vvya ukatili wa kijinsia vinavyoripotiwa katika sehemu mbalimbali nchini vinaathiri juhudi za serikali katika kuboresha suala zima la hali ya maisha ya familia na maendeleo ya jamii yote kwa ujumla

Waziri SITTA amesema katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na maendeleo hapa nchini, ni lazima kuondoa vikwazo vinavyozuia kundi moja kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo kutokana na ukatili wa naotendewa.

Amevitaja vitendo vya ukatili wanavyofanywa wanawake na watoto kuwa ni kukatwa viungo,, ubakaji, vipigo, ukeketaji na hata mauaji.

Amesema kuwepo kwa vitendo hivyo kunaathiri maendeleo ya jammii kwani watu wengi wanaathirika kiafya na kisaikolojia na hivyo kushindwa kushiriki kikammilifu katika shughuli za ujenzi wa taifa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 2

TAARIFA YA MWENYEKITI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – CHAMA CHA WANANCHI) KATIKA KUMBUKUMBU ZA MAUAJI YA JANUARI 2001



“Serikali ya Jamhuri ya Muungano Iseme: “Basi” kwa Ukandamizaji wa Haki za Binaadamu!”


Wapendwa Wanahabari na Watanzania Wenzangu,

Leo ni tarehe 26 Januari 2009. Miaka nane iliyopita, siku ya leo ulikuwa ni mwanzo wa mauaji ya kutisha yaliyofanywa na Vyombo vya Dola vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi wasiokuwa na hatia. Mauaji hayo yaliambatana na matendo mengine ya uvunjaji wa haki za binaadamu kama vile kupigwa kwa raia, kuwekwa ndani bila ya makosa, kubakwa kwa wanawake na kuibiwa mali za raia. Mpaka maafa haya yanamalizika, tayari Watanzania wapatao 70 walishapotezewa uhai wao, mamia wakiachwa na vilema vya maisha, mamia wakitiwa umasikini kutokana na ama kuibiwa au kuharibiwa kwa mali zao na maelfu ya wengine wakiwa wakimbizi nje ya mipaka ya Tanzania.


Wapendwa Wanahabari na Watanzania Wenzangu,

Hakuna fakhari yoyote kuyakumbuka na kuyakumbushia matukio haya machafu katika nchi yetu ambayo yaliiacha historia iliyotukuka ya Tanzania ikiwa imejeruhika vibaya. Watanzania waliopoteza maisha yao, viungo vya miili yao, ndugu na jamaa zao, na; zaidi ya yote; waliopoteza heshima yao kutokana na ukandamizaji ule uliofanywa na Vyombo vile vile vya dola ambavyo vilitarajiwa kuilinda nchi hii na watu wake, hawana la kufidiwa kwa hayo yote. Na hao ni sote sisi kwa umoja na wingi wetu. Maafa ya Januari 2001 yalikuwa ni aibu kubwa kwa taifa letu na yataendelea kubakia kuwa hivyo daima.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inachukuwa dhamana ya yote yaliyotokezea; na sasa – wakati tukiyakumbuka maafa hayo, tuna wajibu wa kutazama nyuma na kukitathmini kile kilichotokea katikati (baina ya mwaka 2001 na 2008) na kuona ikiwa kweli sote, kama taifa, tulijifunza chochote kwa maafa haya na ikiwa pana dhamira ya kweli ya kutokuyarudia tena yale yale.

Wapendwa Wanahabari na Watanzania Wenzangu,

Inafahamika kuwa chanzo cha maafa yale ni chaguzi zisizozingatia haki, uadilifu na usawa ambazo zimekuwa zikiendeshwa na Tume zetu za Uchaguzi tangu kuanzishwa tena mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Uchaguzi wa mwanzo wa 1995 ulitawaliwa na mapungufu ya makusudi na ukamalizika kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kulazimisha ushindi kwa mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Salmin Amour. Uchaguzi wa pili wa 2000 sio tu ulikuwa na mapungufu bali pia ulivuuka hata vipimo vya chini vya chaguzi, kiasi ya kwamba waangalizi wa ndani na nje waliuita ‘aibu kwa demokrasia.’ Uchaguzi wa 2005 nao ulifuata mkondo wa chaguzi mbili zilizotangulia.

Maandamano ya amani ya Januari 27, 2001 yalikusudiwa yawe ni kielelezo tu cha wananchi kupaza sauti zao kuonesha kutoridhishwa kwao na namna ambavyo ZEC ilikuwa ikidharau matakwa yao . Matakwa ya wananchi – na ya kikatiba – ni kwamba uongozi wa nchi upatikane kwa njia ya uchaguzi huru, haki na adilifu. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikajibu kilio hicho kwa mtutu wa bunduki na uvunjaji wa haki binaadamu.

Kutokana na maandishi yake, Muafaka uliofikiwa baina ya vyama vya CUF na CCM baada ya maafa haya, ulikusudia kukimaliza kabisa – kama si kukizika – chanzo cha maafa hayo – ukosefu wa demokrasia na uchaguzi usioakisi matakwa ya wananchi. Lakini kwa kuwa CCM ilihisi kuwa utekelezwaji wa Muafaka huo haukuwa na maslahi kwake, viongozi wa Serikali (ambao ndio hao hao wa CCM) wakaanza kuuhujumu hatua kwa hatua na hatimaye wakauvunja kabisa na kufikia mwaka 2005 hapakuwa tena kitu kinachoweza kuitwa Muafaka kwa upande wa CCM.

Hii ni kusema kwamba CCM haikujifunza hata kidogo kwa yale ambayo Serikali yake iliyafanya mwaka 2001. kiwango cha uvunjwaji wa haki za binaadamu, kujenga khofu kwa raia na mateso yalikuwapo kutoka ama kwa vyombo vya dola moja kwa moja au kutoka kwa makundi ya Janjaweed, ambayo yanamilikiwa na CCM.

Matokeo yake ni kuwa uchaguzi wa 2005 nao ukaongezea hisabu ya chaguzi zetu zisizokidhi vigezo vya kidemokrasia. Na tena, kila ushahidi ulikuwa unaonesha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilikuwa tayari kutumia tena mabavu dhidi ya raia pindi raia hao wangeamua kuingia barabarani kudai haki yao iliyoporwa. Kilichozuia maafa yasitokee mwaka 2005 ni busara za hali ya juu za uongozi wa CUF na sio utotayarifu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wakati huo ikiwa chini ya Uamiri Jeshi Mkuu wa Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

Wapendwa Wanahabari na Watanzania Wenzangu,

Miaka nane sasa baada ya Maafa ya 2001, na bado Tume za Uchaguzi zimeendelea kujenga mazingira ya kutokuwa na chaguzi za haki, huru na adilifu. Kwa mfano, katika mwezi wa Disemba 2008, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alitoa taarifa inayoonesha kuwa tayari ZEC imeanza kushirikiana tena na vyombo vya dola kuhakikisha kuwa inapandikiza wapiga kura katika kisiwa cha Pemba ili waje waisaidie CCM katika chaguzi zinazokuja.

Itakumbukwa kuwa kisiwa cha Pemba kiliathirika zaidi na maafa ya Januari 2001 kutokana na ukweli kuwa wananchi wa huko, kwa wingi na umoja wao, wamekataa katakata kuiunga mkono CCM tangu mageuzi ya siasa yaanze miaka 17 iliyopita. Mkakati wa CCM ni kulazimisha kuwa inapata viti vya ubunge na uwakilishi kutoka kisiwa hicho na tuna ushahidi wa kutosha namna ZEC inavyoyaandaa mazingira hayo. SMT, CCM na ZEC hawakutosheka na maafa ya Januari 2001 na sasa wanaandaa janga jingine, ambalo lazima Watanzania walipinge na walizuie kwa nguvu zao zote.


Mambo kama hayo yameendelea katika chaguzi ndogo mbali mbali zilizowahi kufanyika Tanzania Bara: ule wa Tunduru wa 2007, wa Tarime wa 2008 na wa Mbeya Vijijini wa 2009. Kiwango cha utumiaji mbinu na hila chafu kutoka Tume za Uchaguzi na pia maguvu ya vyombo vya dola hakioneshi kabisa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria demokrasia na, kwa hivyo, kuwa imejifunza kutokana na maafa iliyosababisha Januari 2001.

Wapendwa Wanahabari na Watanzania Wenzangu,

Sisi Chama cha Wananchi (CUF) tunachukua fursa hii kuungana na kila raia wa nchi hii kuomboleza maafa haya ambayo yameendelea kuwa aibu kubwa kwa taifa letu. Tunawahakikishia kwamba hichi ni chama cha siasa chenye dhamira ya kutumia njia za kistaarabu kufikia lengo la pamoja la kitaifa – yaani kuwa na Tanzania imara kiuchumi, kisiasa, kijamii na kitamaduni. Tunaamini katika uhuru wa binaadamu na demokrasia kama njia pekee za kufikia lengo hilo la kitaifa.

Kwa hivyo, wakati tukiungana pamoja kukumbuka msiba huu mkubwa kwa taifa, tunatoa wito kwa, kwanza, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , iseme: “Basi, imetosha!” Basi, kuwakandamiza raia wanapodai haki zao. Basi kutumia vyombo vya dola kwa maslahi ya kisiasa. Basi kujenga jamii yenye khofu kila inapokaribia na wakati wa uchaguzi. Pili, tunatoa wito kwa Tume za Uchaguzi zote mbili – NEC na ZEC – kwamba nazo ziseme basi kusimamia na kuendesha uchafuzi wa haki ya raia kuchagua viongozi wanaowataka na badala yake wasimamie na waendeshe uchaguzi utakaoakisi matakwa ya Watanzania.

Kwa kutumia maneno ya Mstaafu Mkapa, ambayo kwa bahati mbaya hakutaka kuyatimiza kwa makusudi, “ Tanzania ni yetu sote…Hakuna mwenye hati miliki ya nchi hii.” Hatimiliki ya Tanzania ni ya Watanzania wenyewe. Ni vyema Serikali, kama taasisi iliyopewa dhamana ya kusimamia hatimiliki hiyo, kuona kuwa haki za mwenye mali (Mtanzania) zinachungwa, kuheshimiwa na kudumishwa. Na kigezo kimoja cha kuhakikisha hilo ni kuwa na chaguzi huru, za haki na wazi. Huo ndio wajibu wa SMT na Tume zetu za Uchaguzi.


HAKI SAWA KWA WOTE


PROF. IBRAHIM H. LIPUMBA

MWENYEKITI,

CUF – CHAMA CHA WANANCHI
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 0

askari wa JWTZ amuogesha dereva wa school bus



Hiyo picha nimetumiwa na mdau, naomba tuiwakilishe hivyo
hivyo japo haionekani vizuri:-

"Kaka naomba uiwakilishe hii picha ya askari wa JWTZ aliyemuogesha
dereva wa school bus pale kawe darajani kwa komba asubuhi ya leo baada
ya kumwagia maji viatu vyake ambavyo anadai alivipiga kiwi leo asubuhi.
Haya sio ya kusikia nimeyaona kwa macho na watu wadau wengine pia
alishuhudia. Hebu tuulize wana jamii; Mlinzi wa wananchi anapofanya kitu
hii wewe unapata picha gani?" Nawakilisha

NB:Wadau mimi kama kawaida yangu ya ujumbe,si mnajua mjumbe hauwawigi
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 3

bongo mvua kiduuchu mtafutano


Bongo bwana mvua kiduuchu tu balaa kila mahali,Mvua ya kiasi imenyesha leo asubuhi jijini Dar,lakini adha ya msongamano wa magari na mifereji ya maji machafu kujaa imekuwa kero kubwa sana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 0

kikwangua anga kimesimama


Kila kukicha vikwangua anga vinazidi kuongezeka ndani ya Bongo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 1

kp leo

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 0

MAUAJI YA ALBINO - DHAMBI YA UBAGUZI WA RANGI TANZANIA

TANZANIA NA DHAMBI YA UBAGUZI WA WA RANGI

Nimekaa na kufanya tafakuri ya kina kuhusiana na mauaji ya ndugu zetu zeruzeru (albino) yanayoendelea kuisakama Tanzania. Katika tafakuri yangu hiyo nimejaribu kuangalia mambo makubwa mawili, suala la kwanza ni dhana nzima ya ubaguzi wa rangi (racism/racial discrimination). Na suala la pili ni mauaji yenyewe ya zeruzeru.

Lengo la kutaka kuchukua dhana hii ya ubaguzi na vitendo vya mauaji ya zeruzeru ni kutaka kuangalia kama mauaji haya na manyanyaso haya ni muendelezo wa dhambi ya ubaguzi wa rangi au ni “uonevu” tu kama wanasiasa na viongozi wetu wasemavyo.

Binafsi nijuavyo ubaguzi wa rangi si suala la kusema huyu mweusi (Black) au huyu ni mweupe (Mzungu), na huyu ni wa rangirangi (coloured). Ukiangalia ubaguzi wa rangi uliokuwepo Afrika Kusini kipindi cha makaburu, watu walipangwa katika makundi kutokana na rangi zao, mweusi, mweupe na wa rangirangi. Na kila kitu lilipata “benefits” zake. Katika katika kumbi za starehe kulikua za watu weupe ambapo mtu mweusi haruhusiwi kuingia, na kuna sehemu zingine hata kutembea mweusi hakuruhusiwa akikamatwa na kufungwa jela na kipigo kikali. Pia ubaguzi kama huu ulikuwepo katika nchi nyingi za magharibi. Mtu mweusi hakuruhusiwa kukaa baadhi ya viti ndani ya basi, nakumbuka nimeona picha ambazo zikiandika ONLY BLACKS AND DOGS HERE. Hii ilikua hatari sana kwani mtu mweusi alinyimwa haki zake kutokana na rangi yake ya ngozi.

Baada ya kuangalia hayo yaliyotokea Afrika Kusini na nchi za magharibi kuhusiana na ubaguzi wa rangi. Nikaanza kuangalia maana halisi ya ubaguzi wa rangi ni nini. Je, ubaguzi wa rangi ni suala la kusema mtu huyu ni mweusi, mweupe, au wa rangirangi tu? La hasha, ni lazima mtu apangwe kutokana na rangi yake, na rangi hiyo imfanye au anakosa haki zake za msingi kutokana na rangi hiyo. Na hata ukisikiliza kwa makini I HAVE A DREAM SPEECH ya Dr. MLK Jr, ilikua inaweka wazi kuwa walichokua wanataka ni mtu kuthaminiwa utu wake, mtu kutambuliwa kwa afanyayo na uwezo wake na si rangi yake imfanye akose mambo ya msingi, ateswe, atengwe nk. Leo hii tumeshuhudia ndoto ya Dr. MLK Jr, imetimia…sit u kwa Obama kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani, la hasha bali watu katika mataifa ya magharibi wanaheshimiwa, kutambuliwa kutokana na utu wao, uwezo wao wa kufanya mambo na si suala la rangi tena.

Tanzania kwa kipindi hiki inakumbwa na mauaji ya zeruzeru kwa kasi kubwa ya ajabu. Imefika kuwa zeruzeru ameondolewa utu wake, amekua bidhaa adimu na ya gharama kubwa, zaidi ya kipindi cha utumwa. Serikali inachukua hatua mbalimbali, zingine ni za kufurahisha kuwa hazina msingi wowote zaidi ya kukurupuka. Mfano mpango wa serikali kugawa simu za mkononi kwa zeruzeru wote ili wakitaka kukamatwa wapige simu polisi. Sasa najiuliza, je hili suala la simu, je simu hiyo inachajiwa na teknolojia gani?

Maana vijijini napo kuna zeruzeru na huko hakuna umeme, sasa itakuaje? Na pia tayari hizi simu zitakua ni kivutio kingine kwa zeruzeru kuvamiwa kwani kila mtu atajua zeruzeru ana simu, hivyo hata majambazi, wachuna ngozi, na wakata viungo vya zeruzeru kuongeza, huo ni mtazamo wangu tu.Na pia kipindi hiki tumeshuhudia serikali imefuta leseni za waganga wa kienyeji kama suluhisho. Je, ni kweli kama serikali isemavyo kuwa wanaosababisha mauaji ya zeruzeru ni waganga wa kienyeji au hata waendaji kwa waganga hao, hususani vigogo wenyewe wanaotaka vyeo vikubwa zaidi na utajiri mkubwa zaidi. Hili tuliachie hapo.

Ngoja tujiulize hivi zeruzeru (albino) ni mtu gani?Anaweza tambuliwaje kwa muonekano wake? Sintopenda kwenda ndani sana kwenye masuala ya kibaolojia kutoa sababu za kuzaliwa kwa zeruzeru. Kwa kumtambua zeruzeru haihitaji uwe na microscope au elimu kubwa sana ya masuala ya kisayansi. Zeruzeru kwa kumuangalia rangi ya ngozi yake unaweza kumtambua.Zeruzeru ni mwafrika lakini si black kama wengineo, sasa sijui ni wa rangirangi (coloured) au la.

Swala la msingi ni kutaka kujua sasa je, mauaji haya ya zeruzeru nayo yamo katika kundi la ubaguzi wa rangi au la???? Binafsi naamini bila kipingamizi chochote kuwa mauaji haya ya zeruzeru ni ubaguzi wa rangi (racism) kama uliotokea Afrika Kusini, Marekani na nchi zingine za magharibi, lakini huu ni mkali zaidi. Nasema huu ni mkali zaidi kwani umelenga zaidi katika kuondoa maisha ya mwanadamu mwenzake kwa ukatili wa kunyofoa viungo, tofauti na ule wa kumzuia mweusi kutembelea mitaa flani au katika upandaji wa mabasi nk.

Kitu kingine cha kushangaza na kujiuliza, je kwanini Tanzania au watanzania kwa ujumla hatusemi ukweli kuwa mauaji ya zeruzeru ni ubaguzi ili tuweze kupambana nao ipasavyo, na jumuiya za kimataifa ziweze kutoa msaada wake?? Kwa mtazamo wangu, watanzania wengi tumeaminishwa kuwa sisi ni bora kuliko taifa lingine lolote lile kitamaduni na kimaadili…kumbe sio hivyo, si kweli. Kitendo Fulani kikifanywa na taifa mfano la Burundi, Kongo, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani nk tunasema ni ubaguzi wa rangi, unyanyasaji nk..kwa ujumla tunawanyooshea kidole kuwa wamepotoka.

Je, mbona kitu hichohicho kikitokea Tanzania hatutaki kuweka wazi tunaanza kutafuta majina mengine kama unyanyasaji wa albino nk? Au kwani maana ya ubaguzi wa rangi, kitendo ni lazima kifanywe na mtu mweupe (mzungu) dhidi ya mweusi (mwafrika) hususani? Au hata mtu mweusi akimfanyia kitendo cha kumtenga mtu mweupe na kumnyima haki zake, kumnyanyasa kutokana na rangi yake ya uweupe nacho ni kitendo cha ubaguzi? Na kitendo cha mtu mweusi pia kumfanyia kitendo cha kumbagua mweusi mwingine kutokana na rangi yake (mfano mweusi sana/ mweusi tiiii na mweusi Fulani) nacho ni kitendo cha ubaguzi pia au? Au mweupe (mzungu) akimbagua na kumtenga, kumnyanyasa mweupe mwingine kama vile mwarabu, mchina nk nacho ni ubaguzi wa rangi???? Kweli hapa ndio penye kufahamu nini ni nini hasa. Mimi naamini ubaguzi haina maana lazima iwe kwa mweupe afanye kitendo hicho dhidi ya mweusi…lakini mweusi akifanya dhidi ya mweupe au coloured kisitafsiriwe kuwa ubaguzi

Nachojuwa mimi kwa kuangalia baadhi ya matukio yaliyokua yanatokea barani Afrika, mfano kipindi ambacho watu wa Afrika Kusini walipoamua kuwapiga na kuwaua kinyama wahamiaji waliopo kule toka nchi zingine hususani za Afrika, Tanzania ilikua ni nchi mojawapo iliyotoa tamko kali, na kwa uwazi kabisa kutamka “dhambi ya ubaguzi Afrika Kusini bado inawatafuna”. Nikaanza kuangalia mambo mengine ambayo ninayaona huku Marekani, mtu mfano akifanyia kitendo Fulani, akiwa ni mweupe kakifanya, anakimbilia kusema ni ubaguzi wa rangi.

Sasa mimi najiuliza, je endapo mtanzania mweuzi mmoja akaenda nchi yoyote moja ya magharibi kama vile kusoma au kufanya kazi, na mtanzania huyo akauliwa na viungo vyake kunyofolewa kama anavyofanyiwa zeruzeru, je Tanzania itasemaje? Haina ubishi kabisa, kila mtu atasema mtanzania huyo mweuzi kabaguliwa kutokana na rangi yake. Sasa swali la msingi, je kitendo cha zeruzeru kunyofolewa viungo vyake kinyama, na hatimaye kuuliwa na mtu mwenye rangi nyeusi kisa rangi yake ni tofauti na mtanzania mweusi, je kwanini kisiwe kitendo cha ubaguzi wa rangi?Maana zeruzeru naye anatambulika kwa rangi yake ya ngozi, kama ilivyo kwa mweusi mwingine atambuliwavyo.

Kama tupo katika hatua hii tuliyoifikia ya kuweza kuuana kutokana na rangi zetu, moja ni nyeusi, na nyingine ni ya rangi (coloured)..wote ni binadamu, na ni watanzania..tunaelekea wapi wandugu? Hivi imefikia wakati zeruzeru inabidi asitembee peke yake, aitembee baadhi ya mida ikifika hasa jioni maana anachukuliwa kama “bidhaa”. Hadi mbunge maalum ambaye ni zeruzeru anapewa ulinzi binafsi asije uliwa na kunyofolewa viungo vyake. Je, mgombea urais 2010 akiwa ni zeruzeru watu tupo tayari kumpatia urais endapo atakua na sifa zote za kuongoza? Au rangi ya ngozi yake itaendelea kumtafuna kwa kuhesabiwa “bidhaa” muhimu?

Nini kifanyike kuondokana na dhambi hii inayotutafuna ya ubaguzi wa rangi????

TAFAKARI, CHUKUA HATUA DHIDI YA UBAGUZI HUU WA RANGI

NAWASILISHA HOJA

MAKULILO Jr,
www.makulilo.blogspot.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, January 26, 2009 | | Permalink | Maoni 2

haya huyu hapa tena nani ?

Sunday, January 25, 2009
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, January 25, 2009 | | Permalink | Maoni 12

wote wako njema katika fani

Saturday, January 24, 2009

Aliyewahi kuwa moja ya watangazaji wa televisheni ya ITV miaka kadhaa ya nyuma Mussa Taghalile akiwa amepozi na mwanadada Irene Uwoya anaekuja juu ile mbaya katika tasnia ya filamu hapa bongo.Kama utakumbuka Irene ameigiza filamua ya Oprah,Shakira na nyinginezo kibao.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, January 24, 2009 | | Permalink | Maoni 0

vivian steven ndio malikia wa sebene ngwasuma 2009


Mshindi wa malikia wa sebene ngwasuma 2009 Vivian Steven akiwa amenyanyuliwa juu na moja ya mabaunsa kwa usalama wa mimbwende huyo.Wadau kuhusu suala la zawadi waandaaji ambao ni kampuni ya TANVISION kupitia mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo bw.Emanuel Migile amesema kuwa zawadi zote zikiwemo fedha taslim zitakabidhiwa siku ya jumatatu mbele ya waandishi wa habari.Msijari masnepu ya ushahidi mtayaona hapa hapa kaeni mkao wa kujichana tu au sio wana

Mshindi wa shindano la malikia wa sebene ngwasuma 2009 Vivian Steven akiwapungia washabiki na wapenzi wa shindano hilo waliofika kulishuhudia live bila chenga

Mshindi wa shindano la malikia wa sebene ngwasuma 2009 Vivian Steven akipiga picha za pozi na mahojiano mafupi na waandishi wa habari mara baada ya kuibuka kinara wa shindano hilo

Tatu bora ya malikia wa sebene ngwasuma 2009 wakiwa wamepozi kwa pamoja mbele ya kamera za waandishi wa habari

Malikia wa sebene ngwasuma 2008 Ketura Kihongosi akiwa amekumbatiana na mshindi wa malikia sebene ngwsuma 2009 Vivian Steven mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mshindi wa taji hilo kwa usiku ule wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa msasani club jijini Dar

Malikia wa sebene ngwasuma 2008 Ketura Kihongosi akiwa ameketi na taji/crown yake

Malikia wa sebene ngwasuma 2008 Ketura Kihongosi akizungumza jukwaani kabla ya kukabidhi taji kwa malikia mpya wa 2009

Mshindi wa shindano la malikia wa sebene mwaka jana Ketura kihongosi akipanda jukwaani tayari kwa kukabidhi taji kwa mshindi wa mwaka 2009
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, January 24, 2009 | | Permalink | Maoni 0

baadhi waligwasumika kwa nafasi


Rapa mahiri wa bendi ya Fm Academia Kalijo Kitokalolo akiwarusha washabiki kwa ghani zake chenguzi

Kwa washabiki ilikuwa ni full kubanjuka na kungwasumika na kabia kako mkononi bila bugudha yoyote

Ulikuwepo muda wa kujinafasi kwa washibiki kama dada huyu alivyokuwa akijinafasi kwa raha zake kabla ya ile tano bora kutajwa na majaji wa shindano hilo ambao walionekana kuwa makini na kazi yao

wasanii kutoka nyumba ya vipaji ya THT walikuwepo kutoa burudani muruakabisa kama uwaonavyo pichani

Baadhi ya washabiki wa shindalo la malikiwa wa sebene ngwasuma wakilifuatilia kwa umakini
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, January 24, 2009 | | Permalink | Maoni 0

Kutoka mtandao wa Gazeti la MWANANCHI

habari kaka,


JAMANI HII IMEKAA SAWA KWEL;I?KUNA UKWELI NDANI YAKE MAANA KUSEMA KWELI MI INANISHTUA
naomba tafadhali tuwape wadau kujadili hili swala,kwani kama ni kweli basi linatia hofu sana kwa waziri mkuu kutamka maneno kama hayo.

MDAU
THESSALONIKI,UGIRIKI.

Date::1/23/2009
Pinda ataka jino kwa jino
Na Victor Kinambile, Tabora

KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja vikongwe ni hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.

Waziri Pinda, ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na albino, aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuongoza vita hiyo, akisema lina jeshi zuri.
Mauaji ya albino yamekuwa ni tatizo kubwa nchini na hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Pamoja na serikali kutangaza hatua kadhaa za kupambana na wauaji hao, bado matukio ya kuuawa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiendelea kuripotiwa, lakini Waziri Pinda ameenda mbali zaidi katika kukabiliana na tatizo hilo alipotaka wauaji hao wauawe badala ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kauli ya Pinda, ambayo inaweka maswali katika suala la utawala bora, imekuja wakati ambao wananchi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kuua vikongwe kutokana na imani za uchawi.

Akihutubia wakati wa kufungua mkutano wa 16 wa Shirikisho la Vyama vya Kuweka na Kukopa (SCCULT) kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi Umma mkoani hapa, Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea.

Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo.

"Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena)," alisema Pinda huku akiwaacha watu midomo wazi.

Aliviomba vyama vya siasa kushirikiana na wananchi kuhakikisha suala hili la mauji linakwisha kwani wauji "tunaishi nao na ni rahisi kulimaliza iwapo tutakuwa kitu kimoja katika kuondoa kashifa hii ambayo imekuwa mbaya kwa nchi yetu".
Aliuagiza Umoja wa Vijana wa CCM kuhakikisha mauaji hayo yanatokomezwa kabisa, akisema kuwa ni jeshi zuri ambalo likiamua kutokomeza kabisa mauaji ya vikongwe na ndugu zetu maalbino inawezekana.

"Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena," alisema waziri mkuu.

Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya watu wanaoonekana kuwa ni wa "serikali" waliwafuata baadhi ya waandishi wa habari, akisihi suala hilo lisiripotiwe magazetini kwa madai kuwa kauli hiyo ya Waziri Pinda inaweza kusababisha matatizo.

Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kupiga vita mauaji hayo, alitofautiana na Waziri Pinda katika moja ya hotuba zake aliposema kuwa adhabu ya kuua haitofautishi muuaji wa albino na muuaji mwingine na kwamba watakaopatikana na hatia ya kuua albino, atakabiliana na adhabu ya kifo kama ilivyo kwa muuaji mwingine.
Waziri Pinda alionekana kukerwa na mauaji ya albino wakati alipopata taarifa kwamba kuna mama mwingine aliuawa usiku wa kuamkia juzi.

"Nimeambiwa kuwa juzi wilayani Sengerema kuna mama mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi amekatwa mkono na wauaji wakaondoka na mkono huo na tayari mama huyo amekufa," alisema Pinda na kusisitiza kushughulikia wauaji hao.

Akitoa takwimu za mauaji ya vikongwe na malbino alisema mwaka 2003 waliuwawa vikongwe 517, mwaka 2004 waliuawa vikongwe 444, mwaka 2005 (494), 2006 (vikongwe 386), mwaka 2007 (vikongwe 526) na albino sita na mwaka 2008 (vikongwe 526 na albino 28).

Alisema tayari mwaka huu wameuawa albino watatu hivyo kufanya albino na vikongwe waliouawa kufikia kuwa jumla 2,900.

Waziri mkuu ameanza ziara ya siku nne kutembelea mikoa ya Shinyanga, Tabora na Mwanza ili kuhamasisha wananchi watokomeze vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu weye ulemavu wa ngozi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, January 24, 2009 | | Permalink | Maoni 3

nani huyu.?

Friday, January 23, 2009

Ni mwanadada maarufu sana kwa sasa hapa bongo,je unaweza kumtambua kirahisi akiwa amejiachia kihivyo ?
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, January 23, 2009 | | Permalink | Maoni 16

pamoja wanaweza.!


Keisha akiwa na msanii mwenzake kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Mwasiti Shabani

Pichani Keisha akiwa amepozi na wasanii wenzake leo jioni.Toka kulia ni Amin,Mwasiti wa THT,Loveness,Barnabas (THT)pamoja na na dada nanihii
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, January 23, 2009 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu