Maisha Club yateketea kwa moto jioni hii

Sunday, November 8, 2009
Pichani kati ni aliyekuwa akisimamia kiota hicho cha maraha Majay akipewa pole na mmoja wa wadau wa kiota hicho
Mmiliki wa Maisha Club Mama Hellen Sweya akitoka kuangalia moto huo ulivyoteketeza mali zake jioni hii

Spika ikiokolewa
Mlango unavunjwa


Baadhi ya wafanyakazi wa Club Maisha wakijaribu kuvunja ukuta kwa ajili ya kuwarahisishia watu wa Fire kuuzima moto huo uliokuwa ukiendelea kuwaka


Mmiliki wa Club Maisha, Mama Hellen Sweya akipewa pole na baadhi ya watu waliofika eneo la tukio jioni hii
Baadhi ya wafanyakazi wa Club hiyo wakijaribu kuzima moto kwa kuchota maji kutumia ndoo, uliokuwa ukiendelea kuwaka nyuma ya jengo la club hiyo


Gari ya zima moto ikiwa imepaki nje kabisa ya jengo
Baadhi ya vitu vilivyonusurika kuteketea

Baadhi ya vitu vilivyookolewa vikiwa vimewekwa pembeni
Wazee wa Fire wakiendelea kuuzima moto mnamo majira ya saa tisa hivi wakati inelezwa moto huo ulianza tangu majira ya saa saba mchana
Sehemu ya kuingilia ndani ya club na yenyewe kama unavyoiona pichani
Hii ni ile sehemu ya dancing floor ikionekana imeteketea kabisa kwa moto ambao wazee wa Fire walijitahidi sana kupambana nao, lakini ndiyo hivyooo tena.

Mmoja wa wafanyakazi wa zima moto akielekezwa sehemu ambayo moto ulipokuwa ukiendelea kuwaka

Hapa hakuna kilichobaki

Pichani kwa mbele wenyewe wanasema ilikuwa sehemu ya VIP ikiwa kwishnee kabisa, Dah!

Pichani ni sehemu ya mbele karibu na swiming pool ikiwa imeteketea jioni hii

Kiota cha kujiachia cha Maisha Club kilichopo Masaki jijini Dar leo mnamo majira ya saa saba mchana kilianza kuwaka moto, kwa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wamesema kuwa kulikuwapo na ukarabati uliokuwa unaendelea wa vipupwe (AC), kwa bahati mbaya wakati wa ukarabati huo mojawapo ikalipuka kutokana na nyaya zake kugusana, na baadaye moto mkubwa ukazuka katika jengo hilo, imeelezwa kuwa taarifa zilifika kwa watu wa zima moto lakini hawakuwahi kuuzima moto huo kwa haraka kwani kwa asilimia kubwa vitu vilivyokuwemo vilikuwe vimekwishateketea.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, November 08, 2009 | | Permalink |

Maoni: 5

  Tarehe November 9, 2009 7:22 AM Anonymous Anonymous Anasema:
hee jamani mmh jamani ma ahellen sweya angalia mbele mungu atakusaidia kiota kitarudi upya tena kwa kasi ya ajabu kama kimbunga!! haya wadau wenzangu kiota hicho tuombee kirudi tena tuweze kujiachia vilivyo!!
  Tarehe November 9, 2009 11:47 AM Anonymous Anonymous Anasema:
Wewe mdau unanishangaza sana wewe unataka kuingiza vitu vya shetani uvichanganye na mungu?Huyu mama mimi namshauli afanye biashala nyingine tofauti na hiyo biashala ya kupoteza watu,,Hivi wewe uliyesema eti mungu amsaidie apate kiota kipya!! unajua watu waliopotea kutokana ni hiyo nyumba ya huyu mama?Nyumba ilikua imejaa na kila dhambi,na bado kuna zitakazo fuata subilini kidoogo.Uzinzi umezidi ndani ya hizo nyumba.Na mungu ataendere akuziunguza.
  Tarehe November 9, 2009 6:19 PM Anonymous Anonymous Anasema:
Mungu hayupo kabisa na haya mambo ya kuendekeza ufuska kwa kujiita kijivinjari au kujiachia. Mungu hapendezwi hata kidogo. mama, kurudia kujengwa hichi kiota ni kumuonyesha Mungu kuwa hujali au hujaelewa kuwa yeye hataki ufanye hilo unalolifanya na kifuani una msalaba! Hivyo Mshukuru Mungu kwa kukufikishia ujumbe na fungua biashara nyingine kabisa kama shule au zahanati au hata kanisa. Ubarikiwe katika kuupokea ujumbe huu.
  Tarehe November 11, 2009 1:41 PM Anonymous Anonymous Anasema:
Sahihisho, its dance floor not dancing floor
  Tarehe November 12, 2009 6:39 PM Anonymous Anonymous Anasema:
What goes around comes around.... Kuungua kwa kiota hiki baada ya kuwa na raha ya muda mrefu ni sawa sawa na ndoa ya wawili waliokuwa na raha mara wakaachanishwa ndio moto... get the msg old lady and start kushinda kanisani kuokoa uliowaangamiza


Idadi ya watu